UA-45153891-1

Wednesday, February 19, 2014

2FACE IDIBIA AKANUSHA KUMPA UJAUZITO AFISA WA BENKI


Mwanamuziki wa Nigeria 2Face Idibia amekanusha juu ya habari zilizoandikwa katika Blog na mitandao mingine ya kijamii nchini humo kwamba amempa binti mwingine ujauzito. Mwanadada anayehusishwa na habari hiyo anaitwa Teniola ambaye ni mfanyakazi wa Benki moja nchini humo akitokea eneo la Ado-Ekiti na alisoma chuo kikuu cha Lagos. Inasemekana amekuwa akisimamia kwa karibu akaunti ya 2Face na kumuhudumia kibenki kwa muda mrefu katika benki hiyo na 2face alitaka ujauzito huo wa miezi mitatu uondolewe akimuomba kwa ahadi ya kumnunulia gari jipya ili mambo yaishe chini kwa chini pasipokujulikana.

2face amekanusha na kusema taarifa hizo ni uongo kwa asilimia 100,huku akilaani na kueleza hisia zake kupitia mtandao wa Twitter.



No comments:

Post a Comment