UA-45153891-1

Thursday, October 3, 2013

WAGUNDUZI WA INSTAGRAM WALIOMSHTUA MARK ZUCKBERG WA FACEBOOK

Kutoka kulia ni  Kelvin Systrom na Mike Krieger, waanzilishi wa Instagram

Instagram ni mtandao wa kijamii ambao umaarufu wake unazidi kuja juu kutokana na uwezo wake mzuri wa kuhifadhi na kusambaza picha ikiwa ni pamoja na sifa yake ya  pekee ya kubadilisha picha na kuziweka katika umbo la pande nne zinazolingana ‘Squre’, kupokea na kusambaza video kwa haraka sana.

Ulianzishwa na vijana wawili Kelvin Systrom na Mike Krieger wakiwa ndani ya jiji la San Francisco nchini  Marekani Oktoba 2010.

Mwanzilishi na CEO wa Facebook Inc, Mark Zuckerberg

Ikiwa na miaka miwili tu, April 2012, Instagram ilinunuliwa na kampuni ya Facebook Inc kwa dola za kimarekani billioni 1 ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wake 13, bei ambayo ni karibu mara tatu ya ile ambayo mtandao wa Yahoo ulitumia kununua mtandao wa picha wa Flickr mwaka 2005, ambao  ni miongoni mwa mitandao 50 maarufu duniani. Baada ya kuununua mtandao huo, CEO wa Facebook Mark Zuckerberg alisema atauacha mtandao huo ukue kivyake mbali na Facebook lakini chini ya kampuni ya Facebook Inc.


Instagram ambayo inatumiwa zaidi na watu maarufu “Celebrities” inakuwa kwa kasi sana ambapo April mwaka jana ilikuwa na watumiaji milioni 30 na mpaka sasa ina watumiaji zaidi ya milioni 100. Ni kutokana na mambo mengi yaliyofanyika kuuboresha mtandao huo hasa kwa mwaka huu 2013 ambapo kuanzia Juni 2013 imeanza kuruhusu watumiaji wake kuweka na kutuma video ya muda husiozidi sekunde 15 kitu ambacho pia kimezidi kuipa Facebook Inc thamani kubwa dhidi ya wapinzani wao wakubwa wa Twitter wanaotumia  ‘Twitter’s Vine video-sharing’.

Instagram imejishindia tuzo nyingi ikiwa ni pamoja na ile ya TechCrunch kama  mshindi wa pili wa ‘Application’ bora za simu Januari 2011, CEO wa Intagram Kelvin Systrom alitajwa nafasi ya 66 miongoni mwa watu 100 bora wabunifu katika biashara duniani Mei 2011 kupitia utafiti  uliofanywa na ‘Fast Company’. Pia mwaka huo huo Juni 2011 kampuni ijulikanayo kama INC ya Marekani iliwataja waanzilishi wa Instagram Kelvin Systrom na Mike Kriege miongoni mwa watu chini ya miaka 30 waliofanya mambo makubwa.

Tuzo zingine ilizojizolea Instagram ni ya mtandao bora ulioanzishwa ndani ya Marekani “Locally made” kutoka tuzo za ‘SF Week’ nchini humo mwaka 2011, Kampuni ya Apple Inc iliitangaza Instagram kama Application “App” bora ya simu ya mwaka 2011 na  waanzilishi wa Instagram  Kelvin na  Mike waliingia kwenye jarida la 7x7.


No comments:

Post a Comment