UA-45153891-1

Monday, October 14, 2013

TAZAMA USANII WA MWALIMU NYERERE

UKITEMBELEA katika maduka ya vitabu na maktaba utakuta vitabu vilivyoandikwa na watu mbalimbali vinavyofundisha sanaa ya usemaji ‘The art of public speaking’, lakini hotuba za Mwalimu nyerere ni zaidi ya sanaa hiyo.

Pia ukisoma maandishi ya (Erick, 2009), utaona jinsi gani Mwalimu alikuwa msanii kwa kuwa aliweza kuhusianisha falsafa ya Ujamaa na moja ya kazi za sanaa za mikono ambayo ni kinyago cha Mmakonde kilichoitwa Dimoongo cha Robert Yakobo Sangwani na kupelekea sanamu au kinyago hicho kubadilishwa jina na kuitwa Ujamaa. Alikilinganisha kinyago hicho na ujamaa kutokana na muundo wake jinsi watu walivyoshikamana kila mmoja akiwa kama nguzo ya kumsaidia mwingine hasianguke. Inasemekana Mwalimu Nyerere ndiye alikibadilisha jina kinyago hicho na kukiita UJAMAA.

Kinyago  cha kimakonde kilichotolewa mfano wa Ujamaa na Baba wa Taifa Mwalimu J.K. Nyerere

Ngao (Nembo) ya Taifa ambayo ni moja ya alama za Taifa, inaonyesha sanaa na ubunifu wa hali ya juu uliomo katika alama zingine za Taifa kama Bendera, Wimbo wa Taifa na Mwenge wa Uhuru. Yaliyomo, ikiwa ni pamoja na Bibi na Bwana kama ishara ya haki sawa pasipokujali jinsia, yote ni alama ya kauli mbiu ya UHURU na UMOJA ambapo pia ni jina la kitabu cha Mwalimu Nyerere cha mwaka 1966. Pia aliandika vitabu vingi ambavyo vinapatikana makumbusho ya Mwalimu Nyerere.

Ngao ya Taifa

Kwa kuwa wasanii na wabunifu wengi walimtazama na wanamtazama Mwalimu Nyerere kama kiongozi shupavu na ‘Role Model’ wao kitaifa na kimataifa kwa jinsi ya kuonyesha matumizi halisi ya sanaa katika kujenga picha na  mawazo chanya, kwa wao pia inaweza kuwa raisi kubadilisha mawazo kuwa katika vitendo tunapoazimisha siku ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Oktoba 14, 2013.

No comments:

Post a Comment