UA-45153891-1

Monday, March 3, 2014

LUPITA NYONG’O ASHINDA TUZO YA OSCAR KUPITIA FILAMU YA “12 YEARS SLAVE”



Muigizaji maarufu wa kike wa nchini Kenya ambaye anafanyia shughuri zake za filamu Hollywood nchini Marekani, ameshinda tuzo ya Oscar kwenye tuzo hizo za 86 za Academy kwa uhusika wake katika filamu ya 12 Years a Slave ambayo ilitengenezwa mwaka 2013 chini muongozaji Steve McQueen.

Ameshinda tuzo hiyo kipengele cha ‘Best supporting actress’ ambapo alikuwa anachuana na mastaa wengine wakubwa akiwemo Sally Hawkins wa filamu ya Blue Jasmine na muigizaji maarufu wa nchini Marekani Jennifer Lawrence.


Wednesday, February 26, 2014

KITABU ANACHOSOMA LOVENESS LOVE 'DIVA' KWA SASA


Kuwa mtangazaji, mwandishi  au mwanahabari kwa namna yoyote inakupasa pia kuwa msomaji wa maandiko na vitabu mbalimbali hasa vinavyohusu kipengele husika cha habari  zako. Inaelekea mwanadada huyu alishasoma vitabu vingi na bado anaendelea kusoma.  Kwa sasa anasoma kitabu hiki.

UNGEKUWA 2FACE IDIBIA UNGEJISIKIAJE KWA HILI?


Kweli unapokuwa mtu maarufu jiandae kwa lolote litakalokutokea kuanzia kwenye jamii mpaka vyombo vya habari, hasa mitandao ya kijamii. Jibu la swali hili linaweza kuwa "Vibaya!!!", ingawa naamini kwa  Staa yeyote, jibu linatakiwa kuwa  "Kawaida!!!". Na inabidi litolewe kwa kumaanisha, sio tu kwa sababu linatakiwa kuwa hivyo.

ELIZABETH MICHAEL 'LULU' ANAVYOTUMIA MITANDAO YA KIJAMII


Kama ilivyowai kuandika mwandishi mmoja wa mtandao unaoitwa 'Social Media today' kwamba tunakoelekea mitandao ya kijamii itakuwa kwa ajili ya kuonyesha badala ya kuandika hivyo kila mtumiaji atakuwa na Kamera ya picha za Still na ya Video, ndivyo anavyoonyesha muigizaji Elizabeth Michael 'Lulu'. Star huyo wa Bongo Movie ambaye hapitishi siku zaidi ya moja kabla hajasalimia na kuzungumza kwa picha na maneno mawili mpaka matatu tu kila siku kwenye ukurasa wake wa Facebook, Jana Jumanne Februari 25, 2014 alikuja kwa mtindo huo. Tazama zingine mbili za  Jumapili na Jumatatu iliyopita na alivyoandika.

PICHA ZA VIDEO YA DIAMOND NA D'BANJ KAMA VIRUSI


Ikiwa ni masaa machache tangu mwanamuziki staa wa wimbo wa 'Number One' Diamond Platnumz alipoweka picha za Video ya Project ya 'Do agric' anayofanya na mwanamuziki wa nchini Nigeria D'Banj,zimesambaa kwenye  mitandao mbalimbali ya Afrika mashariki kama virusi au kwa lugha nyingine wanasema zimekuwa 'Viral' ambapo mitandao imezichukua na kuzizungumzia  ikiwa pamoja na mtandao wa 'vibeweekly.com' ulioandika kichwa cha habari "Diamond Releases Behind The Scenes Photos Of His Video With Dbanj" na kuandika haya  juu ya msanii huyo.

'LIPSTICK' NA 'LIPGLOSS' ALIZOZINDUA MSHINDI WA BIG BROTHER 2013 DILLISH MATHEWS


Mshindi wa Big Brother 2013 Dillish Mathews, anaendelea kutumia jina lake kubuni bidhaa mbalimbali ambapo siku chache zilizopita ndani ya mwezi huu wa Februari 20, 2014, alizindua bidhaa za urembo ikiwa pamoja na 'Lipstick' na 'Lipgloss' .Wengi wamekuwa wakisuburi ni jambo gani litafuata kuhusu Dillish ikiwa ni muda mfupi sasa tangu aachane na mpenzi wake Stephen kwa sababu anategemea kupata mtoto kutoka kwa mwanamke mwingine.  

Mwanadada huyo ambaye pia siku chache zilizopita alikuwa nchini Nigeria kwenye maandalizi ya filamu, alizindua vipodozi hivyo ndani ya jiji la Windhoek nchini Namibia. Hizi ni baadhi ya aina za bidhaa zake alizozindua kama zinavyoonekana.

Tuesday, February 25, 2014

OMOTOLA APEWA SOMO NA WANAHABARI NCHINI NIGERIA

Omotola Jalade

Siku chache zilizopita, mtoto wa muigizaji wa kike maarufu nchini Nigeria Omotola Jalade-Ekeinde alisherehekea siku ya kuzaliwa  na kuweka baadhi ya picha zake kwenye mtandao wa Instagram.  Blogger s wa nchini humo walizichukua picha hizo za mtoto wa miaka 14 anayeitwa Meraiah Ekeinde na kuziweka kwenye Blog zao ikiwa pamoja na kuzizungumzia. Kupitia mtandao wa Facebook, Omotola aliwashukuru  waandishi hao kwa kumtakia mwanae furaha ya siku ya kuzaliwa ingawa pia aliwaonya na kukemea kitendo cha  kutumia picha za mtoto mdogo hasa wale ambao  walioandika maneno “hot and sexy”. Hivi ndivyo alivyoandika kwenye ukurasa wake wa Facebook, pia sehemu ya barua ya wazi aliopewa na mmoja wa waandishi wa habari za burudani mitandaoni nchini Nigeria, anayeitwa . Osagie Alonge.

TUNDAMAN WA TIP TOP CONNECTION ANAPOSEMA “MKATABA WA KIROHO”


Wiki iliyopita kulikuwa na taarifa juu ya wanamuziki wa Bongo Flava waliojitoa Tiptop Connection kutaka kurejea tena ikiwa pamoja na MB Dogg, Spark na Keisha. Alipoulizwa msanii mwenzao Tundaman juu ya suala hilo alisema,

WALTER CHILAMBO AMALIZA MKATABA WAKE NA ZANTEL


Mshindi wa Bongo Star Search 2012 Walter Chilambo amemaliza mkataba wake na kampuni ya simu ya Zantel ambao ndiyo mdhamini wa shindano hilo linafanyika kila mwaka chini ya kampuni ya Benchmark Production.

SASA KUNA WAZEE WA NGWASUMA NA VIJANA NGWASUMA


Bila shaka wengi wanaifahamu bendi ambayo ni miongoni mwa zile  maarufu hapa nchini, inayoitwa FM Academia ‘Wazee wa ngwasuma’. Baada ya bendi hiyo kuwa na wanamuziki wengi mpaka kufikia kiasi kwamba wengine wanafanya vizuri nyuma ya vipaza sauti na vyombo  vingine vya muziki lakini hawajulikani  kwa muda mrefu japo kazi nzuri inaonekana, baadhi yao wamehamua kujitoa na kuanzisha bendi nyingine inayoitwa  ‘Vijana wa ngwasuma’.