UA-45153891-1

Saturday, February 1, 2014

FAHAMU MAMBO 10 KUHUSU MUIGIZAJI MKENYA WA HOLLYHOOD ‘LUPITA NYONG’O'


1. Wakati yeye alitangazwa na jarida la Forbes kama miongoni mwa waafrika wadogo 20 wenye nguvu mwaka 2013, binamu yake aitwaye Isis Nyong’o naye alishatajwa kama mmoja wa kundi hilo mwaka 2011.

2.  Binamu yake mwingine, Tavia Nyong’o, ni a Profesa  katika chuo  cha sanaa cha NYU’s Tisch.

3.  Lupita alizaliwa Mexico, akakulia Kenya na kusomea nchini Marekani

4.  Ni mtoto wa mwanasiasa maarufu nchini Kenya Peter Anyang' Nyong'o

5.  Alimaliza masomo yake ya sanaa ya maigizo katika Chuo kikuu cha ‘Yale’ na mwaka 2009 alipata tuzo nyingi ikiwa pamoja na za MTV na za Oscar.

6.   Anazungumza lugha zaidi ya tano ikiwa pamoja na Kiingereza, Kiswahili, Spanish kiitaliano na lugha yake ya asili Kijaluo.

7. Ana uwezo mkubwa pia katika fani ya mitindo ambapo alitajwa na jarida la Vogue kama mmoja wa mastaa wanaokuja juu na watakaofanya vizuri katika fani hiyo mwaka 2014, pia alipewa taji la Golden Globes, kama mmoja wa  waliopendeza “Kutokelezea ndani ya vazi la  ‘Ralph Lauren’

8. Wabunifu wa mavazi anaowakubali zaidi ni pamoja na Antonio Berardi, Erdem, Prada and Miu Miu.

9.  Lupita anasema alitamani kuanza kuigiza baada ya kumuona Whoopi Goldberg akitajwa kwenye tuzo za Oscar kupitia filamu yake ya mwaka1985 ‘The Color Purple’.

10. Mbali na kuigiza pia ni mtayarishaji mzuri katika tasnia ya filamu ambapo mwaka 2009, aliandiaka,  akaongoza na kutayarisha  ‘Documentary’ inayoitwa ‘ In My Genes’ ambayo inazungumzia maisha ya unyanyapaa wa Albino wa  Kenya.

No comments:

Post a Comment