UA-45153891-1

Sunday, February 9, 2014

WEMA NA JOKATE INALIPA KUELEWANA

Wema Sepetu, Jokate Mwegelo na Lisa Jensen siku ya tukio la Miss Tanzania 2006

Gazeti moja maarufu hapa nchini linaloitwa 'Risasi' limeandika juu ya uhusiano mzuri uliopo kati ya warembo wawili Wema Sepetu na Jokate ambao hapo awali walilipotiwa kutopikika chungu kimoja kwa kile kinachodaiwa kuwa sababu ni wote kuwa na uhusiano na mwanamuziki 'Diamond Platnumz'. Kwa mujibu wa chanzo hicho cha habari, wawili hao walikutana kwenye ukumbi wa Triple A jijini Arusha ambapo Wema alikuwa akimtambulisha msanii kutoka Lebo yake ya 'Endless Fame Production'  anayeitwa Miraji Hussein 'Mirror'. Jokate alifika kiwanjani hapo kimyakimya kwa kufanya kile kinachoitwa 'Surprise'. "Jokate akionekana mwenye furaha alipanda jukwaani na kuomba kuzungumza machache ambapo alimkumbatia Wema kwa furaha huku akionekana hana kinyongo". Kiliandika chanzo hicho cha habari.


Wema na Jokate walishiriki Miss Tanzania 2006 ambapo Wema ndiye alitwaa taji hilo, Jokate akawa mshindi wa pili na nafasi ya tatu ikishikwa na Lisa Jensen. Hivyo inalipa kwa wawili hao kuelewana na kuwa pamoja kwa faida yao. Hata kama pengine sababu ya kila mmoja kuwa mbali na mwenzake siyo  hiyo inayoandikwa sana na vyombo vya habari, lazima kuna jambo lililokuwa kati yenu wanadada. Songa mbele, fanya kazi, mna vipaji, mnaweza sana, hayo mengine ni sehemu ya maisha tu. For the love of the creative industry.

No comments:

Post a Comment