UA-45153891-1

Tuesday, February 25, 2014

TUNDAMAN WA TIP TOP CONNECTION ANAPOSEMA “MKATABA WA KIROHO”


Wiki iliyopita kulikuwa na taarifa juu ya wanamuziki wa Bongo Flava waliojitoa Tiptop Connection kutaka kurejea tena ikiwa pamoja na MB Dogg, Spark na Keisha. Alipoulizwa msanii mwenzao Tundaman juu ya suala hilo alisema,
“Waliondoka wakati viongozi hawajaridhia, viongozi wetu akiwemo Babu Tale na Abdul Bonge walitulea na kutufikisha hatua nzuri bila mkataba wa kuwafanya wao wanufaike kwa kila tunachokipata, badala yake  ilikuwa kama mkataba wa kiroho ambao ni wa matakwa na husingeweza kumzuia mtu kuondoka.
Mkataba huo unawafunga kwa kuwafanya waone aibu na ndiyo maana wanarudi”. 

 Tundaman ambaye anafanya vizuri na kwa sasa akiwa na wimbo mpya wa Msambinungwa, yuko chini ya usimamizia wa Tiptop Connection kwa muda mrefu sasa.

No comments:

Post a Comment