UA-45153891-1

Monday, February 10, 2014

TAZAMA HII “RIHANNA KUOLEWA NA DON JAZZY, HARUSI YA KIASILI KUFANYIKA”


"Rihanna kuolewa na Don Jazzy, harusi ya kiasili kufanyika"

Ni kichwa cha habari kinachotawala kwenye mitandao ya kijamii nchini Nigeria, Ni baada ya shabiki mmoja wa mtayarishaji wa muziki, muimbaji na mwandishi wa nyimbo wa nchini humo Michael Collins Ajereh  'Don Jazzy' kutengeneza picha ambayo inaonyesha mwanamuziki huyo akiwa na staa wa kike wa nchini Marekani Rihanna katika mavazi ya utamaduni wa Nigeria.

Don Jazzy alipoiona picha hiyo aliipenda na kuiweka kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram, ndipo wanamitandao walipoanza kutangaza harusi ya wawili hao. Bila shaka ni miongoni mwa picha zilizotengenezwa na 'Photoshop' kwa ubunifu na  kuleta mawazo na hisia tofauti kwa watazamaji.

No comments:

Post a Comment