UA-45153891-1

Wednesday, November 20, 2013

HUYU NDIYE BABA WA MAPACHA WA P-SQUARE

Kutoka kulia ni Baba mzazi wa Peter na Paul, Mzee Okoye, katikati ni Bilionea maarufu wa nchini Nigeria anayeitwa Aliko Dangote ambaye alikuwepo kwenye harusi ya Peter, kushoto ni Peter ambaye ndiye aliweka picha hii kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii baada ya harusi yake.

KELLY ROWLAND AVALISHWA PETE YA UCHUMBA NA MENEJA WAKE TIM WITHERSPOON

Kelly Rowland

Staa aliyeupa shavu wimbo wa Dilema, Kelly Rowland amevishwa pete ya uchumba na meneja wake anayeitwa Tim Witherspoon siku chache zilizopita. Mwanadada huyo mwenye umri wa miaka 33 ambaye alikuwa miongoni mwa waliounda kundi lililotamba na wimbo wa Survivor siku za nyuma la Destiny’s child, alikuwa katika uhusiano wa zaidi ya miaka 4 na Tim japo haikujulikana kutokana na kutoweka wazi uhusiano huo tofauti na mastaa wengi nchini Marekani.
Picha kutoka video iliyoonekana Instagram

Kulikuwa na habari za chinichini lakini hata hiyo wafuatiliaji walianza uchunguzi wa jambo hilo baada ya Kelly kuonekana na pete ya uchumba kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram wakati alipoweka video akimtakia mtoto wa rafiki yake mmoja furaha na heri ya siku ya kuzaliwa. Katika video hiyo, alipomaliza kuongea alionyesha ile ishara ya busu kwa njia ya mkono na ndipo pete nzuri ya Almasi ilipoonekana kwenye kidole chake.

 Kelly Rowland na Tim Witherspoon

Tuesday, November 19, 2013

WANAOONGOZA KWA UTAJIRI NCHINI TANZANIA KWA SASA


Kwa mujibu wa jarida la Forbes, ni miongoni mwa matajiri 50 wakwanza barani Afrika

1. ROSTAM AZIZ- Nafasi ya 27 Afrika, Dola za kimarekani milioni 1000 ($1000M)
2. REGNARD MENGI- Nafasi ya 34 Afrika, Dola za kimarekani milioni 550 ($550M)
3.SAID SALIM BAKHRESA- Nafasi ya 38 Afrika, Dola za kimarekani milioni 500 ($500M)
4. MOHAMMED DEWJ- Pia nafasi ya 38 Afrika, Dola za kimarekani milioni 500 ($500M)

Sunday, November 17, 2013

PICHA ZA HARUSI YA PETER OKOYE WA P-SQUARE NA LOLA OMOTAYO, ILIYOFANYIKA LEO NOVEMBA 17, 2013


PETER WA P-SQUARE - BADO YUKO KAZINI INGAWA NI MASAA MACHACHE KABLA YA HARUSI YAKE

Msanii wa P-Square Peter Okoye amekwenda nchini Ghana kutoa burudani kwenye tamasha la “Glo Slide & Bounce” ambalo linafanyika usiku wa kuamkia siku ya harusi yake ambayo ni Jumapili, Novemba 17, 2013. Aliandika kwenye akaunti yake ya twitter kwamba “No bachelor eve for me” akimaanisha kwamba, kwake siku moja kabla ya siku ya harusi siyo ‘issue’ kwa hiyo ratiba zingine zinaendelea kama kawaida.


Peter Okoye akiwa kwenye ndege binafsi ya P-Square

Alisisitiza kwamba atarudi nyumbani pasipo kuchelewa maana kwa kutumia ‘Private Jet (PJ)’ kwa maana ya ndege binafsi, inawezekana bila tatizo. P-Square wanamiliki ndege yao binafsi ambayo hivi punde watatua nayo hapa nchini Tanzania.


Aliyoandika kwenye akaunti yake ya Twitter

 Ndege ya P-Square

Thursday, November 14, 2013

HARUSI YA 'PETER WA P-SQUARE' NA 'LOLA OMOTAYO' YANUKIA


 Peter na Lola

Siku ya jumapili Novemba 17, 2013 ikiwa ni siku tano tu kabla ya mapacha wa kundi la P-Square kufanya onyesho jijini Dar es salaam, familia ya Bwana Okoye ambaye ni baba wa vijana hao itakuwa na tukio la kihistoria la harusi ya kiutamaduni kati ya mmoja wa mapacha hao anayeitwa Peter Okoye na mpenzi wake wa muda mrefu Lola Omutayo ambaye alivishwa pete ya uchumba siku kadhaa zilizopita.

Kamati ya maandalizi ya harusi hiyo imesema kadi ya mialiko ambazo zimetengenezwa kwa ‘chip’ ya ki-electroniki zimeshatumwa karibu kwa wageni wote wanaotarajiwa kushuhudia tukio hilo, na bado zingine zinawasubiri watu wengi maarufu watakaotoka nje ya nchi ambao hawakutajwa.
 Kadi ya Harusi ya Peter na Lola itakayofanyika Jumapili Novemba 17, 2013

Lola Omutayo ambaye  alikuwa na ndoto za kuwa msanii wa Nollywood, siku za nyuma alienda nchini Marekani  kusoma ambapo alipata shahada ya  “Theatre Arts”  kutoka chuo kikuu cha Francisco. Aliporudi nchini Nigeria aliajiriwa na kampuni ya ECONET  ambayo kwa sasa ni  Airtel kama Meneja matukio na baadae kuhamia kampuni ya matangazo ya Daily Times na kisha kwenye kampuni ya mafuta na gesi inayomilikiwa na baba yake.

 Anasema alikutana na Peter kikazi wakati kampuni ya British American Tobacco (BAT) ambayo ni moja ya wateja wa kampuni ya baba yake ilipokuwa ikifanya shughuri za kimatangazo na P-Square, ndivyo alivyokutana  na Peter. Lola na Peter  wana mtoto mmoja wa kiume anayeitwa Cameron.

Peter na Lola kwenye 'Birthday' ya mtoto wao

Ingawa mama mzazi wa Peter alishatangulia mbele ya haki, mwaka mmoja uliopita, baba yake atawaongoza wanae na ndugu wa karibu wa familia kutoka kijiji cha Akwa jimboni Anambra kwenda Lagos kushuhudia harusi hiyo. Peter mwenye umri wa miaka 33 anakuwa mtoto wa kwanza wa Mzee Okoye kuoa. Pacha wake Paul bado hajaoa lakini tayari ametangaza ndoa kwa mpenzi wake anayeitwa Anita Itokwu-Isama. Kaka yao Jude mwenye miaka 38 bado hajamtambulisha yeyote katika familia kama mtarajiwa wake.

JUHUDI NA KUJITUMA NDIYO SIRI YA MAFANIKIO YA JACKLINE WOLPER

Jackline Wolper

Taarifa kutoka vyombo mbalimbali vya habari ikiwa pamoja na Redio  na  TV kupitia vipindi vya Bongo Movie, zinamzungumzia Jackline Wolper kama  msanii bize kuliko wasanii wote wa kike kwenye tasnia hiyo hapa nchini Tanzania ambaye amefanya na bado ana kazi nyingi zaidi  mwaka huu.

Msanii huyo ambaye anajituma sana na ana historia ya upambanaji mpaka kufikia kufahamika na kukubalika, anaandikwa kwenye magazeti mbalimbali hapa nchini pamoja na mitandao ya kijamii ambayo inazungumzia zaidi kipato chake kupitia Bongo Movies. Taarifa kutoka mtandao wa Vibe zinasema ndiye msanii anayelipwa pesa nyingi kucheza Filamu ambapo kiasi anachopewa kwa kila ‘Movie’ ni zaidi ya shilingi za kitanzania milioni tano.

Jackline Wolper ambaye anajiita Wolpergambe, pia ndiye aliyeshiriki kwenye Filamu nyingi zaidi mwaka huu ambapo kwa mwaka huu pekee, mpaka kufikia Oktoba 20, 2013 alikuwa tayari ameshiriki kucheza Filamu 22.

 Picha za gari la Jackline Wolper aina ya Land Cruiser Prado

Wednesday, November 13, 2013

GUMZO LA REMIX YA DIAMOND NA DAVIDO MITANDAONI

Mitandao mbali mbali zikiwemo Tovuti na Blogs za Afrika Mashariki, zinazungumzia balaa la Remix ya wimbo wa "Number One" inayofanywa na Diamond wa nchini Tanzania na Davido wa nchini Nigeria ambayo video yake inapikwa nchini Nigeria.
"Let me just say that you couldn't think of more ways that these two artists are alike. For starters, they both have radio hits, they both shoot expensive videos and both have a knack of blowing money (which they both have in plenty) for fun........................."
Hii ni kutoka www.homeboyzradio.co.ke ya nchini Kenya


"Diamond Platinumz tayari ameshafika nchini Nigeria kwa ajili ya kazi ya kimuziki pamoja na wasanii nchini humo ambapo baada ya kufanya remix ya My Number One na Davido, kazi inaendelea na sasa amewafata hukohuko kwao Nigeria".
Hii ni kutoka millardayo.com ya nchini Tanzania


"....While Diamond is arguably the highest riding artiste in East Africa, Davido is believed to be the fastest rising singer in Nigeria and the new union could just create a fresh showbiz force".
Hii ni www.standardmedia.co.ke ya nchini Kenya.

 

 East African superstar singer from Tanzania Diamond Platinumz is in Nigeria to work with Davido and Iyanya who were in Tanzania recently for Fiesta. After a collabo  with the two Nigerians Diamond will make two videos with Davido and Iyanya and his tour also aims at making music network with Nigerian artists.
Hii ni kutoka swahiliworldplanet.blogspot.com ya nchini Tanzania

Thursday, November 7, 2013

BI. ASHA BILAL KUWAONGOZA MASHABIKI WA KANGA ZA KALE HOTELI YA SERENA

Mke wa Makamu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi Asha Bilal  

Mke wa Makamu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi Asha Bilal,  anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maonyesho ya mitindo ya kimataifa ya mavazi ya kanga, yanayojulikana kama ‘Kanga za Kale.

Maonyesho hayo yatafanyika katika Hoteli ya Serena ijumaa wiki hii, yatakusanya watu wengi maarufu ambapo mke huyo wa makamu wa Rais atawaongoza mashabiki wa fani ya mitindo ya mavazi  akiwa katika vazi la Kanga.

Mkurugenzi wa Fabak Fashion, Asia Idarous, ambao ndio waandaji wa maonyesho hayo, amesema tofauti na maonyesho mengine yaliyotangulia, Kanga ya Kale ya mwaka huu ina ladha tofauti kidogo.

“Licha ya kuonyesha matoleo mapya na mitindo ya kanga pia kuonyesha yale ya zamani ili kuleta vionjo zaidi kwa wavaaji wa sasa, tunakusudia kutoa darasa kuhusiana na thamani ya kanga japo kwa muda mfupi tu”, anasema.

Watakaofika kwenye maonyesho pia watapata burudani kutoka katika Kundi la Mashauzi Classic, huku wakishuhudia mitindo kadha wa kadha ya kanga kutoka kwa wabunifu mbalimbali nchini.

Maonyesho ya Kanga za kale nchini yanafanyika kwa mara ya tano tangu pale yalipoanzishwa rasmi mwake  mwaka 2008.
 

Friday, November 1, 2013

HARUSI YA DENIS MWANGUO NA KOKUSHUBILA KAIJANANTE NI MOJA YA MATUKIO YALIYOFANA SANA OKTOBA 2013

 Denis na Kokushubila wakifunga ndoa kanisani Oktoba 12, 2013 katika kanisa la KKKT Tabata, ambayo ilifuatiwa na sherehe ya Harusi katika ukumbi wa Best Choice Tabata Aroma jijini Dar es Salaam.
 
 Wakisikiliza neno
 Wageni wakiingia ukumbini
 Bwana na Bibi Harusi ukumbini
 
 Mama na baba wa Bw. Harusi Mr& Mrs Mwanguo

Baba na mama wa Bi. Harusi Mr & Mrs Kaijanante
 Babu upande wa familia ya Denis akifurahia kupata mjukuu mwingine
 Kushoto ni mama wa Bibi Harusi na kulia ni mama wa Bw.Harusi wakiwa na watoto wao wapendwa
Kaka yake Bibi Harusi, Shumbusho Kaijanante akiwa na Bestman pamoja na dada zake, nyuma ni Redemptah, aliyekuwa Matron, ambaye pia ni dada yake Kokushubila.
 Meza kuu ya wazazi upande wa Bibi Harusi
 Dada zake Bibi  Harusi, Bi.Abela na Bi.Stephy Koku Semugabo
Furaha na shangwe kwa wageni waalikwa ndugu na jamaa
 
 Ndugu na marafiki wa karibu waliosoma na Bibi Harusi (Mates) pamoja na watoto maarufu kama malaika wa shughuri
 'Ladies Mates' wa Kokushubila
 Wapambe wa ukweli, ndugu na marafiki, wakiingia ukumbini, wao walitumia jina la jumla kama "Mates"
 Hapana chezeya wewe!
 Wawili zamu kwa zamu

 Twende kazi...!

 Haya sasa...!
 Shangwe shangweni, zawadi zawadini......!

 Ndivyo Kamera ya Sony Cyber-Shot DSC-H9 ilivyomnasa huyu mdau Clarence...akiyarudi na binamu yake Stephy Koku, kushoto kwake ni mama yake mzazi na kulia kwake ni mama yake mdogo, ambao wote ni shangazi zake Bibi Harusi. Kokushubila anashuhudia tukio hilo.

KAMATI:  Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa


Semadat inakutakia Novemba njema.