UA-45153891-1

Thursday, February 20, 2014

NAPE NNAUYE ASHUKA MASHAIRI REDIONI, AMKUBALI MWANA FA, JAYDEE, BANANA, LINAH NA BARNABA


Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Nape Nnauye alisikika jana Redioni akiimba. Ni baada ya kuulizwa ni kitu gani anapenda kufanya mbali na kazi zake ambapo alisema yeye anapenda muziki na anaweza kuimba na kupiga vyombo vya muziki ikiwa pamoja na Kinanda, Gitaa na Drums. Nape ambaye alisema ana vyombo vya muziki nyumbani kwake ambavyo huvitumia kupiga na kufurahia muziki, aliendelea kusema alipata uzoefu wa fani hiyo siku za nyuma akiwa pamoja na 'Captain' Komba kwenye shughuri hizo za kimuziki.
Alipoulizwa kuhusu wasanii wa Tanzania ambao anawakubali zaidi alimtaja Mwana FA, Banana Zoro, Barnaba, Linah na Lady Jaydee.  Pia aliulizwa na watangazaji wa East African Radio juu ya nyimbo anazopenda na kuutaja wimbo wa 'Husiende mbali' ulioimbwa na Juliana Kanyomozi kwa kushirikiana na  Bushoke.

Pia alitoa maoni yake juu ya muziki wa kizazi kipya 'Bongo Flava' ambapo alisema kwa kiasi kikubwa anafurahia zaidi midundo kwa kuwa mashairi ya waimbaji wengi bado hayajawa na uzito, nyimbo nyingi zinazungumzia mapenzi ya utoto badala ya mapenzi ya kikubwa au wanandoa.Alisema sababu inaweza kuwa kwamba wengi wanaofanya muziki huo ni wa umri wa chini. Ametoa ushauri kwa wanamuziki wa Bongo Flava kutumia muda wa kutosha kujiandaa badala ya kuwa na pupa ya mafanikio ya haraka au 'kutoka' kama alivyolitumia neno hilo maarufu kwa vijana Pamoja na yote alizungumzia mipango ya serikari ya kutetea haki za wasanii.

No comments:

Post a Comment