Ni ndani ya kipindi cha Mboni Show kilichoruka Alhamisi ya tarehe 23 January 2014 kuanzia saa tatu usiku chini ya mwanadada Mboni Masimba. Hii ni picha ya pamoja.
.
Friday, January 24, 2014
Thursday, January 23, 2014
D'BANJ ATAMBULIWA RASMI NA MTANDAO WA FACEBOOK (VERIFIED)
Ukurasa wa Facebook wa mwanamuziki maarufu wa Nigeria D'Banj 'Kokomaster', staa wa Oliver twist, imehakikiwa na kuthibitishwa na mtandao huo kwa kuwekewa alama ya 'tick' ya rangi ya Bluu, hivyo kuitofautisha na zile zilizofunguluwa kienyeji na watu wangine kwa kutumia jina lake.
D'Banj anakuwa mtu wa pili nchini humo ambapo kabla ya hapo aliyekuwa na ukurasa wa Facebook katika hali hiyo ya kutambuliwa ni Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan peke yake.
Tofauti na kwenye mtandao wa Twitter ambao watu wengi maarufu nchini humo wana alama hiyo, kwa upande wa Facebook si kitu rahisi na kwa hapa nchini Tanzania hakuna aliyewekewa alama hiyo kwenye Facebook japo upande wa Twitter wapo kama Rais Kikwete, AY, January Makamba, Flaviana Matata na Hasheem Thabeet.
DIAMOND KUDONDOKA JIJINI NAIROBI KWA AJILI YA PARTY
"After shutting down Nairobi in August last year, Bongo’s prince Diamond Platnumz is coming back to the country!". Mdivyo ulivyoandika mtandao unaoitwa 'Ghafra' wa nchini Kenya. Diamond yuko nchini humo siyo kwa sababu za kibiashara bali kwa ajili ya 'Party' ambayo haikujulikana inahusu nini. Pia mtandao huo umempa shavu kubwa Diamond kwamba ni msanii mkubwa na msanii pekee kutoka Afrika Mashariki ambaye alialikwa kwenye harusi ya Peter wa P-Square nchini Nigeria.
Pia Diamond mwenyewe alizungumzia safari hiyo kwenye mitandao ya kijamii na kuweka picha inayomuonesha akiwa maeneo ya uwanja wa ndege kama inavyoonekana hapo juu.
BIRTHDAY YA KWANZA YA MTOTO WA PETER WA P-SQUARE 'ALIONA OKOYE'
Aliona ametimiza mwaka mmoja. Wazazi wake Peter na Lola pamoja na 'uncle' wake Paul, wameshiriki kumpongeza wakiwa katika makazi yao mapya Atlanta Marekani. Mtoto huyo ni 'photocopy' ya Peter na rangi ya mama yake.
'MAMA LULU' NA 'MAMA KANUMBA' KUTUA BUKOBA
Mastaa wanawake ambao umaarufu wao na urafiki wao ulitokana na
matatizo, wanaendelea kuuonesha umma kwamba yaliyotokea tayari yametokea
na hakuna aliyependa yatokee, kikubwa ni kumshukuru Mungu kwa kila jambo na kuhimarisha upendo. Ni baada ya kulipotiwa hivi punde na
mtandao maarufu wa Global Publishers kwamba wanaandaa safari ya kwenda
Bukoba mkoani Kagera wanakotokea, ili kula kiapo cha kuimarisha undugu.
Safari ya Lucresia Karugila ‘Mama Lulu’ na Flora Mtegoa ‘Mama Kanumba’ inalenga pia kumuhudumia mama mzazi wa Flora Mtegoa yaani bibi yake marehemu Steven Kanumba, ambaye ni mgonjwa kwa sasa.
GENEVIEVE NNAJI AWA BALOZI WA KAMPUNI YA ETISALAT
Genevieve Nnaji
Muigizaji mashuhuri wa kike nchini Nigeria na Afrika kwa ujumla Genevieve Nnaji amechaguliwa kuwa Balozi wa Kampuni ya Simu ya Etisalat kupitia huduma ya Easy Flex. Shughuri fupi ya kumkaribisha kufanya kazi hiyo imefanyika leo katika hoteli ya Wheat baker nchini humo. Anaungana na staa mwingine Hakeem Kae-Kazim ambaye pia ni Balozi wa Kampuni hiyo. Kampuni hiyo iko kwenye kampeini kabambe ya huduma hiyo.
Wednesday, January 22, 2014
NANCY SUMARI NA "NYOTA YAKO", FARAJA NYALANDU NA "UNAWEZA" NI MFANO WA KUIGWA
Warembo hawa wameshatoa vitabu na wanaendelea kuandika vingine. Nancy Sumari ambaye alikuwa Miss Tanzania 2005 alizindua kitabu cha watoto kinachoitwa 'NYOTA YAKO' mwaka 2013.
Leo tarehe 22 Januari 2014, Faraja Nyalandu nae amezindua kitabu chake kwa ajili ya wanafunzi
kinachoitwa 'UNAWEZA' ambacho kinatoa mbinu kumi za mwanafunzi kumudu
masomo.
Faraja Kotta Nyalandu akizindua kitabu chake kinachoitwa 'Unaweza' Januari 22, 2014
Faraja akiwa na Nancy wakati wa uzinduzi wa kitabu chake
Nancy Sumari alipokuwa akizindua kitabu chake kinachoitwa 'Nyota yako' Machi 2013
MWAFRIKA MWEUSI WA KWANZA KUTEMBEA NJE YA SAYARI YA DUNIA
Mandla Maseko
Anaitwa Mandla Maseko.Ni Dj wa mtaani,nchini Afrika Kusini, mwenye umri wa miaka 25, akitokea wilaya ya Mabopane jirani na jiji la Pretorea.Ni baada ya kushinda mashindano yaliyoandaliwa na wanataaluma wa anga wa nchini Marekani.Amewashinda washiriki zaidi ya milioni moja kutoka nchi 75 na kuwa mmoja wa watu 23 watakaotembelea mwezini.
Alikuwa mwanafunzi wa Uandisi wa Ujenzi (Civil Engineering) ambaye alisitisha masomo baada ya kushindwa kulipa ada.Bado anaishi na wazazi wake na ndugu zake wanne ambapo katika familia yake hakuna hata mmoja ambaye alishatoka nje ya Afrika Kusini. Katika hali ya kawaida inasemekana kutembelea huko ni gharama zisizopungua dola za kimarekani 100,000.
Tuesday, January 21, 2014
RAIS OBAMA ALIPOSEMA BANGI HAINA MADHARA MAKUBWA ZAIDI YA POMBE
Akinukuliwa na gazeti la New Yorker linalotoka Jumapili,alipofanyiwa usaili kuhusiana na mjadala wa uhalalishaji wa Bangi katika maeneo ya Washington na Colorado, Rais Obama alisema "Nilishavuta nikiwa mdogo na ipo kwenye historia. Hii ni tabia mbaya kama ambavyo pia nilivuta sigara. "Ila sizani kama ni hatari kuliko pombe".
"Si hatari zaidi ya pombe?", aliulizwa Rais Obama. Hata hivyo alielezea anachokimaanisha kuwa si kwamba anaunga mkono matumizi yake bali hafurahishwi na masuala ya sheria inayowatolea macho na kuwafunga kwa muda mrefu watoto wa masikini kutokana na mazingira ambayo yanawafanya waonekane, wakati watoto wa familia za maisha ya kati na wa matajiri wakitumia na kuendelea kupeta.
Subscribe to:
Posts (Atom)














