UA-45153891-1

Friday, June 21, 2013

ELIZABETH MICHAEL “LULU” NDANI YA USIKU WA TUDD THOMAS



                             Elizabeth Michael “Lulu”  
                
Msanii wa filamu Elizabeth Michael “Lulu” atakuwa miongoni mwa wasanii maarufu wa filamu watakaoungana na wasanii wa muziki kusindikiza tamasha kabambe la usiku wa Tudd Thomas litakalofanyika Juni 30, 2013 katika  ukumbi wa Dar Live Mbagala Zakheem. Mastaa wengine wa filamu watakaokuwepo ni pamoja na Jackline Wolper, Yusuph Mlela na Jack wa Chuzi.

Tamasha hilo litakuwa ni kwa ajiri ya kuwakutanisha jukwaa moja wanamuziki, wasanii wa filamu na wa fani zingine ambao wamewahi kufanya kazi na mtayarishaji mahiri wa muziki hapa nchini Producer Tudd Thomas, pamoja na wengine wote ambao wako kwenye fani zinazohusu burudani na sanaa kwa ujumla. Kwa sasa Lulu anarekodi wimbo kwa Tudd Thomas amabao pia utakuwa sound track ya filamu yake ambayo iko jikoni.


No comments:

Post a Comment