UA-45153891-1

Tuesday, February 25, 2014

OMOTOLA APEWA SOMO NA WANAHABARI NCHINI NIGERIA

Omotola Jalade

Siku chache zilizopita, mtoto wa muigizaji wa kike maarufu nchini Nigeria Omotola Jalade-Ekeinde alisherehekea siku ya kuzaliwa  na kuweka baadhi ya picha zake kwenye mtandao wa Instagram.  Blogger s wa nchini humo walizichukua picha hizo za mtoto wa miaka 14 anayeitwa Meraiah Ekeinde na kuziweka kwenye Blog zao ikiwa pamoja na kuzizungumzia. Kupitia mtandao wa Facebook, Omotola aliwashukuru  waandishi hao kwa kumtakia mwanae furaha ya siku ya kuzaliwa ingawa pia aliwaonya na kukemea kitendo cha  kutumia picha za mtoto mdogo hasa wale ambao  walioandika maneno “hot and sexy”. Hivi ndivyo alivyoandika kwenye ukurasa wake wa Facebook, pia sehemu ya barua ya wazi aliopewa na mmoja wa waandishi wa habari za burudani mitandaoni nchini Nigeria, anayeitwa . Osagie Alonge.

Mwandishi anasema,
“Inabidi utambue kwamba katika muda ambao picha za mwanao zilionekana kwenye hizo Blogs, tayari zilikuwa kwenye akaunti ya Instagram ya mwanao, kwa hiyo zilikuwa wazi kwa kila mtu. Ndugu Omotola, napenda kukwambia  kwamba vyombo vya habari  havijafanya lolote baya la kufanya viombe ladhi kwako kwa kuweka picha za mwanao mtandaoni. Kiukweli inaonyesha umeshindwa kumlea vizuri mtoto wako”.

Anaendelea kueleza  yaliyomgusa,
“Mwanao Meraiah  yuko katika hatua za awali za ujana, kwanini hajaambiwa lolote kuhusia na matumizi ya mitandao hiyo hasa upande wa uwekaji wa picha na maneno ya kikubwa tena kwa kuyapa ‘hashtags’ kama #StaySexy?. Kwanini umeshindwa kuelewa kwamba mtoto huyu hana biashara kama yako mpaka unamuacha anaweka picha zenye mwonekano kama wa waigizaji wenzako wa Nollywood?.”

Hakuishia hapo,
“Badala yake  unachagua kusema kwamba  yalioandikwa na wanahabari yamekuumiza wewe na baba wa mtoto wako, na kuwahukumu kwa kuingilia mambo binafsi ya mtoto wako ambaye ni mdogo kiumri, umekosea sana. Ni jambo la aibu kwamba mpaka sasa unapolaumu, picha hizo bado hazijatolewa kwenye mtandao huo, ni jambo la aibu pia kwamba unawanyooshea vidole wanahabari  wakati wewe bado hufanyi yanayostaili”, Ni baadhi ya yaliyoandikwa kwenye barua ya wazi ya  mwandishi huyo.

No comments:

Post a Comment