UA-45153891-1

Monday, February 24, 2014

KWANINI FACEBOOK WAMEINUNUA WHATSAPP KWA DOLA BILIONI 19?

CEO wa Whatsapp Jan Koum

Mnamo  Februari 19, 2014, Facebook walitangaza kuinunua Whatsapp kwa  kiasi cha dola bilioni 19, ambapo  WhatsApp kama yenyewe ni  $16 bilioni na $3 billioni kwa ajili pia ya kuwachukua wafanyakazi  wake. Jina la mtandao huo halitabadilika na utaendelea kufanya kazi kwa kujitegemea  lakini chini ya uongozi wa Facebook. CEO wa Whatsapp  Jan Koum ambaye pia ni mmoja wa waanzilishi wa mtandao huo  amekuwa mmoja wa wajumbe wa bodi ya kampuni ya Facebook Inc.

Mitandaoni na kwenye vyombo vingine vya habari iliibuka mijadala ukiwemo wa  kwamba, Je kweli mtandao huo wa kijamii ulioanzishwa na Jan Koum na Brian Acton ulikuwa na thamani ya kununuliwa na Facebook kwa kiasi hicho cha fedha?.  Jibu rahisi kwa walio wengi ni “Hapana”, japo inaweza kuwa kinyume na hivyo au ikawa ni hivyo leo lakini kwa faida ya kesho. 

Zifuatazo zilikuwa  sababu za Facebook kuununua mtandao huo.


1.    Kihistoria ndiyo mtandao uliokua kwa kasi kuliko yote
Mpaka sasa una watumiaji zaidi ya milioni 450 na idadi hiyo imefikiwa haraka na Whatsapp kuliko mtandao wa kijamii wowote ule. Hii ina maana kwamba mitandao mingine imefikisha idadi hiyo baada ya muda mrefu zaidi tangu ilipoanzishwa.

 2 . Mtandao unaopata faida kubwa yanapolinganishwa mapato na matumizi yake
Gharama za uendeshaji ni ndogo, kwa mfano upande wa wafanyakazi,  pamoja na kuwa miongoni mwa mitandao yenye viwango ulimwenguni  mwandisi wake mmoja kwa wastani anahudumia watumiaji milioni 14 na kwa ujumla una wafanyakazi 55 tu mpaka sasa wanaoshughurika na meseji zaidi ya  bilioni 50 kwa siku.

3.    Utofauti wa mtandao huo  kwa washindani wake wa moja kwa moja ‘Mitandao ya Apps’
Ni mtandao uliohamua kufanya jambo moja kwa taaluma na uzoefu wa ujumbe mfupi. Hakuna matangazo wala kitu kingine kinachoonekana bali tu ujumbe  toka mtumiaji mmoja kwenda mwingine ambapo namba ya simu ndiyo inayotumika kufanya usajiri. Wakati Facebook ikitaka kununua mtandao wa aina hiyo ilichunguza zaidi ya mitandao mingine 12 inayotoa huduma hiyo ambapo mingine yote inahusika pia na mambo mengine ikiwa pamoja na matangazo.

4.     Whatsapp  ni mtandao unaojiuza
Ni mtandao ambao pamoja na kukua kwa kasi hivyo, haujawekeza au kutumia nguvu yoyote katika kujitangaza. Hakuna mtu aliyeajiriwa Whatapp kama meneja, mkurugenzi wala afisa mtendaji mkuu  wa Masoko au Uhusiano (PR) wala kuweka nembo yao nje ya ofisi yao tofauti na mitandao mingine ya aina hiyo ambayo inaitwa ‘Apps’. Wachache waliotumia ndiyo waliowashauri ndugu, jamaa na marafiki zao kutumia.

5.    Kuendeleza na kuongeza familia
Kuna watu wako Facebook muda mrefu lakini hawana matumizi nayo zaidi ya upande wa kutumiana ujumbe mfupi wa maneno. Whatapp ilikuwa ndiyo chaguo mbadala kwao hasa pia baada ya kugundua hauhitaji hata kujisajiri kwa jina wala barua pepe. Facebook haikuwa tayari kuwapoteza. Hii ni kama ilivyokuwa kwa Instagram kununuliwa na Facebook  $1 bilioni ili wanaopenda kuonyesha picha na video badala ya kuandika, hata wakienda huko bado ni wa Mark Zukerberg.
 CEO wa Facebook Mark Zukerberg.

No comments:

Post a Comment