David Adedeji Adeleke 'Davido'
JINA lake halisi ni David Adedeji Adeleke. Ni Mtayarishaji wa muziki, mwandishi wa nyimbo na muimbaji, mtoto wa mfanyabiashara bilionea Dk. Deji Adeleke. Alizaliwa Novemba 21, 1992 kwenye familia ya Bw. Deji na Bi.Vero Adeleke ndani Atlanta, Georgia nchini Marekani na baadae kuletwa jijini Lagos nchini Nigeria.
Akiwa na umri wa miaka 13 alianza kujifunza utayarishaji wa muziki kupitia studio nyingi tofauti na baadae kujiunga na kundi la muziki la shuleni alipokuwa ‘High school’. Baadae alianza kufanya kazi na wasanii chipukizi wa wakati huo nchini Nigeria ambao ni Dammy Krane, NPZ na wengine katika miondoko ya Afropop na Afrobeat .
Alianza kupata umaarufu mwaka 2011 kupitia wimbo wake wa ‘Back When’ aliomshirikisha rapper wa Nigeria Naeto.C. Aliendelea kufanya shughuri za kimuziki na wasanii wengine akiwemo Wizkid, Ice Prince, 2face, Olamide, Lynxxx na Skales, huku akiendelea na masomo katika Chuo kikuu cha Babcock jimboni Ogun nchini Nigeria.
Albam yake inayoitwa ‘Dami duro’ aliyoitoa November 2011, ndiyo iliyomfanya kuwa mwanamuziki anayependwa kuliko wote nchini Nigeria katika miondoko ya Afro Pop. Mpaka mwishoni mwa mwaka jana alikuwa Balozi ‘Brand Ambassador’ wa MTN na tunapomzungumzia hivi sasa, hana tofauti sana na wanamuziki kama D’banj, Wizkid, Don Jazzy na wengine kimapato kupitia mikataba mikubwa ya kibiashara ‘Endorsement’.
Yuko kwenye ‘Label’ ya muziki ya HKN Records ambayo yeye pia ni mmoja wa waanzilishi na wamiliki wake.
No comments:
Post a Comment