Rehanna
Muimbaji wa Marekani
Robyn Rihanna Fenty ‘Rihanna’ anasifika kwa ubunifu mkubwa na kutumia fulsa
vizuri inapotokea. Anafanya muziki wa staili nyingi tofauti na kila anapogusa
anatikisa ulimwengu wa muziki. Kumbuka nyimbo zake za RnB ukiwemo wa “Unfaithful”,
za dancehall ukiwemo wa "Pon de Replay," na nyimbo zenye mchanganyiko
wa RnB, Pop na Hip Hop kama "Umbrella” ambao mwanzoni ulikuwa umeandikwa
kwa ajiri ya Britney Spears.
Wimbo wa Umbrella ambao alimshirikisha Jay-Z uliandikwa na watu wanne ambao ni The-Dream, Christopher Stewart, Kuk Harrell pamoja na Jay-Z kwa ajiri ya Britney lakini ukakataliwa, ndipo Rehanna akasema “leta huku huo wimbo”.

Wimbo huo ulimpa umaarufu mkubwa sana na kuwa wimbo kinara kati ya nyimbo zilizotoka nao kwenye Albam moja. Mwaka 2007 ulipata tuzo ya MTV kama video bora, baadae ukaingia kwenye ushindani wa tuzo za Grammy mwaka 2008 kwenye vipengele vya rekodi bora ya mwaka, wimbo bora wa mwaka na wimbo bora wa kushirikiana na kumfanya Rihanna na Jay-Z waondoke na tuzo ya Grammy ya wimbo bora wa kushirikiana kwa mwaka huo.
No comments:
Post a Comment