UA-45153891-1

Tuesday, January 21, 2014

2 FACE IDIBIA NA ANNIE WAMPA MTOTO WAO JINA "OLIVIA"


Mwanamuziki wa Nigeria na staa wa wimbo wa African Queen ambaye pia yuko miongoni wa wanamuziki 10 matajiri barani Afrika, ametupia au kwa neno lingine katupiamo picha yake akiwa pamoja na mtoto wake na kuandika "Say hi 2 Olivia Idibia". Bila shaka Olivia Idibia ndilo jina la mtoto huyo ambaye amempata akiwa na mke wake Annie ambaye ni staa wa Nollywood.

"SHKAMOO JIDE" NDIVYO INAVYOSIKIKA MITAANI NA KUSOMEKA MITANDAONI

Siku hizi kauli hii, haitumiki tu kama ilivyozoeleka, bali pia hutumiwa na vijana wa sasa kama 'salute' kwa mtu anapokuwa amefanya jambo  zuri au lenye ishara ya mafanikio au hatua flani mbele. Mwanadada Judith Wambula Lady Jaydee ameonakana kwenye picha na gari aina ya Range Rover Vogue na akiwa ameandika "My new ride"
Jaydee akiwa na gari lake

JACQUELINE PATRICK, AGNES GERALD ‘MASOGANGE’ MELISA EDWARD NA WENGINE BADO NI ROLE MODELS WA MABINTI WENGI WA SASA

Jacqueline Patrick

"Tukianzia urembo tu they got a gwan,  vipaji vyao navyo tu they got a gwan, mbali na mabaya wayafanyayo, nabaki kusema tu they got a gwan". Pengine mistari hii ingeweza kupendekezwa iwe 'remix' ya wimbo wa'She got a gwan' kama msanii wa wimbo huu angekuwa bado yuko hai au pia mwingine yeyote anaweza kushuka nayo. Lakini lengo hasa ni kusema hivi:

Mastaa wa kike ambao mpaka sasa wamehusishwa na tuhuma za usafirishaji wa madawa ya kulevya  ni Jacqueline Patrick (alikamatwa Macau-China), Saada Kilongo (JNIA-Dar), Agnes Gerald  ‘Masogange (Afrika Kusini) na Melisa Edward (Afrika Kusini). Pia yumo Mbongo aliyenaswa Misri aliyetajwa kwa jina moja la Fatuma huku Sandra Khan ‘Binti Kiziwi’ akitumikia kifungo cha miaka mitano China kwa mujibu wa mtandao wa habari wa Global Publishers.

Hata hivyo,kwa wale dada zetu wanaowatazama hao kama role models wanaombwa wachukue yale mazuri hasa juu ya kazi zao za sanaa na kuyaacha mabaya na ambayo ni kinyume na sheria. For the love of entertainment industry.

Monday, January 20, 2014

"SINGIDA INAPAA" ASEMA MOHAMMED DEWJI


Mbunge wa Singida ambayo pia inajulikana kama 'Singapo' ambaye pia ni mjasiliamali Bilionea Mhe. Mohammed Dewji 'MO'.Amesema singida inapaa baada ya Mhe. Lazaro Nyalandu kuteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na utalii. Amesema hivyo huku akimpongeza Waziri huyo mpya kupitia mtandao wa Twitter. Hapo hapo amempongeza Shemeji yake Faraja Nyalandu ambaye ni mke wa Mheshimiwa huyo aliyekuwa Naibu waziri kabla ya uteuzi huo mpya.

KUTEULIWA KWA MHE. LAZARO,HAPA KUNA MCHANGO WAKO FARAJA NYALANDU


Walio wengi wanafahamu kwamba aliyekuwa Miss Tanzania mwaka 2004,enzi hizo akijulikana kama Faraja Kotta, ni mke wa aliyeteuliwa kuwa waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu ambaye alikuwa Naibu Waziri katika Wizara hiyohiyo. Kwa kuwa 'semadat' si mwandishi wa habari za siasa bali tu zile zingine za kuleta hamasa ya ubunifu kupitia vitu, watu na maisha ya watu wanaosababisha hivyo vitu, basi nizungumzie upande huu wa shilingi.

Mwaka mmoja uliopita, Faraja alipongezwa sana na vyombo vya habari, hasa mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwa ni pamoja na magazeti tanzu yaani Blogs kwa kutimiza miaka mitano ya ndoa. "Thanking God for 5 years of beatiful marriage, I am still in love, I am still happy. I am extremely grateful". Aliandika Faraja Nyalandu kwenye mtandao wake wa twitter au kwa swaga zaidi tunasema ali-tweet.

Mtafuta dondoo wa 'semadat' alitembelea akaunti za twitter za wawili hao na kukuta majibizano ya pongezi ya hapa na pale kwenye akaunti ya Mheshimiwa Nyalandu ambaye ni mtumiaji mzuri sana wa akaunti hiyo. Pongezi moja ikiwa ni kutoka kwa aliyekuwa miss Tanzania mwaka 2000 Jackline Ntuyabaliwa 'K-lynn'. "Congratulations Mh Nyalandu for the new post", alitoa pongezi K-Lynn. "Asante shem", alijibu Mheshimiwa.



 Hata hivyo, mpaka siku  ambayo utangazaji wa uteuzi huo ulifanyika inaisha, Faraja Nyalandu hakuwa ameongea chochote kupitia akaunti yake ya Twitter. Alitafutwa Facebook na Instagram bila mafanikio. Hata hivyo siyo kesi, tunatoa pongezi  kwake tukizingatia nukuu isemayo...
"Behind Every Successful Man There Is A Woman".

ALICHOSEMA SHYROSE BHANJI KUFUATIA UTEUZI WA MAWAZIRI NA MANAIBU WAPYA KWENYE BAADHI YA WIZARA



Sunday, January 19, 2014

MSANII ALIYECHORA PICHA HII ALILENGA KUMCHORA MHESHIMIWA DR. ASHA ROSE MIGIRO?!!!


Katika bofyabofya za hapa na pale kwenye mitandao ya kijamii, muda mfupi baada ya mawaziri na manaibu mawaziri wapya walioteuliwa kutangazwa semadat ikakutana na "tweet" yenye picha, inayosema "Waziri mpya wa Katiba na Sheria ni Dr. Asha Rose Migiro".Baadhi ya watu waliizungumzia picha hiyo ikiwa ni pamoja na Mbunge wa jimbo la Kawe Mhe. Halima Mdee.  Inasemekana picha hiyo iko pande za Rock City yaani jijini Mwanza.

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dr Asha Rose Migiro

MHE. LAZARO NYALANDU (MB) ATANGAZWA KUWA WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amewahamisha na kuwateua baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri ambapo aliyekuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Samuel Nyalandu ameteuliwa kuwa Waziri wa Wizara hiyo. Pia Rais Kikwete amemteua Mhe. Mahmoud Hassan Mgimwa  kuwa Naibu Waziri wa Wizara hiyo ya Maliasili na Utalii. Taarifa kamili ya Uteuzi huo imetolewa kama ifuatavyo....

Saturday, January 18, 2014

SIKU YA KUZALIWA SAMANTHA MUMBA

Mwanamuziki aliyetamba na wimbo wa 'I'm right here'  mwaka 2002 Samantha Mumba, anasherehekea siku yake ya kuzaliwa leo Januari 18 ambapo anatimiza miaka 31.
Samantha Mumba

Thursday, January 16, 2014

KUNA NINI KATI YA 'J'ODIE WA KUCH KUCH(OH BABY)' NA WAHU WA 'SWEET LOVE'?


J'odie 

1.Wote ni  wanadada ambao sio tu ni waafrika lakini pia wanaoupenda uafrika, mmoja akiwa mnigeria na mwingine mkenya.

2. Wote wameimba nyimbo kwa kuwaimbia watoto, ukisikiliza nyimbo hizo kwa mara ya kwanza kama hujayanyaka mashairi vizuri utazani ni za mapenzi kumbe ni vionjo tu na ubunifu wa kuteka hisia za watu.

3.Wote wamepiga kitabu ambapo huyu J'odie wa 'kuch kuch' ana digrii ya Mawasiliano ya umma(Mass Communication) kutoka chuo kikuu cha Lagos na vyeti kadhaa ikiwa pamoja na cheti cha  utawala wa ujasiliamali na cheti cha uongozi, wakati Wahu wa 'sweet love' ana digrii ya Hisabati (Mathematics) kutoka chuo kikuu cha Nairobi na masters katika masuala ya kijamii.

Wahu