UA-45153891-1

Saturday, October 19, 2013

YALE YA NICK MINAJ YASIMKUTE ROSE MUHANDO

Rose Muhando

SIWAFANANISHI wanamuziki hawa kwa aina za muziki wazifanyazo wala tabia zao, La hasha!. Nazungumzia yanayotokea kwenye mitandao ya kijamii ambayo inatuunganisha bila kujali kazi zetu, vipaji vyetu na imani zetu, maana ubunifu unafanywa na watu tofauti.

Watu maarufu  kama wanamuziki, waigizaji,  wanamitindo, viongozi na wengine ndio wanaoongoza kwa kuwa na wafuasi wengi kwenye mitandao hiyo. Pamoja na hayo ni jambo la kawaida sana wafuasi hao ambao pia ni mashabiki wao kufungua hata akaunti kwa majina yao. Utakuta jina la mtu flani maarufu likiwa kwenye akaunti zaidi ya tano mpaka kumi, lakini yake na anayoitambua ni moja.

Siyo kitu kibaya katika mtazamo wa kupima jinsi gani mtu amepata umaarufu maana shughuri hizo zinahitaji upate umaarufu, ndipo kazi yako inaweza kukulipa zaidi.Japo wengine hufanya hivyo si kwa nia njema bali kwa malengo ya kuharibu majina na watu hao au kujipatia masrahi binafsi. Kikubwa hapa ni uvumilivu na kutoa taarifa kwa vyombo husika yatokeapo mabaya maana kwa ulimwengu wa sasa, ukiamua kuikimbia mitandao hii utawakosa wengi pia.

Mwimbaji wa nyimbo za injili Tanzania, Rose Mhando ambaye  aliwai kusema hana akaunti yeyote ile katika FACEBOOK na watu wanaotumia ni kwaajili ya manufaa yao na sio yeye. Aliwaomba wanaotumia hilo jina kwenye hiyo  akaunti kuacha mara moja na kusema atakapozindua ya kwake ambayo ni ya kweli atawaambia mashabiki wake. Kwa mara nyingine tena hivi punde amesikika akisema kuna matapeli wametumia jina lake kufungua akaunti ya Facebook ya kampuni ya mikopo kwa jina lake na kupelekea watu wengi kumfuata wakitafuta fomu za kuomba mikopo.

Semadat ilipomtafuta Rose muhando kwenye mtandao huo ilikuta jina lake kwa akaunti 5 na kurasa, yaani facebook page 3, kwa jina hilo hilo, bila kujua ipi ni akaunti yake halisi.Kuna changamoto za namna tofauti zinazoweza kujitokeza unapotumia mitandao hii kama mtu maarufu, 'brand' au 'Public figure' maana wakati mwingine hata ndani ya mtandao wako halisi, mashabiki wako wanaweza kukuzungumzia vibaya au kutumia lugha isiyokuwa nzuri.

Mwanamuziki wa Marekani Nick Minaj alijitoa kwenye mtandao wa TWITTER kwa kuifuta kabisa akaunti yake baada ya baadhi ya mashabiki wake wakereketwa kuchukia na kumtukana. Ni baada ya wimbo wake aliotarajia kuuzindua kuvuja kupitia mtandao wenye jina lake pasipo yeye kujua. Hata hivyo alishindwa kuvumilia kuwa nje ya mtandao huo ambao ulimuweka karibu na mashabiki wake, akaamua kurudi Twitter baada ya muda mfupi japo alikuwa tayari amewapoteza wafuasi zaidi ya milioni 11.

Namtakia Rose Mhando uvumilivu katika mitandao ya kijamii maana yeye ni staa ambaye kukubalika kwake kumetokana na kipaji na ubunifu wake mwenyewe na kama yupo kwenye mitandao hiyo,  ambayo kibiashara zaidi inaitwa 'Social Media' badala ya 'Social Networks' aendelee kubaki.


Nick Minaj

No comments:

Post a Comment