UA-45153891-1

Friday, June 7, 2013

USIKU WA TUDD THOMAS GUMZO TOWN



Wasanii kibao ambao wamepita kwenye mikono ya Prodyuza Tudd Thomas ndiyo wamekuwa gumzo la jiji kwa sasa kufuatia shoo kali wanayotarajia kuifanya Juni 30, mwaka huu katika ukumbi wa Dar Live, Mbagala Zakhem, Jijini Dar.

Miongoni mwa wasanii ambao wamepita kwenye mikono ya prodyuza huyo ni pamoja na Marlaw, Chege, Barnaba, Diamond, Mwasiti, Linah, Recho, Banana Zorro, Darasa, Godzillah na wengine kibao ambao wote kwa pamoja watakuwepo stejini siku hiyo.Akizungumzia maandalizi ya shoo hiyo, Tudd amesema siku hiyo itakuwa ni ya tofauti kwani wasanii wote waliowahi kufanya naye kazi wanataka kuandika historia kwa kufanya shoo nzuri hivyo itakuwa ni burudani bab’kubwa.

“Kila msanii anataka kuonesha heshima yake stejini pamoja na uwezo wa kuimba, mashabiki watashuhudia shoo kali pamoja na kusikiliza tungo nzuri za wasanii wengi ambao ni nadra kuwakuta kwenye jukwaa moja,” alisema Tudd.

No comments:

Post a Comment