UA-45153891-1

Wednesday, February 26, 2014

KITABU ANACHOSOMA LOVENESS LOVE 'DIVA' KWA SASA


Kuwa mtangazaji, mwandishi  au mwanahabari kwa namna yoyote inakupasa pia kuwa msomaji wa maandiko na vitabu mbalimbali hasa vinavyohusu kipengele husika cha habari  zako. Inaelekea mwanadada huyu alishasoma vitabu vingi na bado anaendelea kusoma.  Kwa sasa anasoma kitabu hiki.

UNGEKUWA 2FACE IDIBIA UNGEJISIKIAJE KWA HILI?


Kweli unapokuwa mtu maarufu jiandae kwa lolote litakalokutokea kuanzia kwenye jamii mpaka vyombo vya habari, hasa mitandao ya kijamii. Jibu la swali hili linaweza kuwa "Vibaya!!!", ingawa naamini kwa  Staa yeyote, jibu linatakiwa kuwa  "Kawaida!!!". Na inabidi litolewe kwa kumaanisha, sio tu kwa sababu linatakiwa kuwa hivyo.

ELIZABETH MICHAEL 'LULU' ANAVYOTUMIA MITANDAO YA KIJAMII


Kama ilivyowai kuandika mwandishi mmoja wa mtandao unaoitwa 'Social Media today' kwamba tunakoelekea mitandao ya kijamii itakuwa kwa ajili ya kuonyesha badala ya kuandika hivyo kila mtumiaji atakuwa na Kamera ya picha za Still na ya Video, ndivyo anavyoonyesha muigizaji Elizabeth Michael 'Lulu'. Star huyo wa Bongo Movie ambaye hapitishi siku zaidi ya moja kabla hajasalimia na kuzungumza kwa picha na maneno mawili mpaka matatu tu kila siku kwenye ukurasa wake wa Facebook, Jana Jumanne Februari 25, 2014 alikuja kwa mtindo huo. Tazama zingine mbili za  Jumapili na Jumatatu iliyopita na alivyoandika.

PICHA ZA VIDEO YA DIAMOND NA D'BANJ KAMA VIRUSI


Ikiwa ni masaa machache tangu mwanamuziki staa wa wimbo wa 'Number One' Diamond Platnumz alipoweka picha za Video ya Project ya 'Do agric' anayofanya na mwanamuziki wa nchini Nigeria D'Banj,zimesambaa kwenye  mitandao mbalimbali ya Afrika mashariki kama virusi au kwa lugha nyingine wanasema zimekuwa 'Viral' ambapo mitandao imezichukua na kuzizungumzia  ikiwa pamoja na mtandao wa 'vibeweekly.com' ulioandika kichwa cha habari "Diamond Releases Behind The Scenes Photos Of His Video With Dbanj" na kuandika haya  juu ya msanii huyo.

'LIPSTICK' NA 'LIPGLOSS' ALIZOZINDUA MSHINDI WA BIG BROTHER 2013 DILLISH MATHEWS


Mshindi wa Big Brother 2013 Dillish Mathews, anaendelea kutumia jina lake kubuni bidhaa mbalimbali ambapo siku chache zilizopita ndani ya mwezi huu wa Februari 20, 2014, alizindua bidhaa za urembo ikiwa pamoja na 'Lipstick' na 'Lipgloss' .Wengi wamekuwa wakisuburi ni jambo gani litafuata kuhusu Dillish ikiwa ni muda mfupi sasa tangu aachane na mpenzi wake Stephen kwa sababu anategemea kupata mtoto kutoka kwa mwanamke mwingine.  

Mwanadada huyo ambaye pia siku chache zilizopita alikuwa nchini Nigeria kwenye maandalizi ya filamu, alizindua vipodozi hivyo ndani ya jiji la Windhoek nchini Namibia. Hizi ni baadhi ya aina za bidhaa zake alizozindua kama zinavyoonekana.

Tuesday, February 25, 2014

OMOTOLA APEWA SOMO NA WANAHABARI NCHINI NIGERIA

Omotola Jalade

Siku chache zilizopita, mtoto wa muigizaji wa kike maarufu nchini Nigeria Omotola Jalade-Ekeinde alisherehekea siku ya kuzaliwa  na kuweka baadhi ya picha zake kwenye mtandao wa Instagram.  Blogger s wa nchini humo walizichukua picha hizo za mtoto wa miaka 14 anayeitwa Meraiah Ekeinde na kuziweka kwenye Blog zao ikiwa pamoja na kuzizungumzia. Kupitia mtandao wa Facebook, Omotola aliwashukuru  waandishi hao kwa kumtakia mwanae furaha ya siku ya kuzaliwa ingawa pia aliwaonya na kukemea kitendo cha  kutumia picha za mtoto mdogo hasa wale ambao  walioandika maneno “hot and sexy”. Hivi ndivyo alivyoandika kwenye ukurasa wake wa Facebook, pia sehemu ya barua ya wazi aliopewa na mmoja wa waandishi wa habari za burudani mitandaoni nchini Nigeria, anayeitwa . Osagie Alonge.

TUNDAMAN WA TIP TOP CONNECTION ANAPOSEMA “MKATABA WA KIROHO”


Wiki iliyopita kulikuwa na taarifa juu ya wanamuziki wa Bongo Flava waliojitoa Tiptop Connection kutaka kurejea tena ikiwa pamoja na MB Dogg, Spark na Keisha. Alipoulizwa msanii mwenzao Tundaman juu ya suala hilo alisema,

WALTER CHILAMBO AMALIZA MKATABA WAKE NA ZANTEL


Mshindi wa Bongo Star Search 2012 Walter Chilambo amemaliza mkataba wake na kampuni ya simu ya Zantel ambao ndiyo mdhamini wa shindano hilo linafanyika kila mwaka chini ya kampuni ya Benchmark Production.

SASA KUNA WAZEE WA NGWASUMA NA VIJANA NGWASUMA


Bila shaka wengi wanaifahamu bendi ambayo ni miongoni mwa zile  maarufu hapa nchini, inayoitwa FM Academia ‘Wazee wa ngwasuma’. Baada ya bendi hiyo kuwa na wanamuziki wengi mpaka kufikia kiasi kwamba wengine wanafanya vizuri nyuma ya vipaza sauti na vyombo  vingine vya muziki lakini hawajulikani  kwa muda mrefu japo kazi nzuri inaonekana, baadhi yao wamehamua kujitoa na kuanzisha bendi nyingine inayoitwa  ‘Vijana wa ngwasuma’. 

NDOTO ZA KITAA ZAZINDULIWA CLOUDS TV


Ni mpango wa kubadili fikra za watu na kuwafanya wafikie ndoto zao . Akizungumza kupitia Clouds FM, Mkurugenzi wa vipindi wa Redio hiyo Ruge Mutahaba alisema,

Monday, February 24, 2014

"UMAARUFU HAUJI KWA SHORTCUT"- BATULI


Ndivyo alivyosema muigizaji 'Batuli' kupitia ukurasa wake wa Facebook takribani wiki moja iliyopita. Mwanadada huyo ambaye anajitaidi kuitumia mitandao ya kijamii kujitangaza, alikuwa akijibizana na mmoja wa mashabiki zake kupitia mtandao huo.

SEMADAT: WAWILI KWA PICHA

Leo tuko na Shilole na Masanja Mkandamizaji

"HAPANA INAWEZA KUWA BARAKA"-MWAMVITA MAKAMBA

Ndivyo alivyosema Mwamvita Makamba, mbobevu wa masuala ya mawasiliano, uhusiano na masoko kupitia akaunti yake ya Facebook siku moja baada ya mtandao wa kijamii wa 'Whatsapp' kununuliwa na kampuni ya Facebook Inc.

KWANINI FACEBOOK WAMEINUNUA WHATSAPP KWA DOLA BILIONI 19?

CEO wa Whatsapp Jan Koum

Mnamo  Februari 19, 2014, Facebook walitangaza kuinunua Whatsapp kwa  kiasi cha dola bilioni 19, ambapo  WhatsApp kama yenyewe ni  $16 bilioni na $3 billioni kwa ajili pia ya kuwachukua wafanyakazi  wake. Jina la mtandao huo halitabadilika na utaendelea kufanya kazi kwa kujitegemea  lakini chini ya uongozi wa Facebook. CEO wa Whatsapp  Jan Koum ambaye pia ni mmoja wa waanzilishi wa mtandao huo  amekuwa mmoja wa wajumbe wa bodi ya kampuni ya Facebook Inc.

Mitandaoni na kwenye vyombo vingine vya habari iliibuka mijadala ukiwemo wa  kwamba, Je kweli mtandao huo wa kijamii ulioanzishwa na Jan Koum na Brian Acton ulikuwa na thamani ya kununuliwa na Facebook kwa kiasi hicho cha fedha?.  Jibu rahisi kwa walio wengi ni “Hapana”, japo inaweza kuwa kinyume na hivyo au ikawa ni hivyo leo lakini kwa faida ya kesho. 

Zifuatazo zilikuwa  sababu za Facebook kuununua mtandao huo.

Saturday, February 22, 2014

WANAHARAKATI WA SANAA KWENYE BUNGE LA KATIBA

Waliowakilisha katika muziki ni pamoja na mtayarishaji wa muziki 'Producer' wa Bongo Records P. Funk na katika filamu  ni pamoja na muigizaji 'Dude'  .Picha inayofuata ni katika kikao.

"AFRIKA HAKUNA UHURU WA KWELI"


Amesema mwanahiphop mashuhuri wa hapa nchini Tanzania 'Fid Q' kupitia ukurasa wake wa Facebook unaopendwa na watu zaidi ya 94, 780. Baadhi yao walikuwa na haya  ya kusema.

ELIZABETH MICHAEL 'LULU' AONYESHA TATUU YAKE ILIYOANDIKWA "ONLY GOD CAN JUDGE ME"


Ikiwa ni muda mfupi tu tangu staa wa Bongo Movie Elizabeth Michael 'Lulu' alipoandika kupitia ukurasa wake wa Facebook kwamba watu wanaendelea kumuandama japo hakusema ni juu ya nini.Kwa sasa ameweka picha kwenye ukurasa wake huo wa Facebook inayoonyesha alama ya 'tatuu' iliyoandiikwa "Only God can Judge me". Muigizaji huyo ambaye kila siku huibuka na picha ya pozi moja, mbili au tatu na kuitupia mitandaoni, ameweka picha zake ndani ya siku tatu kama ifuatavyo:

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2013

Kuona matokeo ya kidato cha nne 2013 BOFYA HAPA

Friday, February 21, 2014

RIHANNA ALIVYOSHEREHEKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA JANA


Ilikuwa Februari 20, 2014 ndani ya jiji la Aspen jimboni Colorado nchini Marekani. Tazama picha zaidi.

NYIMBO TANO ZA KUSIKILIZA KILA UNAPOAMKA

1.Jikubali -Ben Paul

MASHABIKI WA ELIZABETH MICHAEL 'LULU' WAMTIA MOYO




Ni baada ya muigizaji huyo wa Bongo Movie kuandika kwenye ukurasa wake wa facebook leo mapema kwamba kwanini watu wanaendelea kumuhukumu kwa??, hakumalizia bali aliishia hapo. Mashabiki na wafuasi wake walikuwa na haya ya kusema.

RAIS ROBERT MUGABE ATIMIZA MIAKA 90 LEO...!

Rais Robert Mugabe

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ambaye alizaliwa February 21, 1924 ametimiza miaka 90 leo February 21, 2014. Kabla ya uongozi, baada ya kumaliza masomo yake aliajiriwa kama mkufunzi katika chuo cha ualimu cha Chalimbana. Ni watatu kati ya watoto sita katika familia yao na kaka zake wawili wakubwa walifariki dunia akiwa mdogo. Rais Mugabe ameiongoza nchi yake kwa miaka 33 mpaka sasa. HAPPY BIRTHDAY ROBERT MUGABE.

UMASOGANGE NI AJIRA NZURI KINADADA WAKITUMIA FURSA VIZURI


 Agnes Gerald ‘Masogange’

Baada ya kukutana na  habari flani mtandaoni, mwanamuziki wa Bongo Flava Khalid Ramadhani a.k.a Tundaman akiliambia gazeti la Starehe kwamba warembo wanaotumika katika video zake kama 'video vixens' au kwa hapa Bongo maarufu kama ‘video queen’ wengi huwa anaelewana nao tu kwani ni wachache huwalipa ujira na wanaolipwa ni pesa kidogo isipokuwa Agnes Gerald ‘Masogange’ aliyehusika katika video ya Msambinungwa, ndipo 'Semadat Blog' ikatumia neno 'umasogange' kuwakilisha fani hiyo.

“Katika video zangu zote hakuna video queen niliyewahi kumlipa zaidi ya milioni moja ila Masogange nimemlipa shilingi......

Thursday, February 20, 2014

RIHANNA ATIMIZA MIAKA 26


Leo ni siku ya kuzaliwa ya mwanamuziki Rihanna wa nchini Marekani ambaye ametimiza miaka 26. Alizaliwa Februari 20, 1988. Fahamu mambo matano kuhusu yeye.

UHUSIANO WA LINEX NA MASOGANGE 'BLOGGERS' WAOMBWA KUPATA UHAKIKA WA HABARI


Mwanamuziki wa Bongo Flava Linex Sunday 'Afande Mjeda' ametoa malalamiko yake kwa 'Bloggers' walioandika kwamba ana uhusiano wa kimapenzi  na muigizaji maarufu wa Video za muziki hapa nchini Agnes Gerald 'Masogange'. Linex amesema hakuna kinachoendela kati yao zaidi ya ukaribu unaotokana  na uhusiano wa kikazi hasa ikizingatiwa kwamba mwanadada huyo anafanya kazi na wasanii wa muziki. Pia amewaomba waandishi hao wa magazeti tanzu kupata uhakika kwa kufanya mawasiliano nae kabla halijatokea jambo kama hilo linalomuhusu.

NAPE NNAUYE ASHUKA MASHAIRI REDIONI, AMKUBALI MWANA FA, JAYDEE, BANANA, LINAH NA BARNABA


Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Nape Nnauye alisikika jana Redioni akiimba. Ni baada ya kuulizwa ni kitu gani anapenda kufanya mbali na kazi zake ambapo alisema yeye anapenda muziki na anaweza kuimba na kupiga vyombo vya muziki ikiwa pamoja na Kinanda, Gitaa na Drums. Nape ambaye alisema ana vyombo vya muziki nyumbani kwake ambavyo huvitumia kupiga na kufurahia muziki, aliendelea kusema alipata uzoefu wa fani hiyo siku za nyuma akiwa pamoja na 'Captain' Komba kwenye shughuri hizo za kimuziki.

MAN WALTER, 20 PERCENT NA SAKATA LA WIMBO WA SUBIRA



Man Walter (Kushoto)
 
Mtayarishaji wa muziki hapa nchini Tanzania Man Walter, amesema hana tatizo wala ugomvi na msanii 20 Percent japo ameshangazwa na kitendo cha msanii huyo kurekodi wimbo wa 'Subira' katika studio nyingine bila taarifa  mbali na kwamba yeye ndiye alikuwa tayari ametengeneza 'Demo' ya wimbo huo. Wawili hao wanafahamika kama washirika wazuri ambao wamefanya kazi nyingi wakiwa pamoja kwa muda mrefu.

JOSE CHAMELEONE, WYRE SAMBAMBA NA JAY-Z NA KANYE WEST KWENYE 'TUZO ZA WORLD MUSIC'

Jose Chameleone

Wanamuziki wawili wa Afrika Mashariki, Wyre wa nchini Kenya na Jose Chameleone, wameingia kwenye kinyang'anyilo cha tuzo za World Music kipengele cha Msanii bora wa kiume. Wengine ambao wako kwenye kipengele hicho ni pamoja na Jay-z na Kanye West wote wakitokea nchini Marekani.

Wednesday, February 19, 2014

MTOTO HUYU NI KAMA ANAJUA HUYU NDIYE RAIS WA MAREKANI


MTOTO HUYU NA KATIBA...! AKIWA MKUBWA LAZIMA ATAISOMA TU...!

Pongezi nyingi zimuendee  aliyempiga picha hii.

PICHA ALIYOWEKA LADY JAYDEE 'FB' USIKU WA KUAMKIA LEO

 

Na haya ni maoni ya mashabiki wake.

'UMEMISS' KUMUONA NYOTA NDOGO?... BASI TAZAMA PICHA HII

Mwanamuziki wa nchini Kenya aliyewai kukuletea nyimbo kali kama 'Mpenzi (Nibebe)' na 'Watu na Viatu'. Aliingia kwenye kipengele cha wimbo bora wa Afrika Mashariki kwenye tuzo za muziki za Kilimanjaro za hapa nchini Tanzania mwaka 2007.

2FACE IDIBIA AKANUSHA KUMPA UJAUZITO AFISA WA BENKI


Mwanamuziki wa Nigeria 2Face Idibia amekanusha juu ya habari zilizoandikwa katika Blog na mitandao mingine ya kijamii nchini humo kwamba amempa binti mwingine ujauzito. Mwanadada anayehusishwa na habari hiyo anaitwa Teniola ambaye ni mfanyakazi wa Benki moja nchini humo akitokea eneo la Ado-Ekiti na alisoma chuo kikuu cha Lagos. Inasemekana amekuwa akisimamia kwa karibu akaunti ya 2Face na kumuhudumia kibenki kwa muda mrefu katika benki hiyo na 2face alitaka ujauzito huo wa miezi mitatu uondolewe akimuomba kwa ahadi ya kumnunulia gari jipya ili mambo yaishe chini kwa chini pasipokujulikana.

2face amekanusha na kusema taarifa hizo ni uongo kwa asilimia 100,huku akilaani na kueleza hisia zake kupitia mtandao wa Twitter.

Tuesday, February 18, 2014

FLAVIANA MATATA ATAKA KUJUA WIZARA INAYOSIMAMIA BURUDANI NA MITINDO



Ndivyo alivyouliza kupitia akaunti yake ya Twitter usiku wa kuamkia leo.

SIKU YA KUZALIWA DR. DRE....!!!

Dr. Dre
Ukimwambia mtayarishaji yeyote wa muziki ulimwenguni akutajie watu wawili anaowatazama ili  kupata hamasa ya kufika mbali, ni jambo la kawaida kumtaja Dr. Dre akiwa wa kwanza . Kwa jina halisi anaitwa Andre Romelle Young na alizaliwa February 18, 1965.

Ni mtayarishaji wa muziki ‘Producer’ maarufu nchini Marekani na dunia nzima, pia ni rapper, mwanzilishi na CEO wa makampuni ya Aftermath Entertainment na Beats Electronics. Biashara yake ya ‘Headphones’ imemtangaza sana pande mbalimbali za dunia.

Monday, February 17, 2014

TUZO ZA MUZIKI ZA KILIMANJARO TANZANIA (KTMA) 2014 ZAZINDULIWA LEO, MABORESHO YAONGEZWA



Tuzo za  muziki za Kilimanjaro mwaka 2014 zimezinduliwa leo  February 17, 2014 na  mabadiliko kadhaa yakiwa yamefanyika.Tuzo hizo ambazo hutolewa kwa wasanii wa muziki mbalimbali wa Tanzania zilianzishwa mwaka 1999.

George Kavishe kutoka TBL ambao ndio wadhamini wa tuzo hizi amesema maboresho makubwa ambayo yamefanyika mwaka huu ni tofauti na mara zote ambazo wamekua wakihusisha watanzania dakika za kupiga kura tu na hivyo kukosa nafasi ya kupendekeza nani aingie kwenye kipengele 'category' gani. "Mwaka huu tumebadilisha kutokana na matakwa ya soko hivyo Watanzania ndio watapendekeza nani aingizwe kwenye category gani. Kupitia Magazeti, website ya Kilimanjaro na vipeperushi kuanzia kesho February 18 2014 kutaonyeshwa category zote za mwaka huu za kupigiwa kura na wananchi na watanzania watatuma kura zao kupitia simu za mkononi kupitia 15440, ambapo kila mmoja atapendekeza msanii, kikundi au producer gani aingie kwenye kipengele flani", alisema Kavishe.

'WANURI KAHIU' MUONGOZAJI WA FILAMU ALIYESIMAMA JUKWAA MOJA NA BILL GATES


Mwanadada 'Wanuri Kahiu' ambaye ni muongozaji na mtayarishaji wa filamu, aliwawakilisha vizuri wakenya na wanaafrika  mashariki kwa kupata nafasi ya kuzungumza kwenye tukio la TED-X. Alizungumza juu ya filamu yake ya Pumzi, uzoefu wake katika msuala ya filamu na jinsi anavyojisikia juu ya 'Label' anazofanyia kazi.

LUPITA NYONG'O ATANGAZWA KATI YA WANAWAKE 99 WENYE MVUTO DUNIANI


Neno mvuto lina maana pana sana. Wasichana na wanawake wazuri wako kila kona ya dunia,hata hivyo wenye mvuto zaidi na ushawishi katika jamii mara nyingi ni wale wenye kujituma, kufanya kazi kwa bidii kwa uwezo wao, ujuzi walionao na vipaji walivyopewa. Ndiyo maana haikuwashangaza watu pale muigizaji wa Hollywood anayetokea nchini Kenya Lupita Nyong'o alipowekwa kwenye orodha ya mtandao wa "AskMen.com" akiwa miongoni mwa wanawake 99 wenye mvuto na ushawishi mkubwa dunianim mwaka huu 'Most desirable women 2014'.

ERICK OMONDI ALIVYOSHEREHEKEA SIKU YA WAPENDANAO "VALENTINE"


Siku ya wapendanao 'Valentine' ni miongonimwa siku zenye umaarufu mkubwa ulimwenguni na kwa maana nzuri ni siku amabayo watu wanaweka chini tofauti zao na kuonyeshana upendo. Sio tu kwa mtu na mwenza,  kwa familia na marafiki bali pia kwa watu au makundi ya watu wanaojihisi kutopendwa.

VANESSA MDEE NA MIAKA 25 YA NARIA STOPES NCHINI TANZANIA


Ilikuwa ndani ya siku ya Valentine. Akiwa anafahamika kama mtamgazaji, mwanamuziki na mdau mkubwa wa masuala ya kijamii, alionekana kwenye picha aliyoweka kwenye ukurasa wake wa Facebook na kuandika hivi.

PICHA BORA YA VALENTINE 2014


Katika pitapita za hapa na pale mitandaoni, Semadat imeichukua picha hii kama picha bora ya 'Valentine' katika picha zote zilizotumika au zilizowekwa mitandaoni kuhusiana na siku hiyo.Hii ilikuwa kwenye mtandao wa 'secure.give2gether.com' katika kampeni ya kuchangia kiasi flani cha fedha ndani ya msimu wa Valentine ili kuwasaidia watoto kupitia mpango ya "Save a Child's".

Friday, February 14, 2014

WEMA SEPETU AANZA KUYAISHI MAISHA YA NDOTO ZAKE



Muigizaji maarufu wa kike nchini Tanzania na mwanamitindo ambaye alikuwa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu amesema maisha anayoyaishi kwa sasa akiwa na Diamond Platnumz, ni maisha ya ndoto zake ambayo alikuwa akiyaota muda mrefu. 

WALAKA WA NICK WA PILI "THAMANI YA SANAA NI KICK?"


"Thamani ya sanaa ni  kick?". Anauliza Nick wa  pili.  Ni baada ya kupigiwa sana simu na wasanii wengi ambao bado hawajafahamika kwenye 'industry' ya muziki wakimuomba kuonana nae ili awaunganishe watu wa vyombo vya habari ikiwa pamoja na watangazaji wa Redio na Televisheni ili wasukume kazi zao mbele kwa kuzipa kile kinachofahamika kama 'Airtime'.Pia wengine wamekuwa wakimuomba ashirikiane nao katika nyimbo zao au kwa lugha iliyozoeleka kufanya nao  'Kolabo. Akisoma  walaka huo kupitia East African Radio jana, msomaji aliendelea kushuka kwamba wapo wanaoomba pesa ya kurekodi wakati ndo kwanza wameandika wimbo mmoja.

SIKU YA REDIO DUNIANI- WANAWAKE KUPEWA NGUVU KATIKA FANI ZA UTAYARISHAJI NA UTANGAZAJI

Baadhi ya waliokuwa wanahabari wa Radio Tanzania wakiwa na hayati Baba wa Taifa Mwl.J.K. Nyerere

Tarehe ya February 13 kila mwaka ni siku ya Redio duniani ambayo huazimishwa na Redio zote duniani kama moja ya vyombo vya habari muhimu ikiwa ni pamoja na kuongeza ushirikiano wa kimataifa kati ya vyombo vya habari vinavyorusha matangazo hewani, kuongeza uwezo wa kupata taarifa, uhuru wa kujieleza na usawa wa jinsia.

Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la UNESCO ambalo ni mdau mkubwa wa siku za kimataifa ikiwa pamoja na siku hii, redio inaendelea kukua katika zama hizi za Digitali na inaendelea  kubaki kama chombo cha habari ambacho kinawafikia watu wengi duniani kote. Hivyo ni fursa muhimmu kutangaza usawa wa jinsia na kuwapa nafasi wanawake.

Katika kusherehekea siku ya Redio duniani kote, UNESCO wanaupa nguvu usawa wa jinsia kwa kufanya haya yafuatayo:

Thursday, February 13, 2014

NANCY SUMARI AFANYIWA USAILI NA TAASISI YA KIMATAIFA YA 'ONE' KUPITIA TOVUTI YA ONE.ORG



"So excited to have been featured on http://ONE.org  recently... Check out my interview here!". Ameandika Nancy Sumari kupitia akaunti yake ya Twitter leo February 13. ONE ni taasisi ya kimataifa inayojihusisha na masuala ya kupambana na umasikini duniani kote yenye washiriki zaidi milioni 3 kama mawakala  wanaopambana na umasikini uliopitiliza  na magonjwa yanayozuilika 'Preventable disease'  hasa barani Afrika. Nancy Sumari ambaye alkuwa Miss World Afrika 2005, amepata fursa ya kuzungumza juu ya harakati zake kupitia tovuti ya taasisi hiyo inayoitwa one.org.  

JANUARY MAKAMBA NDANI YA KONGAMANO LA MFUMO WA DIGITALI ARUSHA



Ikiwa leo ni siku ya Redio duniani ambayo imeangukia katika siku nne za kongamano la masuala ya habari kwa kutumia mfumo wa Digitali linaloendelea jijini Arusha, Mbunge wa jimbo la Bumbuli na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mhe. January Makamba ameandika kwenye akaunti yake ya mtandao wa Twitter akiwa kwenye Kongamano hilo kwamba ni wakati wake kuzungumza.

Kongamano hilo la jumuiya ya nchi za Commonwealth linaitwa 'Digital Broadcasting Switchover'(#DBS2014) lililoanza Februari 11,2014 na litakalomalizika Februari 14, 2014 linazungumzia masuala mbalimbali ya mawasiliano ikiwa pamoja na changamoto zinazojitokeza katika kuhama kutoka mfumo wa Redio na Televisheni wa Analojia kwenda wa Digitali.

MAJINA YA WATANGAZAJI WA RADIO TANZANIA MIAKA YA 70, 80 na 90



 Moja ya picha za kumbukumbu- Wanahabari wa Radio Tanzania kipindi hicho wakiwa na hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere

Ikiwa ni siku ya Redio duniani, hebu tujikumbushe majina ya watangazaji wa Zamani wa Radio Tanzania-RTD kati ya miaka ya 70s, 80s na 90s waliovuma katika Idhaa zetu za Kiswahili na Kiingereza kupitia Radio Tanzania Dar es salaam (RTD). Wakati huo radio zilizotumika alimaarufu kama redio za phillps, national, panasonic na Nationalpanasonic au maarufu kwa jina la dudu proof

Orodha ya Majina haya hapa:
  •     Abdallah Iddrissa Majura–Michezo
  •     Abdallah Mlawa—Kijaruba, Ombi lako
  •     Abdul Ngarawa -Taarifa ya Habari & Mazungumzo baada ya habari
  •     Abisai Steven
  •     Abou Liongo–Michezo
  •     Ahmed Jongo–(Mpira, na mnazi wa kutupwa wa yeboyebo)
  •     Ahmed Kipozi–Mpira

BILA SHAKA ULISHAMSIKIA MTU ALIYEITWA 'CHARLES DARWIN'


Leo February 12, ndiyo tarehe aliyozaliwa Mwanasayansi wa nchini Uingereza 'Charles Darwin'. Alifahamika kama Baba wa Sayansi ya hatua za mabadiliko ya viumbe hai na visivyo hai, ambayo huchukua miaka mingi sana 'Evolution Science'. Kwa mfano ukitaka kufahamu miamba inatokana na nini, hatua za  mabadiliko ya Binadamu na mengine  mengi yanayofanana na hayo ambayo yameandikwa kwenye vitabu.

Charles Darwin alizaliwa February 12, 1809 na kufariki Dunia  April 19,  1882.

DIAMOND PLATNUMZ AKIWA NYUMBANI KWAO TANDALE JANA


Hivi ndivyo alivyosema Diamond kupitia ukurasa wake wa Facebook ikiwa pamoja na kutupia picha hiyo jioni ya jana Jumanne Februari 11, 2014 akiwa nyumbani Tandale.

LINAH SANGA WA THT KAMA MAMA YAKE.....!

Wiki moja iliyopita, muimbaji wa kike wa THT Linah Sanga aliweka kwenye akaunti yake ya Intagram picha iliyounganishwa na ya mama yake,  kama inavyoonekana hapo juu. Mashabiki na wafuasi wake walikuwa na mengi ya kuchangia.