Neno mvuto lina maana pana sana. Wasichana na wanawake wazuri wako kila kona ya dunia,hata hivyo wenye mvuto zaidi na ushawishi katika jamii mara nyingi ni wale wenye kujituma, kufanya kazi kwa bidii kwa uwezo wao, ujuzi walionao na vipaji walivyopewa. Ndiyo maana haikuwashangaza watu pale muigizaji wa Hollywood anayetokea nchini Kenya Lupita Nyong'o alipowekwa kwenye orodha ya mtandao wa "AskMen.com" akiwa miongoni mwa wanawake 99 wenye mvuto na ushawishi mkubwa dunianim mwaka huu 'Most desirable women 2014'.
Mtandao huo hutoa orodha hiyo kila mwaka kwa kuzingatia mambo mengi ikiwa sio tu muonekano bali pia mafanikio katika shughuri zinazofanywa na wanawake hao pamoja na upeo wao. Lupita amekuwa wa #22 akiwa mbele ya majina makubwa sana ulumwenguni kama Miley Cyrus, Kate Winslet, Katy Perry, Selena Gomez, Kim Kardashian, Zoe Saldana, Sandra Bullock, Kate Middleton na Taylor Swift.
Itakumbukwa pia kwamba mwishoni mwa mwaka jana alitangazwa na jarida la Forbes akiwa miongoni mwa wanawake 20 wadogo wenye nguvu kwa mtazamo wa mafanikio wanayoyapata katika ujasiliamali, uongozi, n.k. Siku chache zilizopita mwaka huu 2014 alitajwa kwenye tuzo za Academy. Ameshaingia kwenye tuzo za filamu za Oscar kipengele cha 'Best Supporting Actress' na ametajwa na majarida kadhaa ya mitindo kama mtu mwenye uwezekano wa kufanya vizuri sana katika fani hiyo pia, ndani ya mwaka 2014.
No comments:
Post a Comment