UA-45153891-1

Saturday, October 19, 2013

UMESIKIA TANGAZO MOJA, SAUTI YA MTOTO AKISEMA "BABA TUCHEZE BAISHOO"? NI HUYU HAPA!



Ni mtoto wa Msanii wa Bongo Flava D-KNOB, anayeitwa Vivica. Aliyembeba ndiye baba yake ambaye alitamba na wimbo wa 'Bad Man' ambao alimshirikisha Carnibal wa nchini Kenya. Nyimbo zingine ambazo mistali ya D-Knob ilisikika ni pamoja na 'Niwe na wewe', 'Elimu mtaani.com' na 'Sauti ya gharama'.

Friday, October 18, 2013

MTOTO WA MIAKA 9 WA NCHINI NIGERIA ALAMBA SHAVU KWENYE KAMPUNI YA MICROSOFT

Jomiloju Tunde-Oladipo

NAMBA  ya wanigeria waliothibitishwa kwa vyeti maalum na kufanya kazi kwenye kampuni maarufu duniani ya Kompyuta ya Microsoft, inazidi kuongezeka lakini kilicholeta utofauti zaidi ni mtoto anayeitwa Jomiloju Tunde-Oladipo mwenye umri wa miaka 9 aliyenyakua cheti au ‘Gamba’ la  ‘Microsoft Certified Professional’ hivi punde.

Imetokea baada mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi kuwa wa kwanza kati ya mwanafunzi 21 wa shule za msingi waliofanya mtihani kwa ajiri hiyo jijini Lagos. Amechukuliwa na kampuni hiyo kama mtaalam wa program ya Microsoft Office ‘Microsoft Office Specialist’ (MOS) upande wa Word 2010 baada ya kupata alama 769 kati ya 1000, ambapo amezidisha  alama 69 kutoka alama 700 ambazo ndicho kilikuwa kiwango cha chini (Pass marks).

Amekwenda kuungana na Lavish Nashree wa miaka 8 kutoka nchini India, na wengine wawili Arfa na Thobani kutoka Pakistan.


“Haikuwa kazi raisi maana nilifanya mtihani mwaka jana sikufanikiwa, lakini niliendelea kusoma kwa bidii nikiwa nyumbani na shuleni pia. Niko kwenye Kompyuta siku zote baada ya muda wa masomo. Kama sifanyi chochote, basi nilienda kwa mwalimu wangu wa Teknolojia ya habari na mawasiliano kujifunza zaidi” Alisema Jomiloju.


Mwalimu wake wa darasa Bi. Elizabeth Ogunrinola pia alisema mtoto huyo ana kipaji cha pekee kwa kuwa si kwamba yuko vizuri kwenye somo la ICT (Tehama) tu, bali masomo yote. Anasoma kwa bidii na ana nidhamu ya hali ya juu.


Baba yake aliongeza kwa kusema “Si kwamba  ni malezi yetu tu yanayomfanya awe vile, lakini ni mtoto mwenye uwezo binafsi, maana ana vipaji vingi, anaweza kutumia vyombo vya muziki ikiwa pamoja na Saxophone na Kinanda (Keyboard).  Ni muigizaji mzuri na ana uwezo mkubwa wa kuogelea. Kila mwisho wa muhula hushiriki kwenye maigizo na mashindano ya quiz. Pia mwaka huu amepata zawadi za masomo mengi ikiwa pamoja na somo la ICT.


‘Microsoft Certified Professional’ ni vyeti ambavyo hutolewa na kampuni ya Microsoft kwa watu ambao wamethibitishwa na kampuni hiyo kuwa na ujuzi katika kutatua matatizo ya programu za Kompyuta, hasa zile zinazotumiwa na watumiaji wa kawaida au wa mwisho (End users) kupitia mifumo ya Windows XP, Vista, Windows7 na zingine kama hizo.

JARIDA JIPYA LA VIBE LATOA FULSA KWA WANAFUNZI WA VYUO


Ukurasa wa  juu (Front page) wa Jarida la Vibe

Jarida jipya la Vibe ambalo limeanza kutoka mwezi huu, yaani October 2013 limewaomba wanafunzi wa vyuo wajitokeze kuwa mabalozi wake "Ambassadors".

 Afisa Mtendaji Mkuu wa Vibe amesema Wanafunzi watakaopata nafasi hizo watanufaika kwa kupata uzoefu wa kazi hasa katika tasnia za Masoko na Habari na pia watapewa barua za utambuzi wa utendaji kazi. Pia amesema, watasaidiwa kupata kazi hasa katika makampuni ambayo Vibe inafanya nayo kazi za Masoko.

Kwa maelezo zaidi tembelea: vibe.co.tz. Pia unaweza kuwatumia email: info@vibe.co.tz.

Thursday, October 17, 2013

BABA YAKE KANUMBA AINGIA RASMI KWENYE FILAMU

Mzee Charles Kanumba

Baba mzazi wa aliyekuwa muigizaji maarufu wa filamu nchini Tanzania Steven Kanumba, Mzee Charles Kanumba ,ameingia kwenye fani ya uigizaji kikwelikweli na tayari yupo kwenye soko la Bongo Movie baada ya kuigiza kwenye filamu inayoitwa “Mwananjilinji” ambayo tayari imeuza kopi za kutosha kanda ya ziwa.

Amesema anafanya hivyo kwa ajiri ya kumuenzi mtoto wake ambaye vipaji vingi alivyokuwa navyo alivirithi kutoka kwake. Alipoulizwa ana vipaji gani, kupitia Amplifier ya Clouds FM, amesema yeye ni muimbaji wa kwaya  muda mrefu sana, mpiga gitaa, muigizaji na mchekeshaji ambaye amekuwa akiyafanya yote hayo kwenye shughuri za kanisa.

Amesisitiza kwamba wapenzi wa filamu wakae mkao wa kula na watarajie makubwa sana kutoka kwake.

REHANNA ANGEKUWA BONGO ANGEKWISHAIMBA BONGO FLAVA, TAARABU NA MCHILIKU


 Rehanna

Muimbaji wa Marekani Robyn Rihanna Fenty ‘Rihanna’ anasifika kwa ubunifu mkubwa na kutumia fulsa vizuri inapotokea. Anafanya muziki wa staili nyingi tofauti na kila anapogusa anatikisa ulimwengu wa muziki. Kumbuka nyimbo zake za RnB ukiwemo wa “Unfaithful”, za dancehall ukiwemo wa "Pon de Replay," na nyimbo zenye mchanganyiko wa RnB, Pop na Hip Hop kama "Umbrella” ambao mwanzoni ulikuwa umeandikwa kwa ajiri ya Britney Spears.


Wimbo wa Umbrella ambao alimshirikisha Jay-Z uliandikwa na watu wanne  ambao ni The-Dream, Christopher Stewart, Kuk Harrell pamoja na Jay-Z kwa ajiri ya  Britney lakini ukakataliwa, ndipo Rehanna akasema “leta huku huo wimbo”. 
  
Wimbo huo ulimpa umaarufu mkubwa sana na kuwa wimbo kinara kati ya nyimbo zilizotoka nao kwenye Albam moja. Mwaka 2007 ulipata tuzo ya MTV kama video bora, baadae ukaingia kwenye ushindani wa tuzo za Grammy mwaka 2008 kwenye vipengele vya rekodi bora ya mwaka, wimbo bora wa mwaka na wimbo bora wa kushirikiana na kumfanya Rihanna na Jay-Z waondoke na tuzo ya Grammy ya wimbo bora wa kushirikiana kwa mwaka huo.

KIM KARDASHIAN ALIVYOTANGAZA KUJITOA KWENYE MTANDAO WA KIJAMII WA INSTAGRAM

Kim Kardashian akiwa na Kanye West

Alipokuwa tayari anafuatwa na watu 5,731,011 kwenye Instagram, mwanamuziki Kim Kardashian alitangaza kujitoa kwenye mtandao huo kwa kufunga akaunti yake mwishoni mwa mwaka jana. Ni baada ya Instagram kuongeza kipengere cha vigezo na masharti ya kutumia mtandao huo Desemba 17, 2012 ambacho kingepelekea picha za watumiaji kuuzwa kwa ajiri ya matangazo pasipokuwalipa wamiliki wa picha hizo.

Maelezo yalikuwa kama ifuatavyo “Unakubari kwamba kampuni au biashara yoyote inaweza kutulipa kuonyesha picha zako, jina lako na mambo mengine kwa ajiri ya matangazo nawewe husipate malipo yoyote”.

Hata hivyo, siku moja baada ya hapo, Instagram iliwaomba radhi watumiaji wake kwa kusema  kwamba, lengo lao lilikuwa kufanya majaribio ya tekinolojia ya matangazo ya mtandao huo japo maelezo yao hawakuyaweka vizuri na watumiaji wakaelewa visivyo.

Kujitoa kwa Kim Kardashian ambaye ndiye alikuwa anaongoza kwa kuwa na wafuasi wengi akifuatiwa na Justin Bieber  aliyekuwa na wafuasi  milioni 4.3 na Obama wafuasi milioni 1.8, kungepelekea kujitoa kwa ndugu zake Khloe, Kylie, Kendall na Rob Kardashian ambao wote walikuwa katika kumi bora ya waliofuatwa na watu wengi kwenye mtandao huo kwa wakati huo.

Kim Kardashian aliendelea kubaki Instagram na mpaka kufikia mwishoni mwa September 2013 alikuwa akifuatwa na watu 9, 935, 306. Ni wa 3 kati ya akaunti 10 duniani zilizofuatwa na watu wengi kwenye mtandao huo akiwa tayari amepitwa na Justin Bieber mwenye  watu 10,822, 685 ambaye anachukua namba 2 akitanguliwa  na  Instagram yenyewe ambayo ndiyo namba 1 .

Inasemekana ujauzito wake na kujifungua vimechangia Kim kupitwa na Justin Bieber kutokana na kuwa muda mrefu mbali na Kamera na picha zake kutosambaa zaidi ikilinganishwa na awali. Kim Kardashian ni mama wa mototo wa Kanye West.

Wednesday, October 16, 2013

AKAUNTI 10 ZA INSTAGRAM ZILIZOONGOZA DUNIANI KWA KUFUATWA NA WATU WENGI ZAIDI MWISHONI MWA SEPTEMBA 2013


1. Instagram yenyewe: 38,022,266

 2.Justin Bieber: 10,822, 685

 
 3. Kim Kardashian: 9, 935, 306
 
4. Rehanna :9,783,752
5. Ariana Grande:7,150,544

6. Kendell Jenner: 6,620,755
7. Taylor Swift: 6,543,194

8. Beyonce: 6,515,223  
9. Khloe Kardashian: 6,241,358

10. Kylie Jenner: 5,907,168

'EID- EL- HAJI' YAANGUKIA 'SIKU YA CHAKULA DUNIANI'



 Eid-el-Haji imeangukia tarehe ya siku ya chakula duniani ambayo huazimishwa Octoba 16 kila mwaka. Kauli mbiu ya siku ya chakula duniani mwaka huu 2013  ni 'Sustainable Food Systems for Food Security and Nutrition'.
 
   
Semadat inakutakieni Eid njema.

Monday, October 14, 2013

ALICHOANDIKA KWENYE 'TWITTER' WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA MH. BERNARD MEMBE MAPEMA LEO OCTOBER 14, 2013 ANAPOMKUMBUKA MWL NYERERE



TAZAMA USANII WA MWALIMU NYERERE

UKITEMBELEA katika maduka ya vitabu na maktaba utakuta vitabu vilivyoandikwa na watu mbalimbali vinavyofundisha sanaa ya usemaji ‘The art of public speaking’, lakini hotuba za Mwalimu nyerere ni zaidi ya sanaa hiyo.

Pia ukisoma maandishi ya (Erick, 2009), utaona jinsi gani Mwalimu alikuwa msanii kwa kuwa aliweza kuhusianisha falsafa ya Ujamaa na moja ya kazi za sanaa za mikono ambayo ni kinyago cha Mmakonde kilichoitwa Dimoongo cha Robert Yakobo Sangwani na kupelekea sanamu au kinyago hicho kubadilishwa jina na kuitwa Ujamaa. Alikilinganisha kinyago hicho na ujamaa kutokana na muundo wake jinsi watu walivyoshikamana kila mmoja akiwa kama nguzo ya kumsaidia mwingine hasianguke. Inasemekana Mwalimu Nyerere ndiye alikibadilisha jina kinyago hicho na kukiita UJAMAA.

Kinyago  cha kimakonde kilichotolewa mfano wa Ujamaa na Baba wa Taifa Mwalimu J.K. Nyerere

Ngao (Nembo) ya Taifa ambayo ni moja ya alama za Taifa, inaonyesha sanaa na ubunifu wa hali ya juu uliomo katika alama zingine za Taifa kama Bendera, Wimbo wa Taifa na Mwenge wa Uhuru. Yaliyomo, ikiwa ni pamoja na Bibi na Bwana kama ishara ya haki sawa pasipokujali jinsia, yote ni alama ya kauli mbiu ya UHURU na UMOJA ambapo pia ni jina la kitabu cha Mwalimu Nyerere cha mwaka 1966. Pia aliandika vitabu vingi ambavyo vinapatikana makumbusho ya Mwalimu Nyerere.

Ngao ya Taifa

Kwa kuwa wasanii na wabunifu wengi walimtazama na wanamtazama Mwalimu Nyerere kama kiongozi shupavu na ‘Role Model’ wao kitaifa na kimataifa kwa jinsi ya kuonyesha matumizi halisi ya sanaa katika kujenga picha na  mawazo chanya, kwa wao pia inaweza kuwa raisi kubadilisha mawazo kuwa katika vitendo tunapoazimisha siku ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Oktoba 14, 2013.