UA-45153891-1

Friday, February 14, 2014

WEMA SEPETU AANZA KUYAISHI MAISHA YA NDOTO ZAKE



Muigizaji maarufu wa kike nchini Tanzania na mwanamitindo ambaye alikuwa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu amesema maisha anayoyaishi kwa sasa akiwa na Diamond Platnumz, ni maisha ya ndoto zake ambayo alikuwa akiyaota muda mrefu. 
Wema amesikika kupitia 'Valentine Special' ya Clouds FM akihojiwa na Zamaradi Mketema juu ya siku ya 'Valentine' ambapo amesema siku hiyo kwake ni kama siku zingine tu kwa kuwa siku zote kila mmoja anapaswa kumuonyesha upendo ampendaye na yeye ni kawaida yake kufanya hivyo. "Nampenda na nitaendelea kumpenda mpaka mwisho wa maisha yangu", Alisema Wema Sepetu alipoulizwa kuhusu Diamond.

No comments:

Post a Comment