UA-45153891-1

Sunday, October 6, 2013

ALLAN LUCKY- MTANGAZAJI WA TELEVISHENI, MWANAMASOKO , MUIGIZAJI, MWANATEHAMA NA MWANAHARAKATI WA MAENDELEO YA ELIMU TANZANIA



Ni maarufu kama “RAISI WA WANAFUNZI”.  Alikulia katika ulimwengu  wa taaluma huku akitamani kuitumia taaluma yake kwenye shughuri za habari zinazolenga kuwakomboa vijana kielimu.

Safari yake ilianzia shule ya msingi Majimaji,  Songea  mkoani Ruvuma kabla hajahamia shule ya msingi Luhira ambako ndiko alikohitimu elimu hiyo mwaka 1998. Aliendelea na elimu ya sekondari  ya “O Level” katika shule ya sekondari Ruvuma  na kufauru kwa daraja la kwanza “Division one, akiwa na  alama ya ‘A’  katika somo la Jiografia,  hivyo akachaguliwa kuendelea na masomo  ya  “A Level” katika  shule ya Sekondari  Minaki  mchepuo wa EGM.  Akiwa amefauru mtihani wa kidato cha sita kwa daraja la pili “Division two”, alijiunga na Chuo cha usimamizi wa fedha  ( IFM) mwaka 2005 kusomea ‘Computer Science’  na kuhitimu  mwaka 2008,  ndipo  akaanza kuzitafuta nafasi za kuonyesha uwezo wake katika taaluma na ubunifu  wa hapa na pale.

Kipindi akiwa masomoni tayari alikuwa ameanza kushiriki matukio mbalimbali kama usimamizi wa miradi na utangazaji, ukiwemo mradi wa mawasiliano wa  ‘Intergrated Communications’,  ‘Whitedent Schools Dental Check-up’ mwaka 2005, ‘Safari Pool Shoot Out’ mwaka 2005 na 2006, ‘Coca Cola Olympic Torch Relay (OTR)’ mwaka 2008 pamoja na ‘Whitedent School Quiz’ ambapo yote ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Aliamini anaweza kuwa mtangazaji mzuri wa TV na ndipo akaamua kushiriki mashindano ya kumtafuta mtangazaji wa kipindi cha Planet Bongo cha EATV mwaka 2008 na kuingia katika fainali, yeye na wengine 6.  Japo hakuwa mtangazaji wa kipindi hicho, alipata nafasi ya kuwa mfanyakazi wa TV hiyo katika shughuri za  IT zinazowezesha habari.

Ndipo akajikita moja kwa moja kwenye shughuri za habari na kuwa  mmoja wa waanzilishi wa kipindi cha SKONGA kilichoanzishwa mwaka 2009. Anatangaza katika vipindi viwili ambavyo ni SKONGA  na  5 SELECT,  vipindi ambavyo vinahusu wanafunzi wa shule za sekondari kuonyesha ujuzi na vipaji vyao. Pia anaandika habari  zinazohusu elimu kwenye gazeti tanzu au maarufu kama 'Blog'  yake ya allanluckyblog.blogspot.com.



No comments:

Post a Comment