UA-45153891-1

Tuesday, November 27, 2012

MSANII SHARO MILLIONEA AFARIKI DUNIA



Msanii wa Bongo movie na mwanamziki Sharo milionea amefariki dunia leo hii kwa ajali ya gari alipokua akielekea Muheza, Tanga., kwa habari zilizothibitishwa na msanii mwenzake wa movie Steve Nyerere, akiongea akiwa katika msiba wa msanii mwingine wa Bongo movie alifariki (John) kwa njia ya simu, akiongea kwa sauti ya masikitiko sana na Dj Fetty alisema
"ni kweli fetty sharo hatupo nae tena na nimeongea na kamanda wa polisi mkoa wa Tanga na kuthibitisha habari hizo"
 akiongea na Clouds Fm, kamanda wa polisi mkoa wa Tanga Bwana Constatine Massawe amesema " kifo cha Millionea kimetokea majira ya saa mbili, eneo linaloitwa Maguzoni songa , akiwa anaendesha gari aina ya toyota Harrier akitokea Dar  kuelekea Muheza, alipofika hapo gari liliacha barabara na kupinduka,na maiti imehifadhiwa katika chumba cha maiti ya  hospitali teule ya Muheza. alikuwa mwenyewe. Mungu ailaze roho ya marehem mahali pema peponi Amen.

Saturday, November 10, 2012

MSHINDI WA EPIQ BONGO STAR SEARCH 2012 NI WALTER CHILAMBO


 
Hawa ndio washiriki watano waliokuwa wamebakia
kutoka katika mchujo tangu ebss 2012 ilipoanza safari yake.
Kutoka kushoto ni  Nsami Nkwabi, Walter Chilambo, Salma Yusuph, Wababa Mtuka na Nshoma Ng'hangasamala            


FAINALI YENYEWE

Kushoto ni washiriki watatu ambao waliingia kumi bora na kulia ni baadhi ya washiriki watatu  ambao walifika hatua ya tano bora.Wakiwa pamoja, ni baada ya kuburudisha kwa wimbo wa pamoja muda mfupi kabla ya fainali ya shindano hilo
Washiriki watano bora wakiwa tayari kuanza kazi, wenye suti ni washereheshaji wa tukio hilo lililofanyika ndani ya ukumbi Diamond Jubilee
 Nsami Nkwabi ndiye aliyefungua dimba akisindikizwa na Barnaba.
 Kila mmoja kwanza alipanda jukwaani na mwanamuziki maarufu kwa kuimba wimbo wa mwanamuziki huyo. Hapa ni Nshoma Ng'hangasamala  akitamba na miondoko ya mwambao wa Pwani.
Salma Yusuph na Linex 
 Wababa na Mwasiti
 Walter na Ditto
 Baada ya Kolabo kila mmoja alisimama kama yeye.Huyu si mwingine bali Nsami Nkwabi !
Baada ya Nsami alifuata Nshoma.Hawa wawili ni mtu na dada yake.
 Salma!!!!!  Msichana mwenye kipaji cha  pekee
 
 Wengine wanamuita "Wafather", wengine "Wadad", huyu si mwingine ni Wababa akiokota mshiko baada ya kuwapa raha mashabiki wake.



Walter  Chilambo  akifanya mambo
 MC’s kijana mtanashati Caesar Daniel na mwana dada mrembo Vanessa Mdee ndio wanasongesha show nzima ya Epiq Bongo Star Search
Majaji wa Epiq Bongo Star Search wakiwa kazini! 
Mashabiki wa Walter wakifanya vitu vyao!
 Na mashabiki wa Wababa kama kawaida!
 Mshindi wa BSS 2010 akitoa burudani
Show ilisindikizwa na burudani toka kwa wasanii  mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya
THT Dancers
  Ommy Dimpoz 


 Linah na Amin
 Mzee Yusuph
 Washiriki watatu waliendelea kubaki kati ya hawa
 Salma Yusuph
 Wababa Mtuka
 Walter Chilambo 
 
 Wote wanaweza lakini mshindi lazima apatikane.Mmoja wao aliishia hapa kimashindano
Aimbapo utatamani kumtunza lakini waweza shindwa kutokana na sauti yake nzuri na hisia zitakavyokugandisha kwenye kiti ulichokalia 
 Bila kujali mwanamuziki ni wa jinsia gani,inasemekana shabiki namba moja wa mwanamuziki ni mwanamke, alafu mwanaume anafuata. Wanawake wanashangilia, wanatunza, wanapiga kura. Pamoja na uwezo na sauti nzuri aliyonayo Walter Chilambo,unazani  pia alifanikiwa katika hilo?.Pia nakumbuka maneno ya jaji Master J aliposema,"Walter pamoja na sauti yako nzuri una bahati sketi zinakuzimia, kila la kheri".
 Haya sasa!
Chief Judge wa EBSS Bi. Lita Paursen maarufu kama Madam Lita, akitoa maelezo mafupi kabla ya kumpa CCO wa Zantel nafasi amtangaze mshindi 
CCO wa Zantel ambao ndio wadhamini wa shindano hilo akisubiri kuondoa kiu ya matazamaji. 
Walter Chilambo baada ya kutangazwa mshindi wa EBSS 2012 
Madam Lita akimpoza Salma nakumpongeza kwa hatua nzuri aliyofikia 
 Walter akikabidhiwa zawadi yake ya milion 50Tsh
 Walter akiondoka baada ya kufanya yake

Wednesday, November 7, 2012

MISS TANZANIA 2012 NI BRIGITTE ALFRED


Rangi mbalimbali za mavazi zilipamba jukwaa vilivyo
 
Walipendeza kweli kweli!
 Mambo yalikuwa mazuri ndani ya Ubungo Plaza
Majaji walikuwa na kazi
MCs
 Kumpata mrembo zaidi kati ya warembo kama hawa ni shughuri!!!
Kama maua
 Miondoko ya kiulimbwende
Wakisomwa washindi watano bora
Watano bora (Top five)
 Maswali kwa warembo waliofika hatua ya tano bora
 Baadhi ya watazamaji 
 Miss Tanzania 2011 akijiandaa kukabidhi kwa Miss Tanzania 2012
Diamond akiburudisha
Rachel nae akifanya vitu vyake
Miss Tanzania 2012 Brigitte Alfred
Miss Tanzania 2012 akiwa na wenzake walioingia tano bora, karibu nae kushoto ni Miss Tanzania 2011
Miss Tanzania 2012 akiwa na mshindi wa pili na watatu
Miss Tanzania 2012 akikabidhiwa funguo za gari
Gari alilozawadiwa Miss Tanzania 2012
 Miss Tanzania 2012 akifungua mlango kuingia kwenye gari alilozawadiwa
 Akiwasha gari
Red  Carpet-Genevieve
 Lisa
Rachel
Alexia
Lina
 Jackline