UA-45153891-1

Monday, February 17, 2014

'WANURI KAHIU' MUONGOZAJI WA FILAMU ALIYESIMAMA JUKWAA MOJA NA BILL GATES


Mwanadada 'Wanuri Kahiu' ambaye ni muongozaji na mtayarishaji wa filamu, aliwawakilisha vizuri wakenya na wanaafrika  mashariki kwa kupata nafasi ya kuzungumza kwenye tukio la TED-X. Alizungumza juu ya filamu yake ya Pumzi, uzoefu wake katika msuala ya filamu na jinsi anavyojisikia juu ya 'Label' anazofanyia kazi.
Ted-x ni tukio ambalo lengo lake  ni kuwakutanisha watu katika kongamano ili kufurahia kile ambacho waandaaji walikipa jina la "Ted-like experience". Hapa watu mbalimbali maarufu na wenye mchango mkubwa katika maendeleo duniani, katika nyanja tofauti ikiwa pamoja na za kiutawala, hupata dakika 18 za kuzungumza ili kubadilishana mawazo na wengine.Waliokuwa kwenye tukio hilo ni pamoja na Kiongozi Microsoft  Bill Gates, Makamu wa Rais wa Marekani mstaafu Al Gore na Waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown.

Wanuri Kahiu aliyetayarisha filamu ya 'Still Life' mwaka 2005, ameshapata tuzo nyingi na kushindanishwa kwenye vipengele vya tuzo mbalimbali za filamu alizoziongoza kama vile 'Best Director', 'Best Screenplay' na  Best Picture'kwenye tuzo za  'African Movie Academ'.Filamu yake ya 'From a Whisper' iliingizwa katika ushindani wa tuzo 12 na kuchukua tuzo tano (5) katika tuzo hizo mwaka 2009.


Alizaliwa jijini Nairobi nchini Kenya na baada ya kumaliza masomo yake katika chuo kikuu cha Warwick mwaka 2001, ambapo alihitimu 'degree' ya 'Management Science', aliendelea na  'Masters' ya  'Fine Arts in Directing' katika kitivo cha Filamu na Televisheni, chuo kikuu cha California.

No comments:

Post a Comment