UA-45153891-1

Sunday, February 9, 2014

PIKIPIKI YA PAPA FRANCIS YAUZWA $327,000


Pikipiki aina ya 'Dyna Super Glide' toleo la mwaka 2013 yenye 1,585cc ambayo Papa Francis alipewa na Willie Davidson, mstaafu wa kampuni ya 'Harley-Davidson motorcycle' imeuzwa kwa mnada kwa bei ya dola za kimarekani 327,000 na kiasi hicho cha fedha kuelekezwa katika jiko la supu na hostel ya watu wasiokuwa na makazi ndani ya Roma.

Pikipiki ya Papa Francis ikiwa eneo la mauzo jijini Paris

Swali lililovuta watu kutaka kufahamu zaidi ni kama kiongozi huyo mkubwa wa Kanisa Katoliki alikuwa tayari amepanda pikipiki hiyo kabla ya yeye mwenyewe kufikia maamuzi hayo ya kuipiga mnada. Aliyempa pikipiki hiyo ni mjukuu wa waanzilishi wa 'Harley-Davidson motorcycle', kampuni iliyotengeneza pikipiki hiyo.

No comments:

Post a Comment