UA-45153891-1

Thursday, February 13, 2014

JANUARY MAKAMBA NDANI YA KONGAMANO LA MFUMO WA DIGITALI ARUSHA



Ikiwa leo ni siku ya Redio duniani ambayo imeangukia katika siku nne za kongamano la masuala ya habari kwa kutumia mfumo wa Digitali linaloendelea jijini Arusha, Mbunge wa jimbo la Bumbuli na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mhe. January Makamba ameandika kwenye akaunti yake ya mtandao wa Twitter akiwa kwenye Kongamano hilo kwamba ni wakati wake kuzungumza.

Kongamano hilo la jumuiya ya nchi za Commonwealth linaitwa 'Digital Broadcasting Switchover'(#DBS2014) lililoanza Februari 11,2014 na litakalomalizika Februari 14, 2014 linazungumzia masuala mbalimbali ya mawasiliano ikiwa pamoja na changamoto zinazojitokeza katika kuhama kutoka mfumo wa Redio na Televisheni wa Analojia kwenda wa Digitali.

No comments:

Post a Comment