UA-45153891-1

Monday, January 13, 2014

FAHAMU MAMBO 10 JUU YA KUNDI LA MUZIKI LA MAFILIZOLO



Theo Kgosinkwe na  Nhlanhla Nciza

1 .Liliundwa na watu watatu. Theo Kgosinkwe, Nhlanhla Nciza, and Tebogo Madingoane

2. Mafikizolo  pia ni jina la album yao ya kwanza walioitoa mwaka 1997 ambayo waliipa jina  hilo kabla ya kutoa Music Revolution mwaka 1999  na Gate Crashers mwaka 2000.

3. Mwaka 2002 walitoa album inayoitwa Sibongile kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa kuwanusuru kwenye ajali ya gari iliyotokea mwaka 2001.

4. Mmoja wao anayeitwa Tebogo Madingoane alifariki dunia Februari 14, 2004 baada ya kupigwa risasi akiwa barabarani.

5. Wawili waliobaki Theo na Nhlanhla  waliendelea na kazi na kutoa album zingine mbili ambazo ziliitwa Kwela na Van Toeka Af  na kuanza kuiandaa album nyingine inayoitwa Six Mabone mwaka 2008.

6. Theo na mwanadada Nhlanhla  walitengana ambapo kila mmoja alianza kufanya muziki kama yeye.

7. Theo alifanikiwa kutoa album yake ya kwanza inayoitwa  “I am”

8. Mrembo Nhlanhla mwenye sauti ya pekee pia alifanikiwa kutoa album mbili zenye majina ya kiasili  Inguquko (Mabadiliko) na Lingcinga Zam (Mawazo yangu).

9. Mwanadada Nhlanhla alipata wakati mgumu alipompoteza mwanae kipenzi wa kike aliyeitwa Zinathi ambaye alikuwa na umri wa miaka mitano aliyefariki kwa ajali ya gari mwaka 2009.

10. Baada ya miaka miwili ya kupanda na kushuka, wawili hao waliamua kujiunga tena mwaka 2010 kumalizia albam yao ya   ‘Six Mabone’ na mpaka sasa wako pamoja wakitamba na vibao kama Khona, Happiness na vingine.

No comments:

Post a Comment