UA-45153891-1

Tuesday, February 18, 2014

SIKU YA KUZALIWA DR. DRE....!!!

Dr. Dre
Ukimwambia mtayarishaji yeyote wa muziki ulimwenguni akutajie watu wawili anaowatazama ili  kupata hamasa ya kufika mbali, ni jambo la kawaida kumtaja Dr. Dre akiwa wa kwanza . Kwa jina halisi anaitwa Andre Romelle Young na alizaliwa February 18, 1965.

Ni mtayarishaji wa muziki ‘Producer’ maarufu nchini Marekani na dunia nzima, pia ni rapper, mwanzilishi na CEO wa makampuni ya Aftermath Entertainment na Beats Electronics. Biashara yake ya ‘Headphones’ imemtangaza sana pande mbalimbali za dunia.


Huwezi kuwazungumzia wanamuziki kama Snoop Dogg, Eminem, Xzibit, 50 Cent, The Game na  wengine wengi wa zamani na wasasa akiwemo Kendrick Lamar, bila kumzungumzia yeye pia. Pia anaungana na mwanamuziki mwingine wa Marekani Juelz Santana aliyezaliwa February 18, 1982 katika kusherehekea siku hiyo ya kuzaliwa.


Juelz Santana

No comments:

Post a Comment