UA-45153891-1

Friday, February 21, 2014

UMASOGANGE NI AJIRA NZURI KINADADA WAKITUMIA FURSA VIZURI


 Agnes Gerald ‘Masogange’

Baada ya kukutana na  habari flani mtandaoni, mwanamuziki wa Bongo Flava Khalid Ramadhani a.k.a Tundaman akiliambia gazeti la Starehe kwamba warembo wanaotumika katika video zake kama 'video vixens' au kwa hapa Bongo maarufu kama ‘video queen’ wengi huwa anaelewana nao tu kwani ni wachache huwalipa ujira na wanaolipwa ni pesa kidogo isipokuwa Agnes Gerald ‘Masogange’ aliyehusika katika video ya Msambinungwa, ndipo 'Semadat Blog' ikatumia neno 'umasogange' kuwakilisha fani hiyo.

“Katika video zangu zote hakuna video queen niliyewahi kumlipa zaidi ya milioni moja ila Masogange nimemlipa shilingi......
1.5 milioni na nimemgharimia kila kitu kiasi kwamba gharama yake ni zaidi ya milioni mbili. Ukweli ni kwamba wasichana wengi ninaowatumia katika video zangu nimekuwa nikiwanunulia nguo, viatu, kuwapeleka saluni na kununua nywele za bei ghali kwa ajili yao, lakini wengi tunasaidiana yaani ni ‘ushkaji’ zaidi; mara nyingi huwa siendi kuwachukua kiofisi.” Alisema Tundaman.

Bila shaka hata hao wanaolipwa kidogo au wasiolipwa kabisa si kwamba wote hawana sifa bali pengine ni kuanza kwa kukuza majina yao kwa kuonyesha umairi wao ili baadae waanze kutengeneza pesa kupitia 'umasogange'. Mwanadada Agness alianza kupata umaarufu kupitia video ya muziki aliyoitendea haki ya mwanamuziki Belle9, ya wimbo unaoitwa Masogange ambayo ndiyo iliyomuachia jina hilo.



No comments:

Post a Comment