UA-45153891-1

Thursday, February 13, 2014

SHILOLE AWATAKA WASANII WA KIKE KUWA NA WIVU WA MAENDELEO


Mwanamuziki wa Bongo Flava na muigizaji wa Bongo Movie Zuwena Mohammed 'Shilole', amewataka wasanii wenzake wa kike kushirikiana badala ya kuoneana wivu mbaya unaosababisha mwingine kufikilia kumshusha aliye juu badala ya kupambana ili apande juu pia na ikibidi kuwa juu zaidi. Akijibu hoja juu ya kutoelewana na msanii mwingine wa kike Baby Madaha kupitia East African Radio jana, Shilole amesema hana ugomvi wowote na msanii huyo na kuongeza kwamba kama anataka kurekodi nae wimbo amwambie wafanye kazi pamoja.

No comments:

Post a Comment