UA-45153891-1

Sunday, October 27, 2013

WEMA SEPETU AFIWA NA BABA YAKE MZAZI BALOZI ISAAC ABRAHAM SEPETU

Balozi Abraham Isaac Sepetu amefariki dunia mapema leo akiwa katika hospitali ya TMJ alikokuwa amelazwa akitibiwa ugonjwa wa Kisukari na kiharusi alioupata hivi karibuni akiwa mjini Zanzibar. Balozi Sepetu, ambaye pia ni baba mzazi wa Miss Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu, hadi anapatwa na ugonjwa na hatimaye mauti, alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Uwekezaji wa Vitega Uchumi Zanzibar.

Wema Sepetu akiwa na wazazi wake enzi za uhai wa baba yake
Alichokiandika Wema Sepetu kwenye mtandao wa kijamii wa  Instagram  baba yake alipokuwa amelazwa Hospitali. Kwenye picha ni mama yake mzazi na baba yake wakiwa hospitalini

WANAFUNZI WA BARBRO JOHANSSON GIRLS WAKUTANA NA DIAMOND MLIMANI CITY, SAHIHI ZAMIMINIKA KWENYE SALE ZA SHULE

Wakiwa  kwenye duka la nguo ndani ya jengo hilo la biashara,  wakakutana na mwanamuziki Diamond akifanya manunuzi ya hapa na pale
  
Picha zikaanza kupigwa
"Hii kama vipi tutaipamba bwenini..........."
Hapa Design kama Ngololo inachezwa kimtindo
"Sign...koleza wino isifutike hata nikifua........."

BABY MADAHA KUZINDUA PERFUME YAKE NCHINI TANZANIA

Baby Madaha

Msanii wa Bongo Fleva Baby Madaha ambaye miezi michache iliyopita alikula mkataba mnono wa  Cand & candy records nchini Kenya, anakuja kuzindua Perfume yake  hapa nchini Tanzania.Alisema kwamba ameshazindua hiyo bidhaa yake jijini Nairobi na sasa anakuja kufanya hivyo nyumbani.

WEMA SEPETU AENDELEA KUNG'ARA


 Wema Sepetu

Muigizaji na Mkurugenzi Mtendaji wa Endless Fame Wema Sepetu, ametunukiwa tuzo ya kuwa muigizaji bora anayesaidia vijana katika sanaa ya uigizaji na jamii kwa ujumla. Alikabidhiwa tuzo hiyo kutoka Rahabu Medical Oktoba 25, 2013 katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.

JUMA NATURE BADO YUPO SANA- HII NI SERENGETI FIESTA 2013 DAR ES SALAAM, TANZANIA

 Mashabiki
Juma Nature akifanya vitu vyake
KR Muller akiwa jukwaani kwenye 'Show' ya Juma Nature

Friday, October 25, 2013

TAZAMA HII RAMANI - KUTOKA SHEKILANGO MPAKA BAMAGA KUNA 'BAR' 260..!


Hii ni barabara ya Shekilango inayopita eneo la Sinza jijini Dar es salaam.

Ni taarifa zilizosikika kutoka chanzo cha habari cha hapa nchini Tanzania wakati akizungumza msemaji wa Taasisi ya kijamii ya kupambana na tatizo la utumiaji wa vilevi kwa wanafunzi.

Siku za nyuma, gazeti la The African lilifanya utafiti na kubaini kwamba eneo la Sinza ndilo linaloongoza kwa kuwa na 'Bar' nyingi zaidi nchini Tanzania kwa kipimo cha Bar per unit Square KM.

FAHAMU HISTORIA YA ‘DAVIDO’ KWA UFUPI KABLA HAJAFANYA YAKE NDANI YA FIESTA 2013 DAR ES SALAAM, LEADERS CLUB

David Adedeji Adeleke 'Davido'

JINA lake halisi ni David Adedeji Adeleke. Ni Mtayarishaji wa muziki, mwandishi wa nyimbo na muimbaji,  mtoto wa  mfanyabiashara bilionea Dk. Deji Adeleke. Alizaliwa  Novemba 21, 1992 kwenye familia ya Bw. Deji na Bi.Vero Adeleke ndani Atlanta, Georgia nchini Marekani na baadae  kuletwa jijini Lagos nchini Nigeria.

 Akiwa na umri wa miaka 13 alianza kujifunza utayarishaji wa muziki kupitia studio nyingi tofauti  na baadae kujiunga na kundi la muziki la shuleni alipokuwa ‘High school’. Baadae alianza kufanya kazi na wasanii chipukizi wa wakati huo nchini Nigeria ambao ni Dammy Krane, NPZ na wengine katika miondoko ya Afropop  na Afrobeat .

Alianza kupata umaarufu mwaka 2011 kupitia wimbo wake wa ‘Back When’ aliomshirikisha rapper wa Nigeria Naeto.C. Aliendelea kufanya shughuri za kimuziki na wasanii wengine akiwemo Wizkid, Ice Prince, 2face, Olamide, Lynxxx na Skales, huku akiendelea na masomo katika Chuo kikuu cha Babcock  jimboni Ogun nchini Nigeria.

Albam yake inayoitwa ‘Dami duro’ aliyoitoa November 2011, ndiyo iliyomfanya kuwa mwanamuziki anayependwa kuliko wote nchini Nigeria katika miondoko ya Afro Pop. Mpaka mwishoni mwa mwaka jana alikuwa Balozi ‘Brand Ambassador’ wa MTN na tunapomzungumzia hivi sasa, hana tofauti sana na wanamuziki kama D’banj, Wizkid, Don Jazzy na wengine kimapato kupitia mikataba mikubwa ya kibiashara ‘Endorsement’.

Yuko kwenye ‘Label’ ya muziki ya HKN Records ambayo yeye pia ni mmoja wa waanzilishi na wamiliki wake.

Wednesday, October 23, 2013

DIVA ATAMANI COLLABO LA SHILOLE NA IYANYA

Loveness Love 'Diva'

MTANGAZAJI  wa Clouds FM Loveness Love 'Diva' ametamani ufanyike wimbo wa kushirikiana kati ya mwanamuziki wa Bongo Flava na Filamu 'Shilole' na Mwanamuziki wa Nigeria 'Iyanya'. "Natamani Iyanya afanye collabo na Shilole maana staili zao za muziki zinafanana", alisema Diva kwenye kipindi chake cha 'Ala za roho' Octoba 21, 2013 huku wimbo unaotamba Afrika wa mwanamuziki Iyanya, unaoitwa 'Kukere' ukichezwa redioni. 

Shilole ambaye siku chache zilizopita alisikika akisema ana mpango wa kurekodi wimbo na Jenifer Lopez wa nchini Marekani, anafanya vizuri na wimbo wake mpya wa 'Nakomaa na jiji' na ataungana na wasanii wengine wa Bongo Flava kwenye tamasha la Fiesta litakalofanyika Jumamosi ya Oktoba 26,2013 katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.

Iyanya anakuja nchini Tanzania kwa ajiri ya tamasha hilo na ataungana na wasanii wengine kutoka nje ambao ni 'Davido' wa Nigeria, 'Mohombi' wa Sweeden, 'Alaine' wa Jamaica na wengine.

Shilole na Iyanya

Tuesday, October 22, 2013

KILA LA KHERI DIAMOND, NAY WA MITEGO, OMMY DIMPOZ, LADY JAYDEE NA RICH MAVOKO


Mastaa wa Bongo flava Diamond, Nay wa mitego, Ommy Dimpoz, Lady Jaydee na Rich Mavoko, wanachuana kwenye kipengele  cha msanii bora wa Tanzania 'Best Artist Tanzania' katika tuzo za Nzumari za nchini Kenya ambazo zitafanyika Novemba 23, 2013.

Nay wa mitego na  Ommy Dimpoz wameingia katika vipengele viwili ambapo kipengele kingine walichoingia ni wimbo bora wa Afrika Mashariki 'Best Song East Africa'.Katika kipengele hicho, wimbo wa 'Muziki gani' wa Nay wa mitego aliomshirikisha Diamond unachuana na  'Tupogo' wa Ommy Dimpoz, 'Badilisha' wa Jose Chameleone wa Uganda na 'Mobimba' wa P-Unit wa nchini Kenya.


 Best Artist Tanzania
Nay wa mitego
Diamond
Ommy Dimpoz
Lady jaydee
Rich Mavoko

Best Song East Africa
Muziki gani-Nay wa mitego ft Diamond
Badilisha- Jose Chameleone
Mobimba- P-Unit
Tupogo-Ommy Dimpoz

Monday, October 21, 2013

ALIVYOZUNGUMZIWA NYAISANGA ENZI ZA UHAI WAKE

Hapa ni kupitia Facebook, baada ya mdau mmoja kutaka kujua aliko
Click picha hizi kusoma Comments.

Comment ya mwisho ni muda mfupi baada ya kuwa amefariki dunia .

Alichoandika kwa mara ya mwisho kwenye akaunti yake ya Twitter 

 R.I.P Julius Nyaisanga

Saturday, October 19, 2013

YALE YA NICK MINAJ YASIMKUTE ROSE MUHANDO

Rose Muhando

SIWAFANANISHI wanamuziki hawa kwa aina za muziki wazifanyazo wala tabia zao, La hasha!. Nazungumzia yanayotokea kwenye mitandao ya kijamii ambayo inatuunganisha bila kujali kazi zetu, vipaji vyetu na imani zetu, maana ubunifu unafanywa na watu tofauti.

Watu maarufu  kama wanamuziki, waigizaji,  wanamitindo, viongozi na wengine ndio wanaoongoza kwa kuwa na wafuasi wengi kwenye mitandao hiyo. Pamoja na hayo ni jambo la kawaida sana wafuasi hao ambao pia ni mashabiki wao kufungua hata akaunti kwa majina yao. Utakuta jina la mtu flani maarufu likiwa kwenye akaunti zaidi ya tano mpaka kumi, lakini yake na anayoitambua ni moja.

Siyo kitu kibaya katika mtazamo wa kupima jinsi gani mtu amepata umaarufu maana shughuri hizo zinahitaji upate umaarufu, ndipo kazi yako inaweza kukulipa zaidi.Japo wengine hufanya hivyo si kwa nia njema bali kwa malengo ya kuharibu majina na watu hao au kujipatia masrahi binafsi. Kikubwa hapa ni uvumilivu na kutoa taarifa kwa vyombo husika yatokeapo mabaya maana kwa ulimwengu wa sasa, ukiamua kuikimbia mitandao hii utawakosa wengi pia.

Mwimbaji wa nyimbo za injili Tanzania, Rose Mhando ambaye  aliwai kusema hana akaunti yeyote ile katika FACEBOOK na watu wanaotumia ni kwaajili ya manufaa yao na sio yeye. Aliwaomba wanaotumia hilo jina kwenye hiyo  akaunti kuacha mara moja na kusema atakapozindua ya kwake ambayo ni ya kweli atawaambia mashabiki wake. Kwa mara nyingine tena hivi punde amesikika akisema kuna matapeli wametumia jina lake kufungua akaunti ya Facebook ya kampuni ya mikopo kwa jina lake na kupelekea watu wengi kumfuata wakitafuta fomu za kuomba mikopo.

Semadat ilipomtafuta Rose muhando kwenye mtandao huo ilikuta jina lake kwa akaunti 5 na kurasa, yaani facebook page 3, kwa jina hilo hilo, bila kujua ipi ni akaunti yake halisi.Kuna changamoto za namna tofauti zinazoweza kujitokeza unapotumia mitandao hii kama mtu maarufu, 'brand' au 'Public figure' maana wakati mwingine hata ndani ya mtandao wako halisi, mashabiki wako wanaweza kukuzungumzia vibaya au kutumia lugha isiyokuwa nzuri.

Mwanamuziki wa Marekani Nick Minaj alijitoa kwenye mtandao wa TWITTER kwa kuifuta kabisa akaunti yake baada ya baadhi ya mashabiki wake wakereketwa kuchukia na kumtukana. Ni baada ya wimbo wake aliotarajia kuuzindua kuvuja kupitia mtandao wenye jina lake pasipo yeye kujua. Hata hivyo alishindwa kuvumilia kuwa nje ya mtandao huo ambao ulimuweka karibu na mashabiki wake, akaamua kurudi Twitter baada ya muda mfupi japo alikuwa tayari amewapoteza wafuasi zaidi ya milioni 11.

Namtakia Rose Mhando uvumilivu katika mitandao ya kijamii maana yeye ni staa ambaye kukubalika kwake kumetokana na kipaji na ubunifu wake mwenyewe na kama yupo kwenye mitandao hiyo,  ambayo kibiashara zaidi inaitwa 'Social Media' badala ya 'Social Networks' aendelee kubaki.


Nick Minaj

UMESIKIA TANGAZO MOJA, SAUTI YA MTOTO AKISEMA "BABA TUCHEZE BAISHOO"? NI HUYU HAPA!



Ni mtoto wa Msanii wa Bongo Flava D-KNOB, anayeitwa Vivica. Aliyembeba ndiye baba yake ambaye alitamba na wimbo wa 'Bad Man' ambao alimshirikisha Carnibal wa nchini Kenya. Nyimbo zingine ambazo mistali ya D-Knob ilisikika ni pamoja na 'Niwe na wewe', 'Elimu mtaani.com' na 'Sauti ya gharama'.

Friday, October 18, 2013

MTOTO WA MIAKA 9 WA NCHINI NIGERIA ALAMBA SHAVU KWENYE KAMPUNI YA MICROSOFT

Jomiloju Tunde-Oladipo

NAMBA  ya wanigeria waliothibitishwa kwa vyeti maalum na kufanya kazi kwenye kampuni maarufu duniani ya Kompyuta ya Microsoft, inazidi kuongezeka lakini kilicholeta utofauti zaidi ni mtoto anayeitwa Jomiloju Tunde-Oladipo mwenye umri wa miaka 9 aliyenyakua cheti au ‘Gamba’ la  ‘Microsoft Certified Professional’ hivi punde.

Imetokea baada mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi kuwa wa kwanza kati ya mwanafunzi 21 wa shule za msingi waliofanya mtihani kwa ajiri hiyo jijini Lagos. Amechukuliwa na kampuni hiyo kama mtaalam wa program ya Microsoft Office ‘Microsoft Office Specialist’ (MOS) upande wa Word 2010 baada ya kupata alama 769 kati ya 1000, ambapo amezidisha  alama 69 kutoka alama 700 ambazo ndicho kilikuwa kiwango cha chini (Pass marks).

Amekwenda kuungana na Lavish Nashree wa miaka 8 kutoka nchini India, na wengine wawili Arfa na Thobani kutoka Pakistan.


“Haikuwa kazi raisi maana nilifanya mtihani mwaka jana sikufanikiwa, lakini niliendelea kusoma kwa bidii nikiwa nyumbani na shuleni pia. Niko kwenye Kompyuta siku zote baada ya muda wa masomo. Kama sifanyi chochote, basi nilienda kwa mwalimu wangu wa Teknolojia ya habari na mawasiliano kujifunza zaidi” Alisema Jomiloju.


Mwalimu wake wa darasa Bi. Elizabeth Ogunrinola pia alisema mtoto huyo ana kipaji cha pekee kwa kuwa si kwamba yuko vizuri kwenye somo la ICT (Tehama) tu, bali masomo yote. Anasoma kwa bidii na ana nidhamu ya hali ya juu.


Baba yake aliongeza kwa kusema “Si kwamba  ni malezi yetu tu yanayomfanya awe vile, lakini ni mtoto mwenye uwezo binafsi, maana ana vipaji vingi, anaweza kutumia vyombo vya muziki ikiwa pamoja na Saxophone na Kinanda (Keyboard).  Ni muigizaji mzuri na ana uwezo mkubwa wa kuogelea. Kila mwisho wa muhula hushiriki kwenye maigizo na mashindano ya quiz. Pia mwaka huu amepata zawadi za masomo mengi ikiwa pamoja na somo la ICT.


‘Microsoft Certified Professional’ ni vyeti ambavyo hutolewa na kampuni ya Microsoft kwa watu ambao wamethibitishwa na kampuni hiyo kuwa na ujuzi katika kutatua matatizo ya programu za Kompyuta, hasa zile zinazotumiwa na watumiaji wa kawaida au wa mwisho (End users) kupitia mifumo ya Windows XP, Vista, Windows7 na zingine kama hizo.

JARIDA JIPYA LA VIBE LATOA FULSA KWA WANAFUNZI WA VYUO


Ukurasa wa  juu (Front page) wa Jarida la Vibe

Jarida jipya la Vibe ambalo limeanza kutoka mwezi huu, yaani October 2013 limewaomba wanafunzi wa vyuo wajitokeze kuwa mabalozi wake "Ambassadors".

 Afisa Mtendaji Mkuu wa Vibe amesema Wanafunzi watakaopata nafasi hizo watanufaika kwa kupata uzoefu wa kazi hasa katika tasnia za Masoko na Habari na pia watapewa barua za utambuzi wa utendaji kazi. Pia amesema, watasaidiwa kupata kazi hasa katika makampuni ambayo Vibe inafanya nayo kazi za Masoko.

Kwa maelezo zaidi tembelea: vibe.co.tz. Pia unaweza kuwatumia email: info@vibe.co.tz.

Thursday, October 17, 2013

BABA YAKE KANUMBA AINGIA RASMI KWENYE FILAMU

Mzee Charles Kanumba

Baba mzazi wa aliyekuwa muigizaji maarufu wa filamu nchini Tanzania Steven Kanumba, Mzee Charles Kanumba ,ameingia kwenye fani ya uigizaji kikwelikweli na tayari yupo kwenye soko la Bongo Movie baada ya kuigiza kwenye filamu inayoitwa “Mwananjilinji” ambayo tayari imeuza kopi za kutosha kanda ya ziwa.

Amesema anafanya hivyo kwa ajiri ya kumuenzi mtoto wake ambaye vipaji vingi alivyokuwa navyo alivirithi kutoka kwake. Alipoulizwa ana vipaji gani, kupitia Amplifier ya Clouds FM, amesema yeye ni muimbaji wa kwaya  muda mrefu sana, mpiga gitaa, muigizaji na mchekeshaji ambaye amekuwa akiyafanya yote hayo kwenye shughuri za kanisa.

Amesisitiza kwamba wapenzi wa filamu wakae mkao wa kula na watarajie makubwa sana kutoka kwake.

REHANNA ANGEKUWA BONGO ANGEKWISHAIMBA BONGO FLAVA, TAARABU NA MCHILIKU


 Rehanna

Muimbaji wa Marekani Robyn Rihanna Fenty ‘Rihanna’ anasifika kwa ubunifu mkubwa na kutumia fulsa vizuri inapotokea. Anafanya muziki wa staili nyingi tofauti na kila anapogusa anatikisa ulimwengu wa muziki. Kumbuka nyimbo zake za RnB ukiwemo wa “Unfaithful”, za dancehall ukiwemo wa "Pon de Replay," na nyimbo zenye mchanganyiko wa RnB, Pop na Hip Hop kama "Umbrella” ambao mwanzoni ulikuwa umeandikwa kwa ajiri ya Britney Spears.


Wimbo wa Umbrella ambao alimshirikisha Jay-Z uliandikwa na watu wanne  ambao ni The-Dream, Christopher Stewart, Kuk Harrell pamoja na Jay-Z kwa ajiri ya  Britney lakini ukakataliwa, ndipo Rehanna akasema “leta huku huo wimbo”. 
  
Wimbo huo ulimpa umaarufu mkubwa sana na kuwa wimbo kinara kati ya nyimbo zilizotoka nao kwenye Albam moja. Mwaka 2007 ulipata tuzo ya MTV kama video bora, baadae ukaingia kwenye ushindani wa tuzo za Grammy mwaka 2008 kwenye vipengele vya rekodi bora ya mwaka, wimbo bora wa mwaka na wimbo bora wa kushirikiana na kumfanya Rihanna na Jay-Z waondoke na tuzo ya Grammy ya wimbo bora wa kushirikiana kwa mwaka huo.

KIM KARDASHIAN ALIVYOTANGAZA KUJITOA KWENYE MTANDAO WA KIJAMII WA INSTAGRAM

Kim Kardashian akiwa na Kanye West

Alipokuwa tayari anafuatwa na watu 5,731,011 kwenye Instagram, mwanamuziki Kim Kardashian alitangaza kujitoa kwenye mtandao huo kwa kufunga akaunti yake mwishoni mwa mwaka jana. Ni baada ya Instagram kuongeza kipengere cha vigezo na masharti ya kutumia mtandao huo Desemba 17, 2012 ambacho kingepelekea picha za watumiaji kuuzwa kwa ajiri ya matangazo pasipokuwalipa wamiliki wa picha hizo.

Maelezo yalikuwa kama ifuatavyo “Unakubari kwamba kampuni au biashara yoyote inaweza kutulipa kuonyesha picha zako, jina lako na mambo mengine kwa ajiri ya matangazo nawewe husipate malipo yoyote”.

Hata hivyo, siku moja baada ya hapo, Instagram iliwaomba radhi watumiaji wake kwa kusema  kwamba, lengo lao lilikuwa kufanya majaribio ya tekinolojia ya matangazo ya mtandao huo japo maelezo yao hawakuyaweka vizuri na watumiaji wakaelewa visivyo.

Kujitoa kwa Kim Kardashian ambaye ndiye alikuwa anaongoza kwa kuwa na wafuasi wengi akifuatiwa na Justin Bieber  aliyekuwa na wafuasi  milioni 4.3 na Obama wafuasi milioni 1.8, kungepelekea kujitoa kwa ndugu zake Khloe, Kylie, Kendall na Rob Kardashian ambao wote walikuwa katika kumi bora ya waliofuatwa na watu wengi kwenye mtandao huo kwa wakati huo.

Kim Kardashian aliendelea kubaki Instagram na mpaka kufikia mwishoni mwa September 2013 alikuwa akifuatwa na watu 9, 935, 306. Ni wa 3 kati ya akaunti 10 duniani zilizofuatwa na watu wengi kwenye mtandao huo akiwa tayari amepitwa na Justin Bieber mwenye  watu 10,822, 685 ambaye anachukua namba 2 akitanguliwa  na  Instagram yenyewe ambayo ndiyo namba 1 .

Inasemekana ujauzito wake na kujifungua vimechangia Kim kupitwa na Justin Bieber kutokana na kuwa muda mrefu mbali na Kamera na picha zake kutosambaa zaidi ikilinganishwa na awali. Kim Kardashian ni mama wa mototo wa Kanye West.

Wednesday, October 16, 2013

AKAUNTI 10 ZA INSTAGRAM ZILIZOONGOZA DUNIANI KWA KUFUATWA NA WATU WENGI ZAIDI MWISHONI MWA SEPTEMBA 2013


1. Instagram yenyewe: 38,022,266

 2.Justin Bieber: 10,822, 685

 
 3. Kim Kardashian: 9, 935, 306
 
4. Rehanna :9,783,752
5. Ariana Grande:7,150,544

6. Kendell Jenner: 6,620,755
7. Taylor Swift: 6,543,194

8. Beyonce: 6,515,223  
9. Khloe Kardashian: 6,241,358

10. Kylie Jenner: 5,907,168

'EID- EL- HAJI' YAANGUKIA 'SIKU YA CHAKULA DUNIANI'



 Eid-el-Haji imeangukia tarehe ya siku ya chakula duniani ambayo huazimishwa Octoba 16 kila mwaka. Kauli mbiu ya siku ya chakula duniani mwaka huu 2013  ni 'Sustainable Food Systems for Food Security and Nutrition'.
 
   
Semadat inakutakieni Eid njema.

Monday, October 14, 2013

ALICHOANDIKA KWENYE 'TWITTER' WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA MH. BERNARD MEMBE MAPEMA LEO OCTOBER 14, 2013 ANAPOMKUMBUKA MWL NYERERE



TAZAMA USANII WA MWALIMU NYERERE

UKITEMBELEA katika maduka ya vitabu na maktaba utakuta vitabu vilivyoandikwa na watu mbalimbali vinavyofundisha sanaa ya usemaji ‘The art of public speaking’, lakini hotuba za Mwalimu nyerere ni zaidi ya sanaa hiyo.

Pia ukisoma maandishi ya (Erick, 2009), utaona jinsi gani Mwalimu alikuwa msanii kwa kuwa aliweza kuhusianisha falsafa ya Ujamaa na moja ya kazi za sanaa za mikono ambayo ni kinyago cha Mmakonde kilichoitwa Dimoongo cha Robert Yakobo Sangwani na kupelekea sanamu au kinyago hicho kubadilishwa jina na kuitwa Ujamaa. Alikilinganisha kinyago hicho na ujamaa kutokana na muundo wake jinsi watu walivyoshikamana kila mmoja akiwa kama nguzo ya kumsaidia mwingine hasianguke. Inasemekana Mwalimu Nyerere ndiye alikibadilisha jina kinyago hicho na kukiita UJAMAA.

Kinyago  cha kimakonde kilichotolewa mfano wa Ujamaa na Baba wa Taifa Mwalimu J.K. Nyerere

Ngao (Nembo) ya Taifa ambayo ni moja ya alama za Taifa, inaonyesha sanaa na ubunifu wa hali ya juu uliomo katika alama zingine za Taifa kama Bendera, Wimbo wa Taifa na Mwenge wa Uhuru. Yaliyomo, ikiwa ni pamoja na Bibi na Bwana kama ishara ya haki sawa pasipokujali jinsia, yote ni alama ya kauli mbiu ya UHURU na UMOJA ambapo pia ni jina la kitabu cha Mwalimu Nyerere cha mwaka 1966. Pia aliandika vitabu vingi ambavyo vinapatikana makumbusho ya Mwalimu Nyerere.

Ngao ya Taifa

Kwa kuwa wasanii na wabunifu wengi walimtazama na wanamtazama Mwalimu Nyerere kama kiongozi shupavu na ‘Role Model’ wao kitaifa na kimataifa kwa jinsi ya kuonyesha matumizi halisi ya sanaa katika kujenga picha na  mawazo chanya, kwa wao pia inaweza kuwa raisi kubadilisha mawazo kuwa katika vitendo tunapoazimisha siku ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Oktoba 14, 2013.

Saturday, October 12, 2013

MSHINDI WA BIG BROTHER AFRICA (BBA) DILLISH MATTHEWS ALIPOKUWA MDOGO


 



Oktoba 11, 2013 ilikuwa siku ya kimataifa ya mtoto  wa kike ambapo mataifa yote hutumia siku  hiyo kutangaza na kuhamasisha haki za watoto wa kike na kutokomeza ubaguzi wa kiuchumi, kijamii na kisiasa.  Taifa lolote linaweza kuendelea kama mtoto wa kike atapata nafasi ya kushiriki kwenye nyanja zote.

Masaa machache kabla ya siku hiyo, kaimu barozi wa Marekani nchini Tanzania ametoa wito kwa watanzania kila mmoja achague mtoto mmoja wa kike atakayemsaidia ili afikie upeo wa uwezo wake kwa kuongea nae, kushirikiana nae na kutambua vikwazo alivyonavyo. Aliendelea kusisitiza kwamba, mtoto wa kike anapoendelea, taifa zima linaendelea.