UA-45153891-1

Friday, January 31, 2014

KWANINI ILIKUWA LAZIMA WEMA SEPETU ARUDI KWA "DIAMOND"?


1. "Influencial Couple"
Hii hutengenezwa na watu maarufu ambao wamefanya mambo makubwa,wote wana nguvu ya ushawishi, wengi wao shughuri zao zinaendana  na wakishapendana baadhi ya mambo huyafanya kwa pamoja. Mwenye damu ya kutamani kuwa na  uhusiano wa namna hiyo hata akutane na kigogo mwenye pesa kiasi gani, kama si yule atakayesababisha kilichotajwa hapo juu, atakaa nae lakini hatatulia. Mfano wa watu hao kwa sasa duniani ni Jay-Z na Beyonce. Wema anapenda uhusiano wa namna hiyo.

2."Inspirational Couple"
Haitofautiani sana na ya kwanza ingawa hapa pia mmoja anaweza kuwa maarufu na mwingine kawaida lakini wakiungana uhusiano wao hutokea kupendwa na kukubalika sana na watu wengine. Utaona jinsi gani mashabiki wengi wa Wema sepetu ni mashabiki wa Diamond Platnumz pia. Jinsi  gani wanavyozungumziwa hata wanapokuwa hawako pamoja.Unajua kwamba kuna watu watatoa chozi ikitokea Obama na Michelle wakaachana?, huo ni mfano wa uhusiano wa namna hii kimataifa.

3."Opportunistic to inspirational Couple"
Hapa mmoja hutumia fursa ya kujifunza au kupata mafanikio zaidi sambamba na uhusiano mzuri ambao pia unaweza kuwa imara na wa kweli. Wema Sepetu alianza uhusiano na watu kama Diamond Platnumz tangu alipoanza kupata nafasi ya kuonana nao alipokuwa miss Tanzania. Fani yake ya uigizaji ilianzia kwa "The late, the great" Steven Kanumba. Mpaka sasa anafanya mambo mengi nyuma ya pazia ikiwa pamoja na muziki.

Unamfahamu Kim Kiyosaki?. Alipokutana na muelimishaji maarufu wa ujasiliamali duniani na mwandishi wa vitabu Robert Kiyosaki kabla hajawa mume wake, Kim Kiyosaki alikuwa ndo ameanzisha jarida lake. Kupitia Robert, Kim alijifunza mbinu nyingi za biashara na kuanzisha kampuni ya viwanja na majengo "Real estate". Kilichofuata baada ya hapo, aliungana na Robert Kiyosaki katika shughuri za kutoa semina za ujasiliamali. Wakiwa tayari ni mke na mume, Robert Kiyosaki aliandika kitabu kinachoitwa "Rich Dad Poor Dad". Kim nae akatoka na "Rich mom".Hivyo utaona jinsi gani mbali na uhusiano, Kim alihamasika na kujifunza kutoka kwa Robert.

Kimtazamo, Wema Sepetu anadondokea kwenye makundi yaliyotajwa hapo juu. Hivyo ilikuwa lazima arudi kwa "Diamond" wa muziki,Diamond wa filamu n.k, ingawa pesa anaipenda pia. Neno Diamond limetumika badala ya mtu maarufu na "Diamond Platnumz" kama jina.


No comments:

Post a Comment