UA-45153891-1

Wednesday, February 26, 2014

UNGEKUWA 2FACE IDIBIA UNGEJISIKIAJE KWA HILI?


Kweli unapokuwa mtu maarufu jiandae kwa lolote litakalokutokea kuanzia kwenye jamii mpaka vyombo vya habari, hasa mitandao ya kijamii. Jibu la swali hili linaweza kuwa "Vibaya!!!", ingawa naamini kwa  Staa yeyote, jibu linatakiwa kuwa  "Kawaida!!!". Na inabidi litolewe kwa kumaanisha, sio tu kwa sababu linatakiwa kuwa hivyo.

Siku chache zilizopita msanii huyu maarufu nchini Nigeria na Afrika nzima alikumbwa na skendo  ya kwamba amempa uja uzito mfanyakazi wa Benki moja nchini humo na yuko katika mpango wa kutoa  kila kinachoweza kutolewa kwa mwanadada huyo ili afanye kila kinachoweza kufanyika  kutoa ujauzito huo. Yeye alikanusha baada ya taarifa hizo kuandikwa na mtandao mmoja nchini humo.

Jana mwanamuziki huyo ametoa salamu kama ilivyo kawaida yake kwa mashabiki na wafuasi wake kwenye ukurasa wake wa Facebook, kwa kusema "My people, how una dey today?". Tazama alichoandika mmoja wa mashabiki wake mtandaoni.




No comments:

Post a Comment