UA-45153891-1

Saturday, February 1, 2014

MAISHA YA BEYONCE KUFUNDISHWA CHUO KIKUU

Beyonce alipokuwa mdogo na alivyo sasa

Idara ya masomo ya wanawake na  jinsia  ya Chuo kikuu cha Rutgers nchini Marekani, imeanzisha kozi  inayoitwa “Politicizing Beyonce” ambayo itahusisha mijadala kuhusiana na umaarufu wa jina la mwanamuziki huyo na mchango alionao katika kuwapa nguvu au kuwahamasisha wanawake.

Muhusika wa mpango huo Kevin Allred alisema, kozi hiyo haitamuhusisha Beyonce na mambo ya siasa au ni mara ngapi amefanya maonyesho kwenye mikutano ya Rais Obama bali tu maisha yake kisanii na ushawishi alionao kwa watu wa jinsia yake.

No comments:

Post a Comment