UA-45153891-1

Saturday, June 22, 2013

WALTER CHILAMBO NDANI-USIKU WA TUDD THOMAS


Wasanii mbalimbali wa muziki wa Bongo Flava na Hip Hop wameendelea kumuunga mkono Producer Tudd Thomas, mtayarishaji mahiri wa muziki hapa nchini Tanzania ili kunogesha tamasha la usiku wa Tudd Thomas litakalofanyika 30, 2013 ndani ya ukumbi wa Dar Live Mbagala.

Msanii Walter Chilambo ambaye alikuwa mshindi wa Bongo Star Search 2012, atafanya vitu vyake ndani ya tamasha hilo. Mwanamuziki huyo staa wa wimbo wa “Siachi” ameahidi kutoa ushirikiano mkubwa kwenye tamasha hilo na kutoa burudani ambayo itawakonga nyoyo mashabiki wake.

Walter anaungana na wasanii wengine wakali watakaokuwepo ambao ni Diamond, Chegge, Mwasiti, Marlaw, Linex, Scorpion Girls, Linah, Barnaba, Amin, Ally Nipishe, Izzo Business, Baba Levo, Godzilla, Queen Darlin, Recho, Makomando na wegine wengi, Ney wa mitego, Roma na Kala Jelemiah.

Pia watakuwepo wasanii maarufu wa filamu ambao ni pamoja na Elizabeth Michael “Lulu”, Jackline Wolper na Yusuph Mlela na Jack wa Chuz.

No comments:

Post a Comment