UA-45153891-1

Saturday, October 12, 2013

MSHINDI WA BIG BROTHER AFRICA (BBA) DILLISH MATTHEWS ALIPOKUWA MDOGO


 



Oktoba 11, 2013 ilikuwa siku ya kimataifa ya mtoto  wa kike ambapo mataifa yote hutumia siku  hiyo kutangaza na kuhamasisha haki za watoto wa kike na kutokomeza ubaguzi wa kiuchumi, kijamii na kisiasa.  Taifa lolote linaweza kuendelea kama mtoto wa kike atapata nafasi ya kushiriki kwenye nyanja zote.

Masaa machache kabla ya siku hiyo, kaimu barozi wa Marekani nchini Tanzania ametoa wito kwa watanzania kila mmoja achague mtoto mmoja wa kike atakayemsaidia ili afikie upeo wa uwezo wake kwa kuongea nae, kushirikiana nae na kutambua vikwazo alivyonavyo. Aliendelea kusisitiza kwamba, mtoto wa kike anapoendelea, taifa zima linaendelea.

Thursday, October 10, 2013

FAHAMU UBUNIFU NA HISTORIA YA MASOUD KIPANYA KATIKA SANAA YA UCHORAJI NA HABARI

Masoud Kipanya

Msanii Ali Masoud maarufu kama ‘Masoud Kipanya’ ambaye kwenye ukurasa wake wa facebook anajitambulisha ‘Political Cartoonist’ kama kazi yake ya kwanza, anajulikana kama mchora katuni maarufu nchini na  mtangazaji wa redio na TV ambaye aliwai kufanya kazi kwenye kituo cha redio cha Clouds FM. Jina lake lilitokana na muonekano wa katuni anayotumia, wenye sura ya panya. Mbali na shughuri hizo pia ni mbunifu katika fani ya mitindo na mtayarishaji wa vipindi.

Alizaliwa tareha 23 Juni 1972 jijini Dar es salaam na kuanza kazi hiyo ya sanaa akiwa shule ya msingi. Kazi yake ya kwanza ilichapishwa kwenye jarida la Heko mwaka 1989, baada ya hapo alifanya kazi kama mhariri wa katuni kwenye gazeti la Sanifu na mhariri mtendaji wa katuni gazeti la majira, pia katuni zake hutokea gazeti la Mwananchi.

Ameshiriki maonyesho mbalimbali Tanzania na Afrika Kusini kama mtaalam wa matumizi ya rangi ‘Painter’ na amejishindia tuzo nyingi ikiwa pamoja na tuzo ya kwanza ya katuni Afrika Mashariki. Pia alishiriki mashindano ya sanaa ya uchoraji yaliyoandaliwa na Friedrich Ebert Stiftung na kupata nafasi ya kutembelea nchini Japan kwenye program ya wiki mbili ya maonyesho ya kimataifa ya utamaduni yaliyoandaliwa na ‘Japan Foundation’.

Ndiye mbunifu wa vipindi vya Televisheni vya ‘Maisha Plus’ na ‘Inawezekana’ pamoja na taasisi binafsi ya  ‘Inawezeka Foundation’. Pia ni CEO wa kampuni ya KP Media.

Kufahamu wachoraji wengine wa katuni, tembelea: bongotoons

Masoud Kipanya Cartoon  @facebook.com



Wednesday, October 9, 2013

WIKI YA KIMATAIFA YA HUDUMA KWA WATEJA -OKTOBA 7-11



Ni  wiki inayosherehekewa duniani kote  kwa kutambua  umuhimu wa huduma kwa wateja na kuwazawadia watu ambao hutoa huduma bora kwa wateja wao. Makampuni na waajiri wengi hutumia fursa hii kuwapa motisha wafanyakazi na kuwaunganisha ili kuendelea kuwapa moyo wa ushirikiano. Kwa mwaka huu 2013, wiki hii imeanza Oktoba 7 na itamalizika Oktoba 11.

Kuna namna mbalimbali za ubunifu  kuifanya wiki hii ikumbukwe na wafanyakazi  ikiwa ni pamoja na kauli mbiu na matukio. Hivi ndivyo ilivyokutwa kwenye mtandao maalum uliobuniwa mahsusi kwa ajiri ya watu wenye mapenzi mema na wiki hii. Unaitwa "THE OFFICIAL CUSTOMER SERVICE WEEK SITE". www.csweek.com



Monday, October 7, 2013

2FACE IDIBIA NA ANNIE, NAMELESS NA WAHU, NDOA ZA WASANII ZINAZOUENZI UTAMADUNI WA KIAFRIKA

2Face na Annie wakati wa harusi yao


Ni miongoni mwa familia za wasanii maarufu barani Afrika. Staa wa wimbo wa "African queen" 2Face Idibia wa Nigeria, alifunga ndoa na muigizaji wa Nollywood Annie Macaulay  Mei 2, 2012 na kisha kufanya harusi ya kiutamaduni iliyofanyika kijijini kwao Eket, Machi 8, 2013,  ikihusisha mavazi, vyakula na burudani za utamaduni wa asili yake.

 Nameless na Wahu


Nameless ambaye  ni mwanamuziki wa Kenya aliyetamba sana na wimbo wa "Nasinzia", pia anautangaza vema utamaduni wa Afrika, yeye na mke wake Wahu ambaye pia ni mwanamuziki na mwanamitindo.

Sunday, October 6, 2013

ALLAN LUCKY- MTANGAZAJI WA TELEVISHENI, MWANAMASOKO , MUIGIZAJI, MWANATEHAMA NA MWANAHARAKATI WA MAENDELEO YA ELIMU TANZANIA



Ni maarufu kama “RAISI WA WANAFUNZI”.  Alikulia katika ulimwengu  wa taaluma huku akitamani kuitumia taaluma yake kwenye shughuri za habari zinazolenga kuwakomboa vijana kielimu.

Safari yake ilianzia shule ya msingi Majimaji,  Songea  mkoani Ruvuma kabla hajahamia shule ya msingi Luhira ambako ndiko alikohitimu elimu hiyo mwaka 1998. Aliendelea na elimu ya sekondari  ya “O Level” katika shule ya sekondari Ruvuma  na kufauru kwa daraja la kwanza “Division one, akiwa na  alama ya ‘A’  katika somo la Jiografia,  hivyo akachaguliwa kuendelea na masomo  ya  “A Level” katika  shule ya Sekondari  Minaki  mchepuo wa EGM.  Akiwa amefauru mtihani wa kidato cha sita kwa daraja la pili “Division two”, alijiunga na Chuo cha usimamizi wa fedha  ( IFM) mwaka 2005 kusomea ‘Computer Science’  na kuhitimu  mwaka 2008,  ndipo  akaanza kuzitafuta nafasi za kuonyesha uwezo wake katika taaluma na ubunifu  wa hapa na pale.

Kipindi akiwa masomoni tayari alikuwa ameanza kushiriki matukio mbalimbali kama usimamizi wa miradi na utangazaji, ukiwemo mradi wa mawasiliano wa  ‘Intergrated Communications’,  ‘Whitedent Schools Dental Check-up’ mwaka 2005, ‘Safari Pool Shoot Out’ mwaka 2005 na 2006, ‘Coca Cola Olympic Torch Relay (OTR)’ mwaka 2008 pamoja na ‘Whitedent School Quiz’ ambapo yote ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Aliamini anaweza kuwa mtangazaji mzuri wa TV na ndipo akaamua kushiriki mashindano ya kumtafuta mtangazaji wa kipindi cha Planet Bongo cha EATV mwaka 2008 na kuingia katika fainali, yeye na wengine 6.  Japo hakuwa mtangazaji wa kipindi hicho, alipata nafasi ya kuwa mfanyakazi wa TV hiyo katika shughuri za  IT zinazowezesha habari.

Ndipo akajikita moja kwa moja kwenye shughuri za habari na kuwa  mmoja wa waanzilishi wa kipindi cha SKONGA kilichoanzishwa mwaka 2009. Anatangaza katika vipindi viwili ambavyo ni SKONGA  na  5 SELECT,  vipindi ambavyo vinahusu wanafunzi wa shule za sekondari kuonyesha ujuzi na vipaji vyao. Pia anaandika habari  zinazohusu elimu kwenye gazeti tanzu au maarufu kama 'Blog'  yake ya allanluckyblog.blogspot.com.



Friday, October 4, 2013

SIKU YA WANYAMA DUNIANI- MBWA KUFANYA GWARIDE LEO


Siku ya wanyama duniani inasherehekewa kila mwaka Oktoba 4, ilianzia maeneo ya  Florence nchini Italy mwaka 1931 kwenye mikutano ya wanaikolojia. Katika siku hiyo, mifumo mbalimbali ya maisha ya wanyama husherehekewa kwa matukio yanayoandaliwa kwa namna  tofauti ikiwa pamoja na makongamano, matamasha,  harambee za kuchangia mifuko kwa ajiri ya kuandaa mazingira safi na makazi ya wanyama pamoja na kutembelea mbuga za wanyama.

Ni siku ambayo wanyama husaidiwa kufurahi, kupata matibabu na kuhamasisha kutatua matatizo yanayowakumba kama  kuteswa na binadamu, kugongwa na vyombo vya usafiri na kuuawa kwa makusudi. Pia wanaharaki wa haki za wanyama hutumia siku hiyo kama fursa ya kuelimisha watu juu ya haki hizo.

Kwa hapa nchini Tanzanaia siku hii inasherehekewa kwa shughuri kama hizo ambapo mbwa watafanya gwaride maeneo ya Kimele kata ya Mapinga maeneo ya Bagamoyo.

Katibu mtendaji wa chama cha kuzuia ukatiri kwa wanyama Tanzania TSPCA Bi. Johari Abdrahaman, ametoa wito kwa watanzania kuwapenda wanyama, kuwathamini na kujua haki zao za msingi.

Thursday, October 3, 2013

WAGUNDUZI WA INSTAGRAM WALIOMSHTUA MARK ZUCKBERG WA FACEBOOK

Kutoka kulia ni  Kelvin Systrom na Mike Krieger, waanzilishi wa Instagram

Instagram ni mtandao wa kijamii ambao umaarufu wake unazidi kuja juu kutokana na uwezo wake mzuri wa kuhifadhi na kusambaza picha ikiwa ni pamoja na sifa yake ya  pekee ya kubadilisha picha na kuziweka katika umbo la pande nne zinazolingana ‘Squre’, kupokea na kusambaza video kwa haraka sana.

Ulianzishwa na vijana wawili Kelvin Systrom na Mike Krieger wakiwa ndani ya jiji la San Francisco nchini  Marekani Oktoba 2010.

Mwanzilishi na CEO wa Facebook Inc, Mark Zuckerberg

Ikiwa na miaka miwili tu, April 2012, Instagram ilinunuliwa na kampuni ya Facebook Inc kwa dola za kimarekani billioni 1 ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wake 13, bei ambayo ni karibu mara tatu ya ile ambayo mtandao wa Yahoo ulitumia kununua mtandao wa picha wa Flickr mwaka 2005, ambao  ni miongoni mwa mitandao 50 maarufu duniani. Baada ya kuununua mtandao huo, CEO wa Facebook Mark Zuckerberg alisema atauacha mtandao huo ukue kivyake mbali na Facebook lakini chini ya kampuni ya Facebook Inc.


Instagram ambayo inatumiwa zaidi na watu maarufu “Celebrities” inakuwa kwa kasi sana ambapo April mwaka jana ilikuwa na watumiaji milioni 30 na mpaka sasa ina watumiaji zaidi ya milioni 100. Ni kutokana na mambo mengi yaliyofanyika kuuboresha mtandao huo hasa kwa mwaka huu 2013 ambapo kuanzia Juni 2013 imeanza kuruhusu watumiaji wake kuweka na kutuma video ya muda husiozidi sekunde 15 kitu ambacho pia kimezidi kuipa Facebook Inc thamani kubwa dhidi ya wapinzani wao wakubwa wa Twitter wanaotumia  ‘Twitter’s Vine video-sharing’.

Instagram imejishindia tuzo nyingi ikiwa ni pamoja na ile ya TechCrunch kama  mshindi wa pili wa ‘Application’ bora za simu Januari 2011, CEO wa Intagram Kelvin Systrom alitajwa nafasi ya 66 miongoni mwa watu 100 bora wabunifu katika biashara duniani Mei 2011 kupitia utafiti  uliofanywa na ‘Fast Company’. Pia mwaka huo huo Juni 2011 kampuni ijulikanayo kama INC ya Marekani iliwataja waanzilishi wa Instagram Kelvin Systrom na Mike Kriege miongoni mwa watu chini ya miaka 30 waliofanya mambo makubwa.

Tuzo zingine ilizojizolea Instagram ni ya mtandao bora ulioanzishwa ndani ya Marekani “Locally made” kutoka tuzo za ‘SF Week’ nchini humo mwaka 2011, Kampuni ya Apple Inc iliitangaza Instagram kama Application “App” bora ya simu ya mwaka 2011 na  waanzilishi wa Instagram  Kelvin na  Mike waliingia kwenye jarida la 7x7.


MASTAA WA NOLLYWOOD WALIVYOSHEREHEKEA SIKU YA UHURU NIGERIA OCTOBER 1


Alichokiandika muigizaji Genevieve Nnaji kwenye ukurasa wake wa Facebook
 
Miss Nigeria 2013 Ezinne Akudo Anyaoha akijiandaa kuwasaidia askari wa usalama barabarani kuongoza magari

Alichokiandika Rita Dominic kwenye Instagram
Miss Nigeria 2013 akisaidia  kuongoza magari kwenye makutano ya barabara ya Adeola Odegu na Ahmadu Bello jijini Lagos Jumanne Oct 1

Tuesday, October 1, 2013

WATANZANIA WANAOTAMBULIWA ZAIDI NA MTANDAO WA WIKIPEDIA



Mwl Julius K. Nyerere

Wikipedia ni mtandao unazungumzia historia za vitu na watu kutokana na taarifa mbali mbali ambazo ziko wazi juu vitu hivyo na watu hao. Utambuzi wa mtandao huu kwa vitu na watu hutokana zaidi na umaarufu wa vitu au watu husika.

Watanzania wanaotambuliwa zaidi na mtandao huo ni Mwl Julius Nyerere , Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete , Gertrude Mongella , William F. Shija, Freeman Mbowe,  Anna Abdallah , Anna Tibaijuka, Maida Abdallah, Salma Kikwete, Reginald Mengi, Laurean Rugambwa, Polycarp Pengo, Leonard Shayo.

Kwa upande wa wasanii na wanamitindo ni Dully Sykes , Bi Kidude, Cool James Joseph Haule (Professor Jay), Saida Karoli , Lady Jaydee , Joseph Mbilinyi (Mr. II), Rose Mhando ,Nakaaya Sumari , Flaviana Matata, Nancy Sumari  na Mustafa Hassanali.


Hasheem Thabeet akiwa mwanamichezo pekee kwenye orodha hiyo.
 
Saida Karoli
 Hasheem Thabeet

YALIYOTOKEA SEPTEMBA 2013 KATIKA UBUNIFU

Fuse ODG nchini Tanzania
Tamasha la kuhitimisha Kilimanjaro Music Awards jijjini Dar es salaam
Kagera waonja fursa
Mamia wajitokeza kwenye usaili wa Zanzibar Fashion week 2013
Miss Tanzania 2013 apatikana
 Tamasha la 32 la sanaa na burudani nchini Tanzania
........................................................................................................................................................................
Semadat inakutakia amani  na afya njema katika mwezi huu wa OCTOBER 2013