"Thamani ya sanaa ni kick?". Anauliza Nick wa pili. Ni baada ya kupigiwa sana simu na wasanii wengi ambao bado hawajafahamika kwenye 'industry' ya muziki wakimuomba kuonana nae ili awaunganishe watu wa vyombo vya habari ikiwa pamoja na watangazaji wa Redio na Televisheni ili wasukume kazi zao mbele kwa kuzipa kile kinachofahamika kama 'Airtime'.Pia wengine wamekuwa wakimuomba ashirikiane nao katika nyimbo zao au kwa lugha iliyozoeleka kufanya nao 'Kolabo. Akisoma walaka huo kupitia East African Radio jana, msomaji aliendelea kushuka kwamba wapo wanaoomba pesa ya kurekodi wakati ndo kwanza wameandika wimbo mmoja.
Nick wa pili anawashauri wasanii wasitafute umaarufu wa haraka kwa kutumia njia hizo ambazo kwa pamoja aliziita "kutafuta kick" kwa umaarufu huo utakuwa wa muda tu na hautawasaidia baadae katika kazi zao badala yake watumie muda huo kuboresha kazi zao ambazo zitawatangaza zenyewe kama zitakuwa nzuri."Mimi kabla sijarekodi nilikuwa naandika nyimbo mbili kila wiki na hata pasipo kurekodi lakini ndiyo ulikuwa mwanzo wa kujifunza kuandika na kurap", alisema Nick wa pili kupitia walaka wake ambao aliupa jina la 'Kalamu ya Nick wa pili'.
No comments:
Post a Comment