UA-45153891-1

Thursday, January 23, 2014

'MAMA LULU' NA 'MAMA KANUMBA' KUTUA BUKOBA

  
Mastaa wanawake ambao umaarufu wao na urafiki wao ulitokana na matatizo, wanaendelea kuuonesha umma kwamba yaliyotokea tayari yametokea na hakuna aliyependa yatokee, kikubwa ni kumshukuru Mungu kwa kila jambo na kuhimarisha upendo. Ni baada ya kulipotiwa hivi punde na mtandao maarufu wa Global Publishers kwamba wanaandaa safari ya kwenda Bukoba mkoani Kagera wanakotokea, ili kula kiapo cha kuimarisha undugu. Safari ya Lucresia Karugila ‘Mama Lulu’ na  Flora Mtegoa ‘Mama Kanumba’ inalenga pia kumuhudumia mama mzazi wa Flora Mtegoa yaani bibi yake marehemu Steven Kanumba, ambaye ni mgonjwa kwa sasa.

1 comment:

  1. Inapendeza hiyo badala ya kuendeleza chuki wao wamekuwa na umoja wabarikiwe sana.

    ReplyDelete