Siku ya wanyama duniani inasherehekewa kila mwaka Oktoba 4, ilianzia maeneo ya Florence nchini Italy mwaka 1931 kwenye mikutano ya wanaikolojia. Katika siku hiyo, mifumo mbalimbali ya maisha ya wanyama husherehekewa kwa matukio yanayoandaliwa kwa namna tofauti ikiwa pamoja na makongamano, matamasha, harambee za kuchangia mifuko kwa ajiri ya kuandaa mazingira safi na makazi ya wanyama pamoja na kutembelea mbuga za wanyama.
Ni siku ambayo wanyama husaidiwa kufurahi, kupata matibabu na kuhamasisha kutatua matatizo yanayowakumba kama kuteswa na binadamu, kugongwa na vyombo vya usafiri na kuuawa kwa makusudi. Pia wanaharaki wa haki za wanyama hutumia siku hiyo kama fursa ya kuelimisha watu juu ya haki hizo.
Kwa hapa nchini Tanzanaia siku hii inasherehekewa kwa shughuri kama hizo ambapo mbwa watafanya gwaride maeneo ya Kimele kata ya Mapinga maeneo ya Bagamoyo.
Katibu mtendaji wa chama cha kuzuia ukatiri kwa wanyama Tanzania TSPCA Bi. Johari Abdrahaman, ametoa wito kwa watanzania kuwapenda wanyama, kuwathamini na kujua haki zao za msingi.
No comments:
Post a Comment