Baadhi ya waliokuwa wanahabari wa Radio Tanzania wakiwa na hayati Baba wa Taifa Mwl.J.K. Nyerere
Tarehe ya February 13 kila mwaka ni siku ya Redio duniani ambayo huazimishwa na Redio zote duniani kama moja ya vyombo vya habari muhimu ikiwa ni pamoja na kuongeza ushirikiano wa kimataifa kati ya vyombo vya habari vinavyorusha matangazo hewani, kuongeza uwezo wa kupata taarifa, uhuru wa kujieleza na usawa wa jinsia.
Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la UNESCO ambalo ni mdau mkubwa wa siku za kimataifa ikiwa pamoja na siku hii, redio inaendelea kukua katika zama hizi za Digitali na inaendelea kubaki kama chombo cha habari ambacho kinawafikia watu wengi duniani kote. Hivyo ni fursa muhimmu kutangaza usawa wa jinsia na kuwapa nafasi wanawake.
Katika kusherehekea siku ya Redio duniani kote, UNESCO wanaupa nguvu usawa wa jinsia kwa kufanya haya yafuatayo:

- Kuwahamasisha wamiliki wa vyombo vya habari, viongozi, waandishi wa habari na serikali za nchi kuandaa sera madhubuti na mikakati ya redio inayohusiana na usawa wa jinsia.
- Kukuza ujuzi kwa vijana katika fani za utayarishaji wa vipindi vya redio kwa kuwalenga zaidi wasichana kama watayarishaji na pia watangazaji.
- Kusisitiza usalama wa wanahabari wa kike.
- Kuzikaribisha nchi zote kusherehekea siku ya redio duniani kwa kuweka mipango kazi kwa kushirikiana na redio za mikoa, za kitaifa na za kimataifa, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, vyombo vya habari vyote na umma kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment