UA-45153891-1

Thursday, December 13, 2012

KALA JEREMIAH KUTOKA NA ALBUM YAKE MPYA

 

Kala Jeremiah baada ya kufanya vizuri katika ngoma yake inayokwenda kwa jina la Dear God, aliweka wazi kwamba siku ya tarehe 20 mwezi huu anatarajia kutoka na album yake mpya inayokwenda kwa jina la Pasaka.Na hapo juu anaonyesha cover yake mpya ya hiyo album.

Monday, December 10, 2012

RAY C AMEPONA: LEO AMEPATA NAFASI YA KUMTEMBELEA RAIS JAKAYA KIKWETE IKULU JIJINI DAR


Mwanamuziki wa Bongo Fleva maarufu kama Ray C siku ya leo amemtembelea Rais Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam na kumshukuru kwa msaada wa matibabu kipindi alipokuwa mgonjwa.
Kwa upande wa mama mzazi wa Ray C amemshukuru sana Raisi Kikwete kwa kuokoa maisha ya mwanaye.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Ray C kushoto ni Mama yake mzazi Ray C Bibi Margareth Mtweve na kulia ni Sarah Mtwere Dada yake Ray C.
Habari kutoka Dj fetty blog 
 

Thursday, December 6, 2012

ALICHOKIANDIKA NONINI KUHUSU PRODUZA P FUNK MAJANI NA PICHA YA MAJANI AMBAYO NONINI AMEIWEKA KWENYE WALL YAKE


Hiyo ni picha ambayo msanii kutoka Kenya Nonini ambaye pia ni mtangazaji alitupia kwenye Wall yake asubuhi,akaambatanisha na ujumbe huuu:
"Producer na mmiliki wa Bongo Records, P.Funk 'Majani',Hakuna msani wa Bongo hajafanya kazi na P- funk pande ya hip hop….Kutoka Kina Proffesor,FidQ,Ngwea na Jaymoe Kimya Kimya....(Huyu ni Daktari Musyoka Wao)"

Monday, December 3, 2012

FID Q AMTAMBULISHA DOGO ALIYEMFUNDA KWA MIEZI 9

 
Mwanamuziki mkongwe wa Hip hop Fid Q , almaarufu kama Ngosha the Don, amesema ameamua kumchukua mwanafunzi mmoja na kumfundisha Muziki ili mwanafunzi huyo aweze kupambana na ushindani mkubwa uliopo kutoka kwa wasanii mbali mbali kwenye Muziki.

Akiongea kupitia kituo kimoja cha Radio leo jijini Dar-Es-Salaam, Fid Q alisema anaona fahari kuwa msanii anayetoa fursa kwa vijana badala ya wao (vijana) kumtegemea kwa kolabo ama pesa lakini kwa kuwafunda yeye mwenyewe wataweza kujihudumia wenyewe katika siku za baadae.

Fid Q amekuwa mfano mzuri sana wa kuigwa katika ubunifu na moyo wa kujitolea, na katika siku za hivi karibuni kupitia mahojiano tuliyoyafanya naye msanii Stamina, alionyesha kumkubali sana Fid Q, na kusema ni mtu anayemtegemgea kwenye Muziki wa Hip Hop kwa sababu anamuona kama ni nguzo na msingi wa Hip Hop hapa bongo.

Stamina alisema “kama kuna msanii ambaye ninamkubali sana, basi ni Fid Q , kwani ni msanii pekee aliyesoma vitabu vingi sana ndiyo maana haishiwi mashairi, pamoja na uwezo wake wa kuchana.
Aidha Fid Q alisema mwanzoni aliwawachukua vijana 6 ambao bado walikuwa hawajakomaa, kwa hiyo akawafanya kama wanafunzi na kuwafundisha muziki, na hatimae sasa mmoja wao amemaliza masomo  na kuwa msanii ambaye aliyeiva kimuziki.

Fid Q alisema “nimeamua kuwafundisha vijana muziki ili wawe na uwezo kama wangu na kuwapa fursa katika maisha yao kwa sababu ni vigumu sana mtu kumpa kazi ambayo itamsaidia kimaisha ila ukimpa fursa utamsaidia sana kuliko kumpa pesa. Alimalizia.

A.Y ASHEREKEA PARTY YAKE NA WATU MBALIMBALI BAADA YA KUPATA TUZO YA CHANNEL "O"


Msanii wa Bongo Fleva almaarufu kama A.Y.baada ya kuwania tuzo ya Channel O Most Gifted East African Award huko nchini South African.
Siku ya jana katika maeneo ya Nyumbani Lounge aliweza kualika ndugu,jamaa na marafiki ili waje kusherekea ushindi wa tuzo hiyo pia bila kusahau mastaa mbalimbali walijitokeza kwa wingi.
                                                           Mchizi Mox,marafiki wa A.y
                                                                      Ommy Dimpoz
                                                       Bonny Love akiwa Mchizi Mox
                                                  Gerry Rhymes,Mchizi Mox na Gk
                                                                 Fm kibonde na A.Y


Sunday, December 2, 2012

Saturday, December 1, 2012

TUDD THOMAS ATOA SIRI YA MAFANIKIO YAKE


Najua nikizungumzia ma producer wakali katika tasnia hii ya muziki hapa bongo basi Tudd thomas atakuwa katika list yangu,sasa leo baada ya kuchonga naye aliweza kunieleza siri ya mafanikio yake katika muziki wa hapa bongo.Alisema kwamba katika maisha yake atosahau kitu kinachoitwa ngoma kwani alieleza hizo ndizo zimemfanya hii leo kujulikana katika tasnia ya muziki na kufanya kazi za wasanii.......... Soma zaidi kwenye Dj Fetty Blog: