UA-45153891-1

Saturday, June 22, 2013

WALTER CHILAMBO NDANI-USIKU WA TUDD THOMAS


Wasanii mbalimbali wa muziki wa Bongo Flava na Hip Hop wameendelea kumuunga mkono Producer Tudd Thomas, mtayarishaji mahiri wa muziki hapa nchini Tanzania ili kunogesha tamasha la usiku wa Tudd Thomas litakalofanyika 30, 2013 ndani ya ukumbi wa Dar Live Mbagala.

Msanii Walter Chilambo ambaye alikuwa mshindi wa Bongo Star Search 2012, atafanya vitu vyake ndani ya tamasha hilo. Mwanamuziki huyo staa wa wimbo wa “Siachi” ameahidi kutoa ushirikiano mkubwa kwenye tamasha hilo na kutoa burudani ambayo itawakonga nyoyo mashabiki wake.

Walter anaungana na wasanii wengine wakali watakaokuwepo ambao ni Diamond, Chegge, Mwasiti, Marlaw, Linex, Scorpion Girls, Linah, Barnaba, Amin, Ally Nipishe, Izzo Business, Baba Levo, Godzilla, Queen Darlin, Recho, Makomando na wegine wengi, Ney wa mitego, Roma na Kala Jelemiah.

Pia watakuwepo wasanii maarufu wa filamu ambao ni pamoja na Elizabeth Michael “Lulu”, Jackline Wolper na Yusuph Mlela na Jack wa Chuz.

Friday, June 21, 2013

ELIZABETH MICHAEL “LULU” NDANI YA USIKU WA TUDD THOMAS



                             Elizabeth Michael “Lulu”  
                
Msanii wa filamu Elizabeth Michael “Lulu” atakuwa miongoni mwa wasanii maarufu wa filamu watakaoungana na wasanii wa muziki kusindikiza tamasha kabambe la usiku wa Tudd Thomas litakalofanyika Juni 30, 2013 katika  ukumbi wa Dar Live Mbagala Zakheem. Mastaa wengine wa filamu watakaokuwepo ni pamoja na Jackline Wolper, Yusuph Mlela na Jack wa Chuzi.

Tamasha hilo litakuwa ni kwa ajiri ya kuwakutanisha jukwaa moja wanamuziki, wasanii wa filamu na wa fani zingine ambao wamewahi kufanya kazi na mtayarishaji mahiri wa muziki hapa nchini Producer Tudd Thomas, pamoja na wengine wote ambao wako kwenye fani zinazohusu burudani na sanaa kwa ujumla. Kwa sasa Lulu anarekodi wimbo kwa Tudd Thomas amabao pia utakuwa sound track ya filamu yake ambayo iko jikoni.


Friday, June 14, 2013

DIAMOND AKIZUNGUMZIA MIZUKA ILIYOMFANYA AMVUTIE SIMU CHEGE ILI WAENDE KUREKODI WIMBO KWA TUDD THOMAS USIKU WA KUAMKIA MEI, 29, 2013

 

Usiku wa Jana mizuka ilinipanda sana sana kiasi kwamba nikaamua
kumvutia simu mwanangu
Chege Chigunda mtoto wa Mama Said aibuke twende studio kutengeneza
 mkono mzuri ambao ni
Idea ilikuwepo kichwani mwangu kwa muda......Tukakutana na kuamua
 kupika mahakuli
mazuri yaende saawia kwa mashabiki zangu na kwa ujumla.......
Chini ya Producer Tudd Thomas akisimamia kwa
 umakini zaidi mipango yote
Iende kikamilifu...

Zifuatazo ni picha  kadhaa nikiwa na Mwanangu wa
Nguvu Chege Chigunda....
Tukifanya mambo studio......
With Tudd Thomas


Tukiweka mambo sawa...Nini kifanyike kuleta
 radha Muziki Mzuri....

With Tudd Thomas & Chege
With Qboy Mnyama akinifahamisha kitu kiufasaha zaidi.....

Nikiwa na wasafi Photographer goes by the
name Kisula......
akisikiliza demo baada ya kumaliza kufanya
Nusu ya nyimbo hii.....

Ilikuwa mida ya alfajiri kabisa tukitoka studio tukiwa tumefanya
 nusu ya nyimbo....
si unajua vitu vizuri avihitaji haraka.....Inshallah siku nyingine
tutamalizia mahakuli
haya......
Pitia Blog Yako ya Kijanja This Is Diamond kupata
updates zote kuhusu Ent.....


Habari kutoka: www.thisisdiamond.com 

Thursday, June 13, 2013

SEMADAT

Habari wanamitandao ya kijamii!!!

DATSONGWRITER TZ Blog,  sasa inaitwa SEMADAT (semadat.blogspot.com)
Facebook page itaendelea kuitwa Dat Songwrter Tanzania na twitter itaendelea kuitwa datsongwritertz.

Nawashukuru na endeleeni kututembelea. 


R.I.P LANGA

.



Aminiel Aligaesha ambae ni Afisa Uhusiano wa hospitali ya Taifa Muhimbili amethibitisha kwamba msanii Langa amefariki dunia June 13 2013 saa kumi na moja jioni baada ya kufikishwa hospitalini hapo toka juzi jioni ambapo kutokana na sababu za kimaadili kwenye tiba, Muhimbili hospitali hawawezi kusema rapper huyu alikua anaumwa nini bali ndugu ndio wenye mamlaka ya kufanya hivyo.

Kwenye maelezo aliyoyatoa kwa millardayo.com Aminiel amesema Marehemu Langa alipokelewa kwenye idara ya wagonjwa  ya dharura usiku wa kuamkia jana na kupatiwa huduma ambapo leo June 13 2013 ndio alihamishiwa kwenye chumba cha wagonjwa Mahututi na baadae kufariki dunia.

 


  

Monday, June 10, 2013

USIKU WA TUDD THOMAS 30/06/2013

HUSIKOSE DAR LIVE SIKU HIYO

OMMY DIMPOZ, MASHUJAA BAND NA KALA JEREMIAH WANG'ARA KILIMANJARO TANZANIA MUSIC AWARDS



Usiku wa jana ulikuwa ni usiku wa furaha sana kwa Mashujaa Band ambao waliongoza kwa kuondoka na tuzo nyingi kuliko wasanii wengne. Mashujaa ambao wanafanya vizuri na wimbo wao wa ''Kidole Risasi'' waliondoka na kura 5 ikiwa ni pamoja na msanii bora wa kiume band Charz Baba, mtunzi bora a mashari ya band Charz Baba, rapper bora wa band Furguson, wimbo bora wa band Risasi Kidole na tuzo ya tano waliichukuwa kupitia category ya band bora ya mwaka huku wakiwatupa kule Twanga Pepeta, Mapacha Watatu na Msondo Ngoma


Wakati huo, upande wa hiphop, Kala Jeremiah aliondoka na tuzo tatu na kuwaacha chini akina Fid Q,Stamina na wengineo, ambapo aliondoka na tuzo ya  msanii bora wa hiphop, mtunzi bora wa mashairi ya hiphop na wimbo bora wa mwaka ''Dear God''

King Crrazy GK akitoa salam zake baaada ya kupigiwa shangwe la hatari alipopanda jukwaani kutoa tuzo ya mssanii bora wa Hiphop

 
Ommy Dimpoz nae, alisepa na tuzo tatu , wimbo bora wa kushirikiana ''me and you'', video bora ya mwaka ''Baadae'' na wimbo bora wa bongo pop
 
 
Kutoka arusha, Jambo Squad waliwakilisha vizuri baada ya kuchukua tuzo ya kundi bora la muziki wa kizazi kipya
Mrisho Mpoto ameondoka na tuzo ya wimbo bora wenye vionjo vya asili ''chocheeni kuni''
Mtayarishaji boa wa mwaka ni Man Walter
 

Ben pol aliondoka n tuzo ya mtunzi bora wa muziki bongo fleva.
Wengine ni pamoja na Diamond ambae aliondoka na  tuzo ya msanii bora wa kiume na msanii bora wa kiumee bongo fleva. msanii anaechipukia ''Ally Nipishe'', mtayarishaji anaechipukia ''Mensen Selector, wimbo bora wa hiphop ''nasema nao'' Ney wa mitego, wimbo bora wa Zouk/Rhumba ''ni wewe'' Amini, wimbo bora wa Africa mashariki ''Valu valu'' Chameleon, msanii bora wa kike ''Jay Dee,

Friday, June 7, 2013

BURUDANI MWANZO MWISHO "USIKU WA TUDD THOMAS" DAR LIVE

Ni Juni 30, 2013


USIKU WA TUDD THOMAS GUMZO TOWN



Wasanii kibao ambao wamepita kwenye mikono ya Prodyuza Tudd Thomas ndiyo wamekuwa gumzo la jiji kwa sasa kufuatia shoo kali wanayotarajia kuifanya Juni 30, mwaka huu katika ukumbi wa Dar Live, Mbagala Zakhem, Jijini Dar.

Miongoni mwa wasanii ambao wamepita kwenye mikono ya prodyuza huyo ni pamoja na Marlaw, Chege, Barnaba, Diamond, Mwasiti, Linah, Recho, Banana Zorro, Darasa, Godzillah na wengine kibao ambao wote kwa pamoja watakuwepo stejini siku hiyo.Akizungumzia maandalizi ya shoo hiyo, Tudd amesema siku hiyo itakuwa ni ya tofauti kwani wasanii wote waliowahi kufanya naye kazi wanataka kuandika historia kwa kufanya shoo nzuri hivyo itakuwa ni burudani bab’kubwa.

“Kila msanii anataka kuonesha heshima yake stejini pamoja na uwezo wa kuimba, mashabiki watashuhudia shoo kali pamoja na kusikiliza tungo nzuri za wasanii wengi ambao ni nadra kuwakuta kwenye jukwaa moja,” alisema Tudd.

MAZISHI YA NGWEA YAKAMILIKA MENEO YA KIHONDA MKOANI MOOGORO

M2TheP akimuaga mshikaji wake wa karibu, marehem Albert Mangwea, katika viwanja vya Jamhuri mkoani Morogoro
 
 Maelfu ya wakazi wa Morogoro wakiwa katika foleni kumuaga marehem Albert Mangwea
  
Dada alieanguka na kuzimia akichukuliwa na watu wa msalaba mwekundu

 

Watu waliokusanyika kumlaza Ngwea ndani ya nyumba yake ya milele


  Albert Mangwea, amefikishwa katika nyumba yake ya milele, katika makaburi ya Kihonda mkoani Morogoro, pembeni ya kaburi alilozikwa marehem baba yaje mzazi.
 
Habari kutoka:  djfetty.blogspot.com

 



 



Thursday, June 6, 2013

MAELFU YAUAGA MWILI WA ALBERT MANGWAIR JIJINI DAR ES SALAAM

Msafala kuelekea viwanja vya Leaders
Umati wa watu
Kamati  ikiongozwa na Adam Juma
JB
Bw. Hashim Lundenga
Mbunge wa Kinondoni Mh. Idd Azan
Mzee Magari
Profesa J
Linex na O.P.G
Joh Makini
Diamond
Barnaba
Ommy Dimpoz

Tuesday, June 4, 2013

MWILI WA MAREHEM NGWEA WATUA JIJINI DAR MAELFU WAJITOKEZA KUMPOKEA


Baada ya siku kadhaa za kuahirishwa kufika kwa mwili wa msanii Ngwea, hatimae leo hii Tanzania imempokea kipenzi chao, katika uwanja wa ndege saa nane za mchana. maelfu wajitokeza wakiongozwa na wasanii wenzake wa bongo fleva. Mungu ailaze roho ya marehem mahali pema peponi.
HABARI kutoka djfetty.blogspot.com



Aliewahi kuwa manager wake kwa miaka mitatu mfululizo, Tippo, akiwa uwanjani tayari kwa kumpokea Albert Mangwea