Masoud Kipanya
Msanii Ali Masoud maarufu kama ‘Masoud Kipanya’ ambaye kwenye ukurasa wake wa facebook anajitambulisha ‘Political Cartoonist’ kama kazi yake ya kwanza, anajulikana kama mchora katuni maarufu nchini na mtangazaji wa redio na TV ambaye aliwai kufanya kazi kwenye kituo cha redio cha Clouds FM. Jina lake lilitokana na muonekano wa katuni anayotumia, wenye sura ya panya. Mbali na shughuri hizo pia ni mbunifu katika fani ya mitindo na mtayarishaji wa vipindi.
Alizaliwa tareha 23 Juni 1972 jijini Dar es salaam na kuanza kazi hiyo ya sanaa akiwa shule ya msingi. Kazi yake ya kwanza ilichapishwa kwenye jarida la Heko mwaka 1989, baada ya hapo alifanya kazi kama mhariri wa katuni kwenye gazeti la Sanifu na mhariri mtendaji wa katuni gazeti la majira, pia katuni zake hutokea gazeti la Mwananchi.
Ameshiriki maonyesho mbalimbali Tanzania na Afrika Kusini kama mtaalam wa matumizi ya rangi ‘Painter’ na amejishindia tuzo nyingi ikiwa pamoja na tuzo ya kwanza ya katuni Afrika Mashariki. Pia alishiriki mashindano ya sanaa ya uchoraji yaliyoandaliwa na Friedrich Ebert Stiftung na kupata nafasi ya kutembelea nchini Japan kwenye program ya wiki mbili ya maonyesho ya kimataifa ya utamaduni yaliyoandaliwa na ‘Japan Foundation’.
Ndiye mbunifu wa vipindi vya Televisheni vya ‘Maisha Plus’ na ‘Inawezekana’ pamoja na taasisi binafsi ya ‘Inawezeka Foundation’. Pia ni CEO wa kampuni ya KP Media.
Kufahamu wachoraji wengine wa katuni, tembelea: bongotoons
Masoud Kipanya Cartoon @facebook.com





















