UA-45153891-1

Friday, September 6, 2013

MISS TANZANIA 2013 MOTO UMEWAKA


 

CLARA BAYO
 

ALICE ISAACK

 

ANASTAZIA DONALD

 

DAYANA LAIZER

 

DORICE MOLLEL

 

ELIZABETH PERTY

 

ESHYA RASHID

 

GLORY STEPHEN

 

HAPPINESS WATIMANYWA

 

JACLINE LUVANDA

 

JANETH AWET

 

JOYCE SHAYO

 

LATIFA MOHAMED

LINA ALLAN


LUCY CHARLES

 

LUCY JAMES

 

LUCY TOMEKA

NACY MOSHI

 

MARY CHEMPONDA
 

MIRIAM MANYANGANA


NARIETHA BONIFACE

 

NEEMA MALITI

 

NICE JACK HERMAN

 

PHILLIOS LEMI


PRISCA PAUL

 

SABRINA JUMA

 

SALSHA ISDORY

 

SARAH PAUL

 

SEVERINA LWINGA

 

SVETLANA NYAMEYO

Thursday, September 5, 2013

FLAVIANA MATATA ANAVYOENDELEZA UMATATA WAKE

MWANAMITINDO wa Tanzania anayefanya vizuri kwenye kimataifa Flaviana Matata, ameendelea kutamba katika fani hiyo baada ya kuonekana kwenye bango la  mitindo la mbunifu Kenneth Cole nchini Marekani.

Flaviana Matata ambaye alizaliwa mwaka 1988 mkoani Shinyanga, ni mshiriki wa kwanza kutoka Tanzania kushindana katika Miss Universe 2007 na kuwa mshindi wa 6 kati ya washiriki 15. Ameshatokea kwenye  machapisho mengi ya matangazo  ya Sherri Hill, mwanamitindo maarufu wa kimarekani na mfanyabiashara mkubwa ambaye  anatengeneza na kuuza magauni ya washiriki wa mashindano ya urembo na mavazi ya usiku.

Machi 2011 alishinda tuzo ya Arise Magazine kama mwanamitindo wa mwaka kwenye wiki ya mitindo ya Lagos nchini Nigeria. Pia ameuza sura katika majarida ya Dazed & Confused na i-D ya nchini Uingereza, Glass la Marekani na L'Officiel la Ufaransa. Matata pia alishafanya  baadhi ya “modeling runway” kwa bidhaa kama za Mustafa Hassanali,  Vivienne Westwood, Tory Burch, Suno, na Louise Gray na pia  amehusika katika filamu ya Alexander McQueen ya aliyekuwa mwanamitindo wa Uingereza na kwenye tangazo la  kampeni ya Spring Topshop mwaka 2011, bila kusahau shughuri zake nyingi anazofanya kupitia Flaviana Matata Foundation.





Wednesday, September 4, 2013

DIAMOND ADAIWA KUUVUTA KWAKE WIMBO WA DYNA NYANGE

Kufuatia kutoka kwa ngoma mpya ya Diamond Platnumz inayoitwa "Number One"ambayo gharama ya video yake inakaribia shilingi za kitanzania milioni 50, mwanadada aliyeimba wimbo uliopata kusumbua siku za nyuma wa Nivute kwako, Dyna Nyange kaibuka na kudai kwamba mdundo wa ngoma hii ya Diamond ulikuwa wakwake na ulikuwa ni kwa ajiri ya wimbo ambao alikuwa amshirikishe msanii huyo anayejulikana kama Raisi wa wasafi.

Dyna Nyange
Diamond Platnumz
Mtayarishaji wa wimbo-Sheddy Clever

AY AENDELEA KUIWAKILISHA TANZANIA KWENYE TUZO ZA MUZIKI ZA CHANNEL "O"



Kwa mwaka mwingine tena, AY ametajwa kuwania tuzo za muziki za Channel O.Msanii huyu pekee kutoka Tanzania ndiye aliyeingia kwenye tuzo hizo za CHOAMVA 2013 ambazo zinafanyika kwa mara ya 10. AY ametajwa kuwania vipengele viwili kwenye tuzo hizo ambavyo ni MOST GIFTED MALE VIDEO ambapo Video yake iliyoingia inaitwa PARTY ZONE ambayo amemshirikisha MARCO CHALI, pamoja na kipengele cha MOST GIFTED AFRICA EAST na Video yake hiyo hiyo. 
 AY


VIPENGELE VYOTE KWA UJUMLA

MOST GIFTED DUO/GROUP FEATURING VIDEO

TEAR GAS – Wake Up
XTATIC/AKA & PRIDDY UGLY -Hit Em Up
MI CASA – Can’t Get Enough
EME – Baddest Boy
NAETO C FT D’BANJ – Tony Montana (Bad Pass) Remix

MOST GIFTED NEWCOMER VIDEO
MONEOA – Is’bhanxa
LOLA RAE – Watch My Ting Go
KHAYA MTHETHWA – Move
VICTORIA KIMANI – Mtoto
BURNA BOY – Tonight

MOST GIFTED FEMALE VIDEO
ZONKE – Feelings
LIZHA JAMES FT ANSELMO RALPH – Vais Rochar
STL – Stella Stella Stella
TIWA SAVAGE ft DON JAZZY – Without My Heart
TOYA DELAZY – Heart

MOST GIFTED MALE VIDEO
DONALD – Over The Moon
Zeus FT AKA & TUMI – #DatsWasup
WIZKID – Azonto
AY/MARCO CHALI – Party Zone
IYANYA – Flavour

MOST GIFTED RAGGA/DANCEHALL VIDEO
BUFFALO SOULJAH – Basawine
KAAKIE – Too Much
JESSE JAGZ – Murder Dem
P-UNIT FT COLLO – You Guy (Dat Dendai)
RADIO AND WEASEL – Can’t Let You Go

MOST GIFTED HIP HOP VIDEO
AKA – Jealousy
JAYSO & SARKODIE – Pizza & Burger
REASON – Do It Like I Can
IFANI FT BLAKSUGA – Chocolate Vanilla
EL/M.aNIFEST – Hallelujah

MOST GIFTED R&B VIDEO
BANKY W – Yes/No
ANSELMO RALPH – Curticao
DANNY K – Brown Eyes
CHASE – Lonely
VICTORIA KIMANI/M.I – Oya

MOST GIFED AFRO POP VIDEO
THE SOIL FT ZAKWE – Linkomo
SAUTI SOL – Money Lover
2FACE IDIBIA – Ihe Ne Me
THE MUFFINZ – Umsebenzi Wendoda
DAVIDO – Gobe

MOST GIFTED DANCE VIDEO
KCEE – Limpopo
MAFIKIZOLO – Khona
FUSE ODG FT WYCLEF JEAN – Antenna (Remix)
DJ MALVADO FT PETTY – Jamaica
DJ GANYANI FT FB – Xigubu

MOST GIFTED KWAITO VIDEO
L’VOVO DERRANGO FT PROFESSOR – Palesa
PROFESSOR FT OSIKIDO & CHARACTER – Finger Prints
EES – Woza December
KABELO – Impilo
DJ TIRA FT BIG NUZ & JOOCY – Summer Time

MOST GIFTED AFRICAN (WEST) VIDEO
D’PRINCE – Goody Bag
ICE PRINCE – Aboki
R2BEES – Life (WALAAHI)
DBLACK FT JOEY – Vera
CHIDINMA FT ILLBLISS & SUSPECT – Emi Ni Ballar
P-SQUARE – Alingo

MOST GIFTED AFRICAN (EAST) VIDEO
AY/MARCO CHALI – Party Zone
P-UNIT FT COLLO: You Guy (Dat Dendai)
RADIO & WEASEL – Can’t Let You Go
SAUTI SOL – Money Lover
NAVIO – Kata

MOST GIFTED AFRICAN (SOUTH) VIDEO
DAMA DO BLING – My Eish
OSKIDO – Tsa Mandebele
BLACK COFFEE FT ZAKES – Take it All Off
PAUL G FT FABULOUS – Get Control
DJ DIMPLEZ ft L-TIDO & ANATii – We Ain’t Leaving
KHULI CHANA – Hazzadazmove

Saturday, August 31, 2013

LULU ATOA BURUDANI KALI KWENYE UZINDUZI WA "FOOLISH AGE"


 Lulu na Lady Jaydee

MSANII wa Filamu Bongo, Elizabeth Michael 'Lulu', usiku wa kuamkia leo amefanikisha zoezi la uzinduzi wa filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Foolish Age Tukio la uzinduzi huo lilifanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar, na kuhudhuriwa na mastaa kibao wa tasnia mbalimbali hapa Bongo, wakiwemo; Judith Wambura 'Lady Jaydee', ambaye alitumbuiza sambamba na Barnaba na Amini.


Msanii huyo aliendelea pia kudhihirisha kipaji chake cha kuimba baada ya kuuimba kwa umakini mkubwa, wimbo wa YAHAYA wa Nguli wa muziki wa Kizaki kipya Lady Jaydee na kutunzwa na mapedeshee kibao akiwempo papaa Richie Rich.


Uzinduzi wa fikamu hiyo ya kiswahili ambayo ina sub title ya Kiingereza na ambayo haipaswi kuangaliwa na watoto chini ya miaka 16, huku ikiwa imechezwa na wasanii maarufu na wakongwe  kama Elizabeth Michael mwenyewe, Diana Kimaro, Hashim Kambi, Ombeni Phiri na Mzee Jengua ulifanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam.


 Lulu, Mama yake, pamoja na Lady Jaydee
 Lulu na pesa alizotunzwa

Waongozaji wa shughuli hiyo, mtangazaji Double G wa Radio One/ ITV  na mwanadada kutoka Times FM walikuwepo.
 Richie Rich akimwaga noti
Wema Sepetu na Kajala
 Mama na mwanao ni kama chanda na Pete... huyo ni Natasha (kulia) na Bintiye Monalisa.
Mwogozaji wa Filamu za Kibongo, Leah Mwendamseke nae alikuwepo kuangalia kazi hiyo ya Lulu.
 JB Furaha ilitawala 
 Wadau wengi na mashabiki wakifuatilia uzinduzi wa Filamu hiyo

‘BOMU LAUA WANNE BUKOBA’

Mmoja wa majeruhi wa bomu la shule ya msingi Tumaini 1994, Datius Kalokola hospitalini na baada ya kurudi nyumbani

Ni kichwa cha habari iliyotoka kwenye gazeti flani siku ya alhamisi tarehe 1 Septemba 1994, siku moja  baada ya kutokea mripuko wa bomu katika shule ya msingi Tumaini iliyoko Manispaa ya mji wa Bukoba. Ilikuwa  Jumatano  31 Agosti  1994 majira ya saa mbili asubuhi tarehe kama ya leo, tulipowapoteza wanafunzi  wanne huku 85 wakiwa wamejeruhiwa kutokana na ajari hiyo. Nianze kwa kuwakumbuka wenzetu waliotutoka siku hiyo. Mungu azilaze roho zao mahali pema peponi Ibrahim Mebu, Salehe Abdalah, Yusuph Bahati na Emmanuel Joseph.

Tukiwa tumejipanga mistari “parade” tayari kukaguliwa ili tuanze gwaride  kuelekea madarasani, mara nikasikia kishindo kikubwa kilichoambatana na hali ya mtikisiko. Hali iliyomfanya kila mwanafunzi akimbie pasipo kujua jambo gani limetokea. Baada ya kukimbia umbali wa takribani mita 15 kutoka eneo la tukio ghafra nikahisi kuishiwa nguvu mguu wangu wa kushoto, niliposimama na kugeuka nyuma nikaona idadi ya wanafunzi wasiopungua sita wakiwa wamedondoka chini eneo la tukio.Nilipotizama mguu wangu ulikuwa ukitokwa na damu nyingi.Nilipata mshtuko na mshangao mkubwa  huku nikiwaona wanafunzi wengine pia wamejeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao. Walimu walitahamaki wasijue wafanye nini zaidi ya kutuambia wanafunzi tuliokuwa bado tuko ndani ya mazingira ya shule tulale chini. Wakati huo wengi wetu wakiwa hawaonekani kabisa katika mazingira hayo ndani ya muda mfupi wengine pasipokujua kama wamepatwa na majeraha na wengine wakikimbia kuelekea nyumbani kwao huku wakilia sana na damu zikiwatoka.

Nikiwa kwenye gari l a Msalaba Mwekundu na  majeruhi wengine kuelekea hospitali, tulikutana na baadhi ya wanafunzi wakirudi shuleni baada ya kufika nyumbani na kugundua hawako pamoja na ndugu zao ambao walikuwa nao shule moja. Hali ya utulivu ilipotea ghafla ndani ya mji wa Bukoba na hasa kutokana na taarifa zilizowafikia wazazi  wa wanafunzi ambao walikuwa wakijiandaa kwenda kazini na wengine wakiwa tayari wamefika maeneo yao ya kazi. Hakuna mwanafunzi wa shule ya jirani aliyesubiri kupewa ruhusa ya kwenda nyumbani na mwalimu wake hasa pale wanafunzi wa shule ya msingi Tumaini walipoonekana wakipita karibu na shule hizo wakibubujikwa  machozi huku wakiwa na alama za damu kwenye mashati na magauni yao ya shule na wengine wakitoa taarifa kwamba ndugu zao au marafiki zao wamepoteza maisha kwa sababu hawaonekani.
Tukiwa katika chumba maalum kilichoandaliwa kwa ajiri ya kupokea majeruhi wa ajari hiyo, dakitari alimwambia nesi mmoja amtizame mwenzetu ambaye aliletwa akiwa hajitambui.Alikuwa amelazwa chini pembeni yangu. Baada ya nesi huyo kutekeleza agizo hilo kwa kutumia kipimo ambacho alimuwekea kifuani, nilishuhudia mama huyo nesi akimwaga chozi bila kujizuia. Kumbe huo ndiyo ulikuwa mwisho wa kijana mpole Yusuph Bahati amabaye tuliwai kuishi jirani maeneo ya Kashai. Wakati huo nimeshafahamu kwamba kilichotokea ni mlipuko wa bomu.

Jioni ya siku hiyo baada ya kutolewa kwenye chumba cha upasuaji ndani ya Hospitali ya Mkoa  Kagera, nilijikuta ndani ya wodi namba 4 ya hospitali hiyo pamoja na wanafunzi wengine wengi.Wodi mbili za hospitali hiyo ambazo ni wodi namba 4 na namba 5 zilipokea majeruhi wa ajali hiyo na wagonjwa waliokuwa humo kabla ya ajari wakahamishiwa vyumba vingine. Nakumbuka tulilazwa wanafunzi wawiliwawili kitanda kimoja kwa siku hiyo ya kwanza. Kupitia maongezi ya siku hiyo, nikafahamu kwamba wametutoka wenzetu wanne kutokana na ajari hiyo akiwemo Ibrahim Mebu ambaye alifariki papo hapo.Huyu pamoja na mwingine aliyeitwa Salehe Abdarah tulikuwa wote darasa la nne, wakati Yusuph Bahati na Emanuel Joseph wakiwa darasa la tano.

Kutokana na maelezo yaliyotolewa na baadhi ya wanafunzi ,bomu hilo liliokotwa jalalani na mwanafunzi mmoja ambaye hakufahamika  kwa jina, akamuuzia Ibrahimu Mebu shilingi ishirini, wote pasipokujua kama ni kitu cha hatari. Ibrahimu alikaa nalo kwa takribani siku saba akija nalo darasani na kurudi nalo nyumbani kabla halijaripuka.Kilichosababisha bomu hilo kuripuka ni baada ya kulifungua ikiwa ni katika hali ya michezo pasipo kujua ni kitu gani kitatokea.

Shukurani za dhati ziwaendee wafanyakazi wa Hospitali ya Mkoa wa Kagera na Bugando ya Mwanza kwa jinsi walivyojitoa usiku na mchana kuhudumia majeruhi na hasa wale waliokuwa na hali mbaya sana akiwemo Benedict Nshegize. Nawashukuru pia askari wa jeshi la ulinzi waliofika shuleni hapo kuwaonesha wanafunzi aina na maumbo tofauti ya vitu vya hatari kama hivyo ili wanafunzi wasivisogelee pindi wavionapo na ikibidi kutoa taarifa mahali panapotakiwa. Shukurani kwa mkuu wa mkoa aliyekuwepo kwa kipindi hicho Mzee Philip Mangula kwa ukaribu na msaada aliyoutoa, wazazi, walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Tumaini na shule za jirani.

Kama msimamizi wa gazeti tanzu hili la Semadat (Semadat Blog) na mwandishi wa kumbukumbu hii ,nikiwa pia  miongoni mwa waliokuwa majeruhi wa ajari hiyo, natoa shukurani za pekee kwa wazazi wangu, baba yangu mzazi Mzee Felix Kalokola ambaye kwa sasa ni marehemu, mama yangu mzazi Bi.Philotea Kalokola, Baba mkubwa Mzee Petro Buberwa na mjomba wangu maarufu kama  Dr.Lugenga, wa Hospitali ya Mkoa Kagera. Pia namkumbuka babu yangu marehemu Philadelph Kamanzi ambaye aliendesha baiskeli jioni ya siku hiyo, akiwa na huzuni kubwa kutoka Kijijini Kasharu na kufika mjini Bukoba usiku baada ya kupata taarifa ambazo ni tofauti kidogo kwamba bomu hilo limeangamiza wanafunzi wote wa shule ya msingi Tumaini.

Sina cha kuwalipa ndugu  na marafiki zangu mlionipa huduma kwa kipindi cha takribani miezi miwili nikiwa hospitalini hatimaye nikapona na kurudi shule, hata nikaweza tena kuungana na wanafunzi wenzangu kucheza mpira muda wa mapumziko.
Namshukuru Mungu na namuomba awasaidie wanafunzi wote Tanzania, Afrika na Ulimwengu mzima, hasa wa shule za awali na msingi kuepukana na majanga kama haya.

Miaka 7 mpaka 10 baada ya tukio hilo (Kidato cha nne na cha sita)

Saturday, August 24, 2013

MWANA FA, DIAMOND, KALA JELEMIAH, MWASITI, LINEX NA WENGINE KURUDI SHULE MWAKA HUU



WASANII kibao wa Bongo Flava na Hip hop  wamegeukia upande wa elimu na kuitizama kwa jicho la tatu kwa kuimba wimbo wa kuhamasisha wanafunzi na wadau mbalimbali wa elimu kufanya kila linalowezekana ili kutokomeza ziro kwenye matokeo ya mitihani ya ngazi mbalimbali  za elimu kuanzia elimu ya msingi.

Wimbo huo ambao umerekodiwa katika studio ya Tudd Thomas Production, umeimbwa na wasanii wasiopungua kumi ambao ni Linex, Mwana FA, Keisha,na Diamond. Wengine ni Roma, Mwasiti, Kala Jeremiah, Petter Msechu, Maunda Zollo, Linah na Baba Levo.

Mwisho wa ziro na elimu bora ni muhimu kwa kila mmoja ni baadhi ya maneno yanayosikika katika wimbo huo unaoitwa TOKOMEZA ZIRO.

Saturday, August 17, 2013

WIMBO WA SAIDA KAROLI ULIOTUMIKA KAMA SOUNDTRACK KWENYE FILAMU MPYA YA KIAMERIKA.

WIMBO UITWAO MARIA SALOME WA SAIDA KAROLI UMETUMIKA KWENYE FILAMU MPYA YA KOMEDI HUKO AMERICA IITWAYO PEEPLES.


Basiga bamwita Salome leba.............................!!!!!!!!!!!!!!!!

Thursday, August 8, 2013

WANAMUZIKI 10 BORA KWA UTAJIRI BARANI AFRIKA

1.YOUSSOU N'DOUR-Senegal
2.P-SQUARE-Nigeria
3. D' BANJ-Nigeria
4.KOFFI OLOMIDE- DRC
5.SALIF KEITA-Mali
6. FALLY IPUPA-DRC
7. 2FACE IDIBIA-Nigeria
 8. HUGH MASEKELA-South Africa
9. BANKY W-Nigeria
10.JOSE CHAMELEON-Uganda