UA-45153891-1

Monday, January 20, 2014

KUTEULIWA KWA MHE. LAZARO,HAPA KUNA MCHANGO WAKO FARAJA NYALANDU


Walio wengi wanafahamu kwamba aliyekuwa Miss Tanzania mwaka 2004,enzi hizo akijulikana kama Faraja Kotta, ni mke wa aliyeteuliwa kuwa waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu ambaye alikuwa Naibu Waziri katika Wizara hiyohiyo. Kwa kuwa 'semadat' si mwandishi wa habari za siasa bali tu zile zingine za kuleta hamasa ya ubunifu kupitia vitu, watu na maisha ya watu wanaosababisha hivyo vitu, basi nizungumzie upande huu wa shilingi.

Mwaka mmoja uliopita, Faraja alipongezwa sana na vyombo vya habari, hasa mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwa ni pamoja na magazeti tanzu yaani Blogs kwa kutimiza miaka mitano ya ndoa. "Thanking God for 5 years of beatiful marriage, I am still in love, I am still happy. I am extremely grateful". Aliandika Faraja Nyalandu kwenye mtandao wake wa twitter au kwa swaga zaidi tunasema ali-tweet.

Mtafuta dondoo wa 'semadat' alitembelea akaunti za twitter za wawili hao na kukuta majibizano ya pongezi ya hapa na pale kwenye akaunti ya Mheshimiwa Nyalandu ambaye ni mtumiaji mzuri sana wa akaunti hiyo. Pongezi moja ikiwa ni kutoka kwa aliyekuwa miss Tanzania mwaka 2000 Jackline Ntuyabaliwa 'K-lynn'. "Congratulations Mh Nyalandu for the new post", alitoa pongezi K-Lynn. "Asante shem", alijibu Mheshimiwa.



 Hata hivyo, mpaka siku  ambayo utangazaji wa uteuzi huo ulifanyika inaisha, Faraja Nyalandu hakuwa ameongea chochote kupitia akaunti yake ya Twitter. Alitafutwa Facebook na Instagram bila mafanikio. Hata hivyo siyo kesi, tunatoa pongezi  kwake tukizingatia nukuu isemayo...
"Behind Every Successful Man There Is A Woman".

No comments:

Post a Comment