Oktoba 11, 2013 ilikuwa siku ya
kimataifa ya mtoto wa kike ambapo mataifa yote hutumia siku hiyo
kutangaza na kuhamasisha haki za watoto wa kike na kutokomeza ubaguzi wa
kiuchumi, kijamii na kisiasa. Taifa lolote linaweza kuendelea kama mtoto
wa kike atapata nafasi ya kushiriki kwenye nyanja zote.
Masaa machache kabla ya siku hiyo,
kaimu barozi wa Marekani nchini Tanzania ametoa wito kwa watanzania kila mmoja
achague mtoto mmoja wa kike atakayemsaidia ili afikie upeo wa uwezo wake kwa
kuongea nae, kushirikiana nae na kutambua vikwazo alivyonavyo. Aliendelea
kusisitiza kwamba, mtoto wa kike anapoendelea, taifa zima linaendelea.
No comments:
Post a Comment