UA-45153891-1

Friday, January 31, 2014

KWANINI ILIKUWA LAZIMA WEMA SEPETU ARUDI KWA "DIAMOND"?


1. "Influencial Couple"
Hii hutengenezwa na watu maarufu ambao wamefanya mambo makubwa,wote wana nguvu ya ushawishi, wengi wao shughuri zao zinaendana  na wakishapendana baadhi ya mambo huyafanya kwa pamoja. Mwenye damu ya kutamani kuwa na  uhusiano wa namna hiyo hata akutane na kigogo mwenye pesa kiasi gani, kama si yule atakayesababisha kilichotajwa hapo juu, atakaa nae lakini hatatulia. Mfano wa watu hao kwa sasa duniani ni Jay-Z na Beyonce. Wema anapenda uhusiano wa namna hiyo.

2."Inspirational Couple"
Haitofautiani sana na ya kwanza ingawa hapa pia mmoja anaweza kuwa maarufu na mwingine kawaida lakini wakiungana uhusiano wao hutokea kupendwa na kukubalika sana na watu wengine. Utaona jinsi gani mashabiki wengi wa Wema sepetu ni mashabiki wa Diamond Platnumz pia. Jinsi  gani wanavyozungumziwa hata wanapokuwa hawako pamoja.Unajua kwamba kuna watu watatoa chozi ikitokea Obama na Michelle wakaachana?, huo ni mfano wa uhusiano wa namna hii kimataifa.

3."Opportunistic to inspirational Couple"
Hapa mmoja hutumia fursa ya kujifunza au kupata mafanikio zaidi sambamba na uhusiano mzuri ambao pia unaweza kuwa imara na wa kweli. Wema Sepetu alianza uhusiano na watu kama Diamond Platnumz tangu alipoanza kupata nafasi ya kuonana nao alipokuwa miss Tanzania. Fani yake ya uigizaji ilianzia kwa "The late, the great" Steven Kanumba. Mpaka sasa anafanya mambo mengi nyuma ya pazia ikiwa pamoja na muziki.

Unamfahamu Kim Kiyosaki?. Alipokutana na muelimishaji maarufu wa ujasiliamali duniani na mwandishi wa vitabu Robert Kiyosaki kabla hajawa mume wake, Kim Kiyosaki alikuwa ndo ameanzisha jarida lake. Kupitia Robert, Kim alijifunza mbinu nyingi za biashara na kuanzisha kampuni ya viwanja na majengo "Real estate". Kilichofuata baada ya hapo, aliungana na Robert Kiyosaki katika shughuri za kutoa semina za ujasiliamali. Wakiwa tayari ni mke na mume, Robert Kiyosaki aliandika kitabu kinachoitwa "Rich Dad Poor Dad". Kim nae akatoka na "Rich mom".Hivyo utaona jinsi gani mbali na uhusiano, Kim alihamasika na kujifunza kutoka kwa Robert.

Kimtazamo, Wema Sepetu anadondokea kwenye makundi yaliyotajwa hapo juu. Hivyo ilikuwa lazima arudi kwa "Diamond" wa muziki,Diamond wa filamu n.k, ingawa pesa anaipenda pia. Neno Diamond limetumika badala ya mtu maarufu na "Diamond Platnumz" kama jina.


Thursday, January 30, 2014

OPRAH WINFREY ATIMIZA MIAKA 60 LEO JANUARI 29, SEMA HAPPYBIRTHDAY KWA MAMA HUYU



Ni muigizaji, mjasiliamali, mtayarishaji wa vipindi vya Televisheni, mdau wa masuala ya kijamii kama kusaidia watoto yatima, kinamama na makundi mengine maalum. Anafahamika zaidi kama  muongozaji wa kipindi cha "Talk show" anayewapa hamasa wanawake wengi katika pande zote za dunia.

Japo historia yake ina mambo mengi sana lakini aliendelea kusonga mbele na bado yuko mbioni kuyatimiza yake aliyokuja kuyatendea haki ndani ya ulimwengu huu. 
"I’m alive. Healthy. Strong. I’m turning 60," Anasema mama huyo. "And – please don’t take offense – I no longer have to be concerned about what anyone thinks of me! I’m turning 60, and I’ve earned the right to be just as I am. I’m more secure in being myself than I’ve ever been."

Ndivyo alivyofunguka Oprah. HAPPYBIRTHDAY KWAKE na wote waliozaliwa siku kama ya leo.

Tuesday, January 28, 2014

VAZI LA KATY PERRY SIKU MOJA BAADA YA TUZO ZA GRAMMY NCHINI MAREKANI

Ni siku iliyofuata baada ya tuzo za Grammy ambayo ni maarufu kama "Grammy Salute"

'HAPPYBIRTHDAY' KWA MH. JANUARY MAKAMBA NA RICK ROSS


 Mheshimiwa January Makamba

Leo Januari 28, ni siku ya kuzaliwa ya mheshimiwa January Makamba, mbunge wa Bunbuli na Naibu Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Mawasiliano. Siku hii ndiyo pia aliyozaliwa mwanamuziki na CEO wa 'Maybach Muzic' wa nchini Marekani Rick Ross.

 Rick Ross

WATOTO WA PETER WA P-SQUARE "CAMERON OKOYE" NA "ALIONA OKOYE"

Cameron
Aliona akiwa na wazazi wake

KAMPUNI YA ZOOM YAWASHIKA WAMAREKANI KWA MICROPHONE ZA iQ5


Ikiwa ni miezi mitatu tangu kuzinduliwa kwa microphone zinazopachikwa nje ya simu ambazo zimetengenezwa na kampuni ya Zoom ya Japan, zimeripotiwa kununuliwa kwa wingi sana nchini Marekani. Microphone hizo ambazo zinaitwa iQ5,  zimetengenezwa kwa ajili ya iPhone, iPad na iPod touch. Zinapachikwa na kurekodi kwa kiwango cha hali ya juu sana.

MAMBO SITA YA KUFANYA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII KABLA HUJAPATA KIFUNGUA KINYWA

Kama wewe ni mdau wa mitandao ya kijamii, kwa matumizi binafsi au kiofisi, bila shaka utakuwa unatumia mtandao mmoja wapo kati ya Facebook, twitter, LinkedIn, Google+ au yote hii iliyotajwa. Lazima pia una email ambayo kutumia mitandao ya kijamii haikwepeki. Sasa soma anachokwambia huyu mdau wa matumizi ya  haya mambo.......

Monday, January 27, 2014

MZEE DUDE WA FUTUHI AFARIKI DUNIA


Msanii wa kundi la maigizo na vichekesho  la Futuhi, Mzee Dude amefariki dunia akiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando iliyopo jijini Mwanza. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amen!

KELLY ROWLAND KUTUA NCHINI NIGERIA BAADA YA SIKU YA 'VELENTINE'

 Star na mmoja  wa waliounda kundi la Destiny's child Kelly Rowland atakuwa live Lagos Nigeria tarehe 15 Februari kwenye tamasha la mitindo. Wanamuziki na watu wengine mashuhuri katika sanaa wamekuwa wakipata mialiko mbalimbali nchini humo kwa ajili ya shughuri za maonyesho ya mitindo na matamasha mengine ya burudani. Kim Kardashian alikuwa huko mwaka jana kwa ajili ya shughuri kama hiyo.

ANNA PETER AFANYA KAMA ALIVYOAHIDI KUFANYA SIKU YAKE YA KUZALIWA



"Tarehe 27 January nitakuwa nasherehekea siku yangu ya kuzaliwa. Mwaka huu nimeamua nitumie sauti yangu ambayo Mungu amenibariki kushare na Wasichana na wanawake wenzangu kokote pale duniani ujumbe huu 'Tunaweza' ambao wimbo wake utatoka rasmi siku hiyo tarehe 27". Ndivyo alivyoandika siku chache zilizopita kupitia Blog yake ya annapita.com.

Siku yake ya kuzaliwa ambayo ni leo Januari 27, 2014, mtangazaji huyo wa East African Radio kupitia kipindi cha PowerJams ametoa wimbo wake aliomshirikisha Hellen  ambao unaitwa "Tunaweza"  uliowekwa mkono na Mtayarishaji Mr. T Touch wa Studio ya Seductive Records. Kama wewe ni mwanadada au mama, wimbo huu unakuhusu lakini pia kaka na baba mwambie dada na mama kuhusu wimbo huu ili wapate kuhamasika. HAPPYBIRHDAY ANNA PETER.

 Soma mashairi

WALIOSHINDA TUZO ZA GRAMMY 2014

Mwandishi wa nyimbo Joel Little na mwimbaji Lorde ambao ni washindi wa tuzo ya wimbo bora wa mwaka Grammy 2014. Tuzo hizo zilifanyika  January 26, 2014


Wimbo bora wa mwaka
"ROYALS"-Lorde  (
Uliandikwa na Joel Little na Ella Yelich

Album bora ya R&B:
"GIRL ON FIRE"-Alicia Keys

Wimbo bora wa  R&B:
"PUSHER LOVE GIRL"-Justin Timberlake
Uliandikwa na James Fauntleroy, Jerome Harmon, Timothy Mosley na
 JustinTimberlake,

Mtayarishaji wa muziki wa mwaka (Non-Classical):
Pharrell Williams

Mtayarishaji wa muziki wa mwaka  (Classical):
David Frost

 Video bora ya muziki:
"SUIT AND TIE"-Justin Timberlake Featuring Jay Z, 
Mtayarishaji ni Timory King
Director ni Timory KingDavid Fincher

Wimbo bora wa dini:
"IF HE DID IT BEFORE . . . SAME GOD"- Tye Tribbett  

 Kufahamu washindi wote, soma zaidi...

BABY MADAHA AENDELEA KUTENGENEZA 'HEADLINE' NCHINI KENYA


"Sexy Tanzanian Singer Admits Top Kenyan Record Producer is ‘More Than a Manager to Her". Ndivyo ulivyoandika mtandao maarufu nchini humo unaoitwa 'Ghafla' .

Baby Madaha akiwa na Joe

Muimbaji na muigizaji wa kike ambaye ni zao la Bongo Star Search, Baby Madaha, amekubali kwamba ana uhusiano wa kimapenzi na meneja wake ambaye pia ni mtayarishaji wake 'Producer' wa label ya Candy n Candy, Joe Kariuki. Ni baada ya siku chache zilizopita kuandikwa na mitandao mbalimbali ya Tanzania juu jambo hilo.

Akihojiwa na jarida la 'Spice' la nchini humo, Baby alisema, " Uhusiano wangu na Joe, mmmmh.... Joe amekuwa ni zaidi ya msimamizi wa kazi zangu. Natumia  muda wangu mwingi nikiwa na yeye, sijari watu wanasema nini. Ninafurahi na kama uhusiano wangu na Joe hauniathili kwa namna yoyote kwa nini nitazame wengine. Kama yuko 'single' kuna tatizo gani akiwa na mimi?"

Baby Madaha anafanya vizuri na wimbo wake wa 'Summer holiday' chini ya  studio za  Candy n Candy nchini Kenya.

UKO BIZE LAKINI MACHO YAKO YANAHITAJI KUONA MANDHALI TOFAUTI NA HAPO ULIPO???...TAZAMA PICHA HIZI ZA AFRIKA




Sunday, January 26, 2014

MKE WA 2FACE IDIBIA 'ANNIE' NAE ATUPIA PICHA YA WATOTO WAO


Ikiwa ni siku chache baada ya 2face Idibia kuweka mtandaoni picha ya mtoto wake mdogo anayeitwa Olivia, mke wake Annie kaweka picha ya mtoto wao mkubwa na mdogo akionekana amelala. Pia amezungumzia anachokihisi kwa mtoto huyo mkubwa kuwa ni upendo alionao kwa mdogo wake.

MILLARD AYO ASHEREHEKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA AKIWA DUBAI

Mwandishi wa habari na mtangazaji wa Clouds FM Millard Ayo anasherehekea siku yake ya kuzaliwa leo Januari 26, 2014 akiwa Dubai. Mtangazaji huyo maarufu kama 'Mr.Count down', anayesikika kupitia kipindi cha 'Amplifaya',  alizaliwa siku au tarehe kama aliyozaliwa kocha maarufu wa soka Jose Mourinho.

Staa huyo ambaye ni miongoni mwa watanzania wenye wafuasi wengi kwenye mitandao ya kijamii, amesikika redioni akizungumzia siku hii na pia ameandika kupitia mtamdao wa Instagram kwamba uwepo wake ndani ya Dubai ni zawadi kutoka kwa bosi wake Joseph Kusaga.

SIKU YA KUZALIWA (BIRTHDAY) YA ALICIA KEYS-JANUARY 25


Leo Januari 25 ni siku ya kuzaliwa ya muimbaji wa kike maarufu nchini Marekani, Alicia Keys. Mwanadada huyu star wa wimbo wa 'No one' alizaliwa siku moja au ana'share' birthday na watu wengine mashuhuri akiwemo  mchezaji wa soka Xavi na muigizaji Jenifer Lewis.

Saturday, January 25, 2014

HUYO NDIYE LADY GAGA!!!! ANATEMBEA KAMA ANAPAA...!

Ndivyo alivyokutwa Paris kwenye wiki ya maonyesho ya sanaa ya mitindo.

KUHUSU VIDEO YA "TEMA MATE TUWACHAPE", MADEE NA BARAZA LA SANAA LA TAIFA (BASATA)

Kufuatia mitazamo tofauti ya kimaadili na kiutamaduni juu ya video ya muziki, ya wimbo wa "Tema mate tuwachape" ambayo ni ya msanii wa Bongo Flava maarufu kama Madee, kumekuwa na tetesi kwamba Basata wamempigia simu Madee kuzungumza nae juu ya suala la hilo.

 Madee
Hata hivyo msanii huyo amesema kupitia Planet Bongo ya East African Radio kwamba baada ya kupigiwa simu alizungumza na msimamizi wake na kuambiwa angoje barua kwa sababu anaweza kuwa mtu binafsi kaamua tu kutumia jina la chombo hicho kuzungumza anavyotaka au kuzingua kama wanavyosema watoto wa mjini.

Hivyo video hiyo inaendelea kupeta na itazidi kupeta pasipo kujali maneno ya watu na kama kuna lolote chombo husika kitamtaarifu Madee kwa maandishi. Hii ni kwa mujibu wa maelezo aliyoyatoa staa huyo wa wimbo wa "Pombe yangu".

LOVENESS LOVE "DIVA" ASHUKURU KWA LUGHA YA KIBANTU




Mtangazaji maarufu wa kipindi cha Ala za roho cha Clouds FM ambaye inasemekana mzazi wake mmoja ana asili ya kanda ya ziwa na mwingine mkoani Tanga, aliandika kupitia mtandao wa Twitter ambapo ni kama alikuwa akimjibu shabiki wake aliyesomeka jina Gregory juu ya lugha hasiyoielewa na ambayo hategemei kujaribu kujifunza. Hata hivyo mwishoni alimalizia kwa kuandika maneno ya lugha hiyohiyo ambayo ni moja ya lugha za kibantu zinazotumika hapa nchini Tanzania.

 Maneno aliyoyaandika ni kwa ajili ya kushukuru, yaani "ahsante sana". Neno "Ahsante" kwa lugha hiyo limekuwa likitumiwa sana na mchekeshaji wa kundi la 'Original Comedy' Mjuni Silvery 'Mpoki' kupitia kipindi cha Televisheni. 

Friday, January 24, 2014

FAHAMU JINA LA AINA YA NDEGE ANAYOTUMIA MSAANII 'JAGUAR'

 Jaguar

Ni kawaida sana watu kutaka kujua mtu flani maarufu anatumia usafiri gani kama ni 'mkoko' ni gari gani na aina gani, mfano Mercedes benz SL300, Toyota Altezza AS200, Audi TT na nyinginezo.Lakini tunapokuja katika suala la ndege, hapo wengi huishia kusema ndege.Hata hivyo inatosha kutokana na hadhi ya chombo hicho japo baadhi hupenda kufahamu zaidi.

Ndege ya Jaguar aina ya Cessna

Ndege anayotumia msanii Jaguar wa nchini Kenya ni aina ya Cessna. Japo haijajulikana ni Cessna toleo gani maana kuna Cessna 205, 206, 207, 310 na zingine lakini ni aina ya ndege iliyotengenezwa na Kampuni ya Cessna ambapo toleo la kwanza lilitoka mwaka 1962 na mpaka kufikia mwaka 2006 zilikuwa tayari zimetengenezwa ndege 8509 za aina hiyo. Ni aina ya ndege inayotumika kibiashara na safari binafsi. Bei ya ndege hizo ni kati ya dola za kimarekani laki tisa ($900,000) mpaka milioni 26 ($26,000,000).

Jaguar anaitumia ndege yake kibiashara na si kwa matumizi binafsi.

MASHABIKI WA JUSTIN BIEBER WAANZA KUPOTEZA IMANI NAE


Ni baada ya kukamatwa na polisi kwa tukio lililomtia hatiani kwa makosa ya kuendesha gari akiwa amelewa pombe, matumizi ya madawa ya kulevya, leseni iliyoisha muda wake na  kuendesha  mwendo wa  kasi kwa shinikizo. Alikamatwa pamoja na muimbaji aliyejulikana kama Khalil Amir Sharieff baada ya askali kuwaona wakiendesha magari flani ya bei mbaya katika hali ya mashindano.

Justin Bieber akipigwa pingu

Justin Bieber mwenye umri wa miaka 19 ambaye ana ushawishi mkubwa kwa vijana wadogo kupitia sanaa ya muziki na  mwanamuziki anayefuatwa zaidi na watu wengi kwenye mitandao ya kijamii, mashabiki wake wametoa maoni yao kupitia mitandao hiyo ambapo wengi hawajafurahishwa na matukio hayo na kusema anapoteza muelekeo. Baadhi yao wanashauri apate muongozo mzuri  ili hasipotee zaidi.

BABA MZAZI WA MARY J. BLIGE AUMIZWA NA MPENZI WAKE WA ZAMANI


Baba yake na mwimbaji mashuhuri wa RNB, Mary J. Blige, ameripotiwa kuwa yuko katika hali mbaya baada ya kuumizwa shingo kwa kuchomwa kisu na 'X-girlfriend' wake katika ugonvi wa nyumbani. Taarifa zinasema tatizo limeanza baada ya baba  huyo anayeitwa Thomas Blige mwenye umri wa miaka 63 kumshambulia mpenzi wake kwa maneno kwamba ametoboa magurudumu ya gari lake.
Mary J. Blige

Mwanamke aliyefanya tukio hilo lililotokea majira ya asubui Alhamisi ya January 23, 2014 anashikiliwa na Polisi. Thomas Brige ambaye kwa sasa amelazwa hospitali, inasemekana zamani alikuwa mwanamuziki wa Jazz na ni veterani wa jeshi. Aliondoka na kumuaacha Mary J.Blige akiwa na miaka minne.

Inasemekana ndiyo maana katika wimbo wa Mary J. Blige unaoitwa 'Father in you', mwanadada Mary alishuka mistari "When I was a little girl / I didnt have a father / And that's why I'm learning on you/".

KIM KARDASHIAN NA KANYE WEST WAKANUSHA JUU YA TAARIFA KWAMBA WATAFUNGA NDOA PARIS

Mwanamuziki Kanye West na mchumba wake mwanamitindo ambaye pia ni muimbaji Kim Kardashian, wako ndani ya jijini linalosemekana kuwa la starehe kushinda yote barani Ulaya Paris kwa ajili ya wiki ya mitindo, japo taarifa kutoka kwa watu na vyanzo mbalimbali vya habari zimekuwa zikiripoti kwamba watafunga ndoa huko. 

Hata hivyo wamesema kwamba wamejaribu kuangalia sehemu mbalimbali zinazoweza kufaa kwa ajili ya harusi yao kama vile hotel kali zinazosumbua pande hizo. Waliipenda sana 'Palace of Versailles' lakini bado hawajaamua kufanyia harusi yao huko.

STEVE NYERERE, LULU NA EVANCE WAZUNGUMZIA TASNIA YA FILAMU

Ni ndani ya kipindi cha Mboni Show kilichoruka Alhamisi ya tarehe 23 January 2014 kuanzia saa tatu usiku chini ya mwanadada Mboni Masimba. Hii ni picha ya pamoja.

Thursday, January 23, 2014

KUWA 'SUPERSTAR' YATAKA MOYO, SOMA KILICHOMKUTA CPWAA...!

Semadat Blog imekutana  na 'post' yake Fb ikiwa haijamaliza hata dakika moja. Hebu ruka nayo:

D'BANJ ATAMBULIWA RASMI NA MTANDAO WA FACEBOOK (VERIFIED)

'Facebook page' ya  D'Banj ndivyo inavyoonekana

Ukurasa wa Facebook wa mwanamuziki maarufu wa Nigeria D'Banj 'Kokomaster', staa wa Oliver twist, imehakikiwa na kuthibitishwa na mtandao huo kwa kuwekewa alama ya 'tick' ya rangi ya Bluu, hivyo kuitofautisha na zile zilizofunguluwa kienyeji na watu wangine kwa kutumia jina lake.

D'Banj anakuwa mtu wa pili nchini humo ambapo kabla ya hapo aliyekuwa na ukurasa wa Facebook katika hali hiyo ya kutambuliwa ni Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan peke yake.

Tofauti na kwenye mtandao wa Twitter ambao watu wengi maarufu nchini humo wana alama hiyo, kwa upande wa Facebook si kitu rahisi na kwa hapa nchini Tanzania hakuna aliyewekewa alama hiyo kwenye Facebook japo upande wa Twitter wapo kama Rais Kikwete,  AY, January Makamba, Flaviana Matata na Hasheem Thabeet.

DIAMOND KUDONDOKA JIJINI NAIROBI KWA AJILI YA PARTY


"After shutting down Nairobi in August last year, Bongo’s prince Diamond Platnumz is coming  back to the country!". Mdivyo ulivyoandika mtandao unaoitwa 'Ghafra' wa nchini Kenya. Diamond yuko nchini humo siyo kwa sababu za kibiashara bali kwa ajili ya 'Party' ambayo haikujulikana inahusu nini. Pia mtandao huo umempa shavu kubwa Diamond kwamba ni msanii mkubwa  na msanii pekee kutoka Afrika Mashariki ambaye alialikwa kwenye harusi ya Peter wa P-Square nchini Nigeria.

Pia Diamond mwenyewe alizungumzia safari hiyo kwenye mitandao ya kijamii na kuweka picha inayomuonesha akiwa maeneo ya uwanja wa ndege kama inavyoonekana hapo juu.


BIRTHDAY YA KWANZA YA MTOTO WA PETER WA P-SQUARE 'ALIONA OKOYE'


Aliona ametimiza mwaka mmoja. Wazazi wake Peter na Lola pamoja  na 'uncle' wake Paul, wameshiriki kumpongeza wakiwa katika makazi yao mapya Atlanta Marekani. Mtoto huyo ni  'photocopy' ya Peter na rangi ya mama yake.

'MAMA LULU' NA 'MAMA KANUMBA' KUTUA BUKOBA

  
Mastaa wanawake ambao umaarufu wao na urafiki wao ulitokana na matatizo, wanaendelea kuuonesha umma kwamba yaliyotokea tayari yametokea na hakuna aliyependa yatokee, kikubwa ni kumshukuru Mungu kwa kila jambo na kuhimarisha upendo. Ni baada ya kulipotiwa hivi punde na mtandao maarufu wa Global Publishers kwamba wanaandaa safari ya kwenda Bukoba mkoani Kagera wanakotokea, ili kula kiapo cha kuimarisha undugu. Safari ya Lucresia Karugila ‘Mama Lulu’ na  Flora Mtegoa ‘Mama Kanumba’ inalenga pia kumuhudumia mama mzazi wa Flora Mtegoa yaani bibi yake marehemu Steven Kanumba, ambaye ni mgonjwa kwa sasa.

GENEVIEVE NNAJI AWA BALOZI WA KAMPUNI YA ETISALAT

Genevieve Nnaji

Muigizaji mashuhuri wa kike nchini Nigeria na Afrika kwa ujumla Genevieve Nnaji amechaguliwa kuwa Balozi wa Kampuni ya Simu ya Etisalat kupitia huduma ya Easy Flex. Shughuri fupi ya kumkaribisha kufanya kazi hiyo imefanyika leo katika hoteli ya Wheat baker nchini humo. Anaungana na staa mwingine Hakeem Kae-Kazim ambaye pia ni Balozi wa Kampuni hiyo. Kampuni hiyo iko kwenye kampeini kabambe ya huduma hiyo.

Wednesday, January 22, 2014

NANCY SUMARI NA "NYOTA YAKO", FARAJA NYALANDU NA "UNAWEZA" NI MFANO WA KUIGWA

Warembo hawa wameshatoa vitabu na wanaendelea kuandika vingine. Nancy Sumari ambaye alikuwa Miss Tanzania 2005 alizindua kitabu cha watoto kinachoitwa 'NYOTA YAKO' mwaka 2013.

 Leo tarehe 22 Januari 2014, Faraja Nyalandu nae amezindua kitabu chake kwa ajili ya  wanafunzi kinachoitwa 'UNAWEZA' ambacho kinatoa mbinu kumi za mwanafunzi kumudu masomo.

Faraja Kotta Nyalandu akizindua  kitabu chake kinachoitwa  'Unaweza' Januari 22, 2014
 Faraja akiwa na Nancy wakati wa uzinduzi wa kitabu chake
Nancy Sumari alipokuwa akizindua  kitabu chake kinachoitwa  'Nyota yako' Machi 2013

MWAFRIKA MWEUSI WA KWANZA KUTEMBEA NJE YA SAYARI YA DUNIA

Mandla Maseko

Anaitwa Mandla Maseko.Ni Dj wa mtaani,nchini Afrika Kusini, mwenye umri wa miaka 25, akitokea wilaya ya Mabopane jirani na jiji la Pretorea.Ni baada ya kushinda mashindano yaliyoandaliwa na wanataaluma wa anga wa nchini Marekani.Amewashinda washiriki zaidi ya milioni moja kutoka nchi 75 na kuwa mmoja wa watu 23 watakaotembelea mwezini.

Alikuwa mwanafunzi wa Uandisi wa Ujenzi (Civil Engineering) ambaye alisitisha masomo baada ya kushindwa kulipa ada.Bado anaishi na wazazi wake na ndugu zake wanne ambapo katika familia yake hakuna hata mmoja ambaye alishatoka nje ya Afrika Kusini. Katika hali ya kawaida inasemekana  kutembelea huko ni gharama zisizopungua dola za kimarekani 100,000.

Tuesday, January 21, 2014

RAIS OBAMA ALIPOSEMA BANGI HAINA MADHARA MAKUBWA ZAIDI YA POMBE


Akinukuliwa na gazeti la New Yorker linalotoka Jumapili,alipofanyiwa usaili kuhusiana na mjadala wa uhalalishaji wa Bangi katika maeneo ya Washington na Colorado,  Rais Obama alisema "Nilishavuta nikiwa mdogo na ipo kwenye historia. Hii ni tabia mbaya kama ambavyo pia nilivuta sigara. "Ila sizani kama ni hatari kuliko pombe". 

"Si hatari zaidi ya pombe?", aliulizwa Rais Obama. Hata hivyo alielezea anachokimaanisha kuwa si kwamba anaunga mkono matumizi yake bali hafurahishwi na masuala ya sheria  inayowatolea macho na kuwafunga kwa muda mrefu watoto wa masikini kutokana na mazingira ambayo yanawafanya waonekane, wakati watoto wa familia za maisha ya kati na wa matajiri wakitumia na kuendelea kupeta.