UA-45153891-1

Friday, October 18, 2013

MTOTO WA MIAKA 9 WA NCHINI NIGERIA ALAMBA SHAVU KWENYE KAMPUNI YA MICROSOFT

Jomiloju Tunde-Oladipo

NAMBA  ya wanigeria waliothibitishwa kwa vyeti maalum na kufanya kazi kwenye kampuni maarufu duniani ya Kompyuta ya Microsoft, inazidi kuongezeka lakini kilicholeta utofauti zaidi ni mtoto anayeitwa Jomiloju Tunde-Oladipo mwenye umri wa miaka 9 aliyenyakua cheti au ‘Gamba’ la  ‘Microsoft Certified Professional’ hivi punde.

Imetokea baada mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi kuwa wa kwanza kati ya mwanafunzi 21 wa shule za msingi waliofanya mtihani kwa ajiri hiyo jijini Lagos. Amechukuliwa na kampuni hiyo kama mtaalam wa program ya Microsoft Office ‘Microsoft Office Specialist’ (MOS) upande wa Word 2010 baada ya kupata alama 769 kati ya 1000, ambapo amezidisha  alama 69 kutoka alama 700 ambazo ndicho kilikuwa kiwango cha chini (Pass marks).

Amekwenda kuungana na Lavish Nashree wa miaka 8 kutoka nchini India, na wengine wawili Arfa na Thobani kutoka Pakistan.


“Haikuwa kazi raisi maana nilifanya mtihani mwaka jana sikufanikiwa, lakini niliendelea kusoma kwa bidii nikiwa nyumbani na shuleni pia. Niko kwenye Kompyuta siku zote baada ya muda wa masomo. Kama sifanyi chochote, basi nilienda kwa mwalimu wangu wa Teknolojia ya habari na mawasiliano kujifunza zaidi” Alisema Jomiloju.


Mwalimu wake wa darasa Bi. Elizabeth Ogunrinola pia alisema mtoto huyo ana kipaji cha pekee kwa kuwa si kwamba yuko vizuri kwenye somo la ICT (Tehama) tu, bali masomo yote. Anasoma kwa bidii na ana nidhamu ya hali ya juu.


Baba yake aliongeza kwa kusema “Si kwamba  ni malezi yetu tu yanayomfanya awe vile, lakini ni mtoto mwenye uwezo binafsi, maana ana vipaji vingi, anaweza kutumia vyombo vya muziki ikiwa pamoja na Saxophone na Kinanda (Keyboard).  Ni muigizaji mzuri na ana uwezo mkubwa wa kuogelea. Kila mwisho wa muhula hushiriki kwenye maigizo na mashindano ya quiz. Pia mwaka huu amepata zawadi za masomo mengi ikiwa pamoja na somo la ICT.


‘Microsoft Certified Professional’ ni vyeti ambavyo hutolewa na kampuni ya Microsoft kwa watu ambao wamethibitishwa na kampuni hiyo kuwa na ujuzi katika kutatua matatizo ya programu za Kompyuta, hasa zile zinazotumiwa na watumiaji wa kawaida au wa mwisho (End users) kupitia mifumo ya Windows XP, Vista, Windows7 na zingine kama hizo.

No comments:

Post a Comment